Habarini Wanajukwaa,
Mbunge wa Mbinga Vijijini Ndung Martin Msuha kwasasa yupo katika hatari kubwa ya kupoteza jimbo hilo la Mbinga vijijini, Mnyetishaji aliepo Mbinga vijijini ameeleza kuwa Tangu aingie ndugu msuha hakuna cha maana alichofanya zaidi ya kwenda bungeni na kupumzika hata pale baadhi ya wanambinga walipomfuata huko kuomba msaada wa mambo ya kitendaji jimboni amekuaa akiwajibu kwa dharau sana, ni hivi mwaka jana tu ndugu msuba alialikwa kwenfa kuchangia hospital ya mikalanga aliishia kuahidi(na sio kutoa)/50,000(Elfu Hamsini), hii ni hatari hasa kwa kiongozi kama yeye alieaminiwa na wananchi kushindwa saidia hospitali iliyowasaidia na inayowasaidia watu wengi w bonde la agati..
Sasa mbunge amekumbuka shuka pakiwa pamekucha hali yake ya kiuongozi ni mbaya na anahofu ya kutorudi tena.
Zaidi ya hayo ndugu Dr.John Ndunguru anazungumziwa sana na watu waliowengi kuwa mrithi wa jimbo hilo ila zaidi kuna vijana wengi wasomi wakimatengo wanatafsirika sana na wanazungumzwa sana midomoni mwa wanambinga kijijini wengi na wanashawishiwa sana warudi wasaidie kupush baadhi ya mambo kwa imani kuwa vijana ndo taifa la sasa na la baadae..Kijana mapunda aliepo bodi ya mikopo, kijana Ndunguru(mkulima), kijana Ndunguru( huyu mwanaharakati wa muda mrefu chuo kikuu cha Dar es salaam), Kijana Kapinga(mwalimu), Meneja wa kiwanda cha kahawa hapo.Mbinga..
Hali imekuwa ngumu sana hapo jimboni, vijana hao wanasikika na kusemwa semwa midomobi mwa wanambinga walio wengi lakini mwisho wao ndio wenye maamuzi ya kuwasaliti ndugu zao au kwenda kuwakomboa ndugu zao.
Yetu Macho!!! Vita vya panzi ziumiazo Nyasi.
Mwisho Tunataka wajasiri na wapambanaji Mbinga watakaoweza vusha Mbinga yetu toka ilipo kwenda sehemu nyingine.