Kuendelea kumtaja Hayati Magufuli kwa mabaya ni upuuzi wa ajabu

Kuendelea kumtaja Hayati Magufuli kwa mabaya ni upuuzi wa ajabu

Usipojua historia basi tambua kuanzia Leo Ina tabia ya kujirudia.

Tunasoma, hadithiwa na kuambiwa maisha ya wanadamu waovu waliopita ili tusitende uovu huo kwa kizazi Cha Sasa na kijacho.

Mwovu haachi kunenwa na Walimwengj kama ilivyo kwa Watenda mema
Shetani
Firahuni
Mwanaharamu Mwendazake
Hitler
Jean Bedell Bokasa
Nduli Dada Amin
Mobutu
Genghis Khan
Ivan the Terrible
Japanese Emperors
Belgium King
Mtema Kuni

Na wengineo wenye daraja hilo
 
Kwa akili yako na uwezo wako wa kufikiri; ukifanya comparison analysis kwanini ikiwa Kuna awamu zilizopita na zilifanya maovu kwanini hayati alaumiwe Sana kuliko watangulizi wake!

Ukweli Ni kwamba alifika the highest degree of impunity Katika Mila na desturi za maisha ya watanzania. He was everything.

Umeandika vyema kwamba so vyema watu kumwit shetani yule. Hata Mimi siungi mkono kumuita binadamu shetani. Lakini unakumbuka kauli yake mwenyewe kwa kinywa chake mwenyewe kwamba anatamani matajiri waishi Kama mashetani? Na kweli matajiri wakaanza kukiona Cha maoto ikiwemo utitiri wa kesi zilizoitwa za uhujumu uchumi? Hakuwahi hata siku moja kujitenga na matendo maovu yakiyokua yakitendeka isipokua alitoa zawadi ya vyeo na madaraka kwa waliyofanya matendo hayo maovu.

Unakumbuka as watendaji waliokufa chini yake walipomfananisha na Mungu na Wala hakuwahi kukataa isipokua alisema anatamani kuwa siku Moja akifa aende mbinguni kuongoza malaika hata sio wateule wa Mungu? Huoni Kama hiyo Ni kufuru?

Kuna mkuu mmoja wa mkoa alisema bila aibu mbele za umma kwamba Mungu amshukuru Magufuli kwa kuiondoa corona! Magufuli hakuwahi kutoka hadharani kukataa Hilo Wala kuonesha kutokufananishwa na Mungu! Maandiko yanatuambia Mungu alimwadhibu Lucifer kwa sababu alitaka kusujudiwa Kama Mungu(Mungu Ana wivu na Hilo amelionesha katika maandiko)

Tumeshakataa kabisa kumhusisha Magufuli na kushambuliwa kwa TAL. Lakini kiuhalisia Rais ndio Amiri Jeshi Mkuu wa vyombo vya ulinzi na Usalama. TAL aliposhambuliwa wanachama wake waliojitokeza kumuombea walikutana na mkono wa polisi mpaka makanisani. Hakuwahi kujitenga na matendo hayo. Ama hata tu kwa kuongea hadharani. (Alifurahia)

Akiweka Jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya kimara kibaha aliviambia vyombo vya habari "you are free but not to that extent" akalenga specifically Mwananchi Newspaper muda mfupi tu Azory Gwanda akapotea na maelezo ya mke wake Ni watu wa serikali! Utawala wake ulikaa kimya kimya na hakuwahi kujitenga na matendo hayo. Mpaka waziri bwana Kabudi aliponukuliwa alisema kuwa "amekufa"

Alitumia Jeshi kudhulumu Korosho za wamakonde; kila walipodai haki yao kwa mujibu wa Sheria alijitokeza hadharani mwenyewe na kumwambia PM iwapo wataandamana ataanza na shangazi zake kuwapiga virungu (udhalilishaji na ubabe)

Sote tunajua kwamba Tanzania Ni nchi ya vyama vingi inayoheshimu utawala wa Sheria na demokrasia. Alitamka wazi wazi kwamba siwezi kukupa mshahara nyumba na gari halafu umtangaze mpinzani ameshinda uchaguzi! Kauli yake ilikua nzito na mwangwi wake ulionekana kwenye chaguzi mbili mfululizo (mitaa na uchaguzi mkuu) Kuna watu wanaachiliwa huru hivi Sasa na Mahakama za Rufani kwa kubambikiwa kesi za mauaji. Hakuwahi kujitenga na Mambo haya hata siku moja isipokuwa aliwazawadia vyeo kina Mahera na wenzake! Alienda mbele kuwafananisha binadamu wenzie na magunzi! Kwamba ukichanganya betri na magunzi haviwaki na kutamka wazi kwamba msipochagua CCM sileti maendeleo!

Bomoa bomoa ya kimara hakuna atajayeishahu shida Ni kwamba alipokua mwanza alitamka hadharani kuwa wale was mwanza walimpigia kura kwahiyo wasibomolewe huo Ni ubaguzi wa wazi wazi usiotilia Shaka.

Mambo Ni mengi Sana ukiyaandika hayaishi Wala kitabu hakitatosha!
Alikua na mazuri yake lakini maovu yali-outshine mazuri yake! Kwakua aliwaongoza watu waacheni waseme ili viongozi wajao wajifunze kuwa mabaya au mema ya mtu huambatana nae. Kifo hakikupi Kinga ya kujadiliwa kabisa.
Adious
Siku ambayo Watanzania wataujuwa ukweli halisi ni nani alimpiga bastora Kwa mkono wake Ben Saanane na kumpoteza kwenye pipa la acid basi hawa mbwa wote wa shetani wa Kirundi wataomba Ardhi ipasuke.
 
Anaandika, Robert Heriel

Sikuwa mshabiki wa Magufuli Kutokana na namna alivyokuwa anaongoza, sisemi Kuwa Magufuli hakuwa na mambo Mema aliyoyafanya, yapo mengi mazuri Sana hasa ya miundombinu, lakini pia yapo Mabaya ambayo aidha aliyafanya au kuyafumbia macho, ambayo ndio yalinifanya nimuone kama kiongozi asiyefaa.

Ninashangazwa na kile kinachoendelea hasa Kwa upande wa Upinzani kuendelea kumtaja taja MTU ambaye tayari anasiku nyingi ameshafariki.

Wabaya Waliohai wapo wengi, Kwa nini mhangaike na Watu waliokwisha Kufa wasio na chochote cha kuchangia katika Ulimwengu wa Waliohai? Wema Waliohai pia wapo wengi.

Hatuwezi kuongoza nchi Kwa kuangalia Wafu, na hatutataka nchi yetu iongozwe na watu wenye mawazo na Matendo ya Wafu.

Tunahitaji viongozi ambao wanaongoza nchi Kwa kuangalia Maisha ya kizazi kijacho kitaishije,
Nchi inaongozwa Kwa mahitaji yajayo sio mahitaji yaliyopita. Nchi inaongozwa Kwa maslahi ya Watu wa kesho sio Kwa maslahi ya Watu wa Jana na juzi waliokwisha Kufa.

Wanaoishi Wasiwe watumwa wa Wafu, Watu waliokwisha Kufa. Hivyo ndivyo taifa hili linapaswa kujengwa na kuongozwa. Kwa sababu tunaenda Mbele na sio Nyuma.

Sijui Fulani alikuwa Nani akasema nini, hiyo haina maana yoyote Kwa wakati au kizazi kijacho, kitakachoangaliwa ni manufaa ya kizazi kijacho.

Hata Mungu tunayemuabudu ni MUNGU aliyehai na Mungu wa Waliohai sio Mungu wa Wafu.

Wanasiasa mnaomtaja taja Magufuli Kwa ubaya mnayohaja ya kujitafakari, kama mnaagenda zenu za Siri Sawa lakini eleweni kuwa haitasaidia Jambo LOLOTE lile.

Acha nipumzike SASA.

Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Makanya, Same, Kilimanjaro.
Kwa hiyo unashauri somo la historia lifutwe mashuleni badala yake wafundishe unajimu
 
Mkuu hii barua yote unarudia kueleza mabaya ya Magufuli, huu uzi unahoji kwamba huku kulala na kuamka kutwa kuzungumzia mabaya ya Magufuli inatuletea faida? Toka Magufuli afariki hadi leo karibu miaka miwili bado tu tunaeleza mabaya ya Magufuli kama bado yupo hai, shabaha ya kufanya hivi ni nini au ndio kupunguza tu hasira?
Kwani wewe UHURU JR unalazimishwa kuisoma hiyo barua ndefu? Shabaha ya kuendelea kuandika mabaya ya magufuli kwa miaka miwili ni kuwafahamisha Wajinga waliodanganywa na magufuli mwenyewe kuwa alikuwa "mzalendo". Kumbe likikuwa Jizi na muuaji wa wakosoaji
 
wanaomtaja makufuli vibaya wanaasili ya ushoga
Kwahiyo unaona umeandika Jambo la maana kabisa ambalo watasoma wenye akili timamu na kuelewa?

Hata wanaopinga Magufuli kusemwa vibaya wanakuona mpumbavu usiyekua na chembe ya hekima linapokuja swala la public speaking!

Kama kwa utambuliaho (ID) fake umeweza KUANDIKA hivi. Itakuaje pale unapozungumza mbele za watu! Tangu lini ushoga ukawa Ni asili badala ya kuwa ama urafiki kwa wanawake au tabia na mwenendo mbaya kwa wanaume?

Jaribu kujenga hoja ya kumkingia kifua Magufuli badala ya kujenga Mazingira ya yeye kuendelea kusemwa kwa matendo yake mabaya na sio kusemwa vibaya! Kuna tofauti kubwa Sana Kati ya kusemwa vibaya na kusema matendo mabaya ya mtu ili watu wajifunze na wasiyarudie kabisa.
 
Kwa hiyo inashauri somo la historia lifutwe mashuleni badala yake wafundishe unajimu
Nadhani wanataka kutudharaulisha Kama Mwigulu anavyosema tusijadili kuhusu uchumi unao tuhusu sisi tujadili uganga wa kienyeji! Utadhani Magufuli alitawala watu wengine na sio sisi!
 
Huyo Magu aka Mwendazake tutaendelea kumtaja sana tu kwa kila baya ambalo amefanya Tanzania. Tunawaomba masalia yake mliobaki muendelee kuvumilia tu.
 
Kwani historia inasomwa kwa manufaa gani? Ukijua umuhimu wa historia nadhani utakuwa umeshapata jibu la swali lako.
Mnamlaani na kumwita shetani mara sijui kafa kwa corona mara sijui Mungu kaamua ugomvi, wengine huko wanafukua makaburi kwa kumsema kwa mafumbo sasa hapo kuna lipi la kujifunza?

Tungekuwa tunajadili yapi alikosea na wapi alipatia, wapi alitakiwa kufanya hivi na vile hapo kweli ningeona la kujifunza ila haipo hivyo mtu anakwambia et hayo mazuri eleza wewe na mie naeleza mabaya tu.
 
Kwani wewe UHURU JR unalazimishwa kuisoma hiyo barua ndefu? Shabaha ya kuendelea kuandika mabaya ya magufuli kwa miaka miwili ni kuwafahamisha Wajinga waliodanganywa na magufuli mwenyewe kuwa alikuwa "mzalendo". Kumbe likikuwa Jizi na muuaji wa wakosoaji
Ok wakishajua alikuwa mwizi na muuwaji halafu ndio nini? Kwa sababu kabla ya Magufuli walikuwepo majizi na miuwaji ila hakuna walichofanywa, sasa hao wajinga wakishajua kama mnavyojua nyinyi kwamba marehemu(hayupo tena) nae alikuwa mwizi na muuwaji kama wengine ndio tunafaidika nini kama taifa?

Tufanye mkafanikiwa kuwashawishi watu wote kuona kwamba Magufuli hakufanya zuri hata moja yote mabaya, baada ya hapo ndio mtakuwa mmefanya kipi cha maana au inakuwa mmemshinda marehemu?
 
Huyo Magu aka Mwendazake tutaendelea kumtaja sana tu kwa kila baya ambalo amefanya Tanzania. Tunawaomba masalia yake mliobaki muendelee kuvumilia tu.
Ni akili ya ajabu kudhani kwamba watanzania wote wamegawanyika makundi mawili tu kwamba kuna wanamsifia Magufuli na kuna wanaomchukia Magufuli.
 
Ok wakishajua alikuwa mwizi na muuwaji halafu ndio nini? Kwa sababu kabla ya Magufuli walikuwepo majizi na miuwaji ila hakuna walichofanywa, sasa hao wajinga wakishajua kama mnavyojua nyinyi kwamba marehemu(hayupo tena) nae alikuwa mwizi na muuwaji kama wengine ndio tunafaidika nini kama taifa?

Tufanye mkafanikiwa kuwashawishi watu wote kuona kwamba Magufuli hakufanya zuri hata moja yote mabaya, baada ya hapo ndio mtakuwa mmefanya kipi cha maana au inakuwa mmemshinda marehemu?
Samahani nitakua nje ya Mada kidogo:

Mashaka yangu Ni kwenye umri wako na uwezo wako wa kujadili Mambo yanayohusu umma critically(kwa kuhoji na kujihoji)

Taifa lazima litafanikiwa kwa maana ya kwamba, kwa madhara aliyoacha negatively watu ambao wanatamani au watakaopewa dhamana ya uongozi katika taifa hili hawatarudia makosa hayo in the future na Tanzania pataendelea kuwa mahala salama pa kuishi.

Niliandika Jana Kama ulisoma vizuri . Magufuli hakuwahi kujitenga na matendo maovu yaliyofanyika chini ya utawala wake kwa mwamvuli wa UZALENDO!

Kama awamu zilizopita zilifanya maovu yalikemewa hivi hivi hadharani. Na Ni nafasi yako Sasa kubainisha kwamba wakati wa JKN, AHM, BEN na JK kulikua na uovu gani ulio-outshine mazuri ya serikali!

Two wrongs can never make it right! Kama yalifanyika makosa wakati wa nyuma sio tiketi ya kuendelea kufanya makosa ndio Samia Mwenyekiti wa Chama chako anafaya marekebisho ili Mambo hayo yasijiruddie!

Kama unasoma historia utaona Ni dhahiri kwamba historia inatusaidia kujua wapi tumetoka, tulipo na tunapotaka kwenda!

Ukweli Ni kwamba hatujasema hakufanya lolote jema Ila mema yake sio sababu ya kukataa kujitenga na uovu uliofanyika chini ya utawala wake na akakataa kutoka hadharani na kuukemea! Lugha magizo kutoka juu ilitamalaki Sana enzi zake!

Na kwa taarifa yako sio watanzania wote wataokukubali yule jamaa alikuwa mwovu kuliko mtawala yeyote aliyewahi kuitawala TANZANIA. Ikiwemo wewe hautakubali. Kwahiyo usiwe na hofu.

Wakati watu wanakazana kueleza maovu yake nadhani na wewe ungetumia nguvu kubwa kutangaza mema yake!

Kabla ya kuonesha mapenzi binafsi zingatia public interests halafu uweke mizania! Vinginevyo utaumia Sana na yeye alishakufa Ni mzoga hakusikii Wala haoni ukimtetea!
 
Shabaha ya kufanya hivi Ni:
1. Viongozi waliopo na watakaokuwepo wajue kwamba uongozi Ni dhamana na watu walioko chini yao wapaswa kuongozwa kwa haki na usawa bila ubaguzi wa namna yoyote ile.

2. MAMA TANZANIA Ni Mali ya watanzania wote hivyo kila mtu ana haki katika Jamhuri kwa mujibu wa Sheria tulizojiwekea wenyewe na Tanzania sio Mali ya mtu mmoja ajiamulie atakavyo Kama Yuko kwenye familia yake au geto kwake.

3. Kifo sio KINGA ya kutokusemwa mabaya ukiyotenda ukiwa hai hivyo matendo ya mtu yataambatana nae vizazi na vizazi yakiwa mema sawa yakiwa mabaya sawa. Sisi wakristo matendo ya watawala na watu waovu yanerkodiwa barabara katika kitabu kitakatifu ili binadamu tujifunze kupitia hayo! Ingekua kifo kinatoa Kinga ya kutosemwa Basi habari Za Nebukadneza na Faraoh au Herode zisingeandikwa kamwe!

4. Na nikwambie hakuna mtu ana chuki binafsi na Magufuli, kwa sababu alikua mtawala wa Jamhuri na sio kiongozi wa familia ya mtu awaye yeyote, watu Wana chuki na tabia zake mbaya, hulka yake mbaya na mfumo mbaya aliouasisi ambao Ni kinyume na Mila na desturi zetu sisi watanzania!
Tokea muanze kueleza mabaya ya Magufuli kwa muda wote huu wa karibu miaka miwili mnaona mnaelekea vizuri kwenye hiyo shabaha yenu? Tunaona viongozi ambao nao wanashiriki kueleza mabaya ya huyo Magufuli lakini wakati huo unaona nao wanalalamikiwa kwa viburi na kuweka mbele masilahi yao binafsi kuliko ya wananchi.

Kinachoendelea ni kuaminishana kuwa uovu Tanzania ulianza kwa Magufuli na kuishia kwa Magufuli.
 
Wataje kwa majina acha kuelea hewani bwana Mzee JF Ni GT forum!
Tokea muanze kueleza mabaya ya Magufuli kwa muda wote huu wa karibu miaka miwili mnaona mnaelekea vizuri kwenye hiyo shabaha yenu? Tunaona viongozi ambao nao wanashiriki kueleza mabaya ya huyo Magufuli lakini wakati huo unaona nao wanalalamikiwa kwa viburi na kuweka mbele masilahi yao binafsi kuliko ya wananchi.

Kinachoendelea ni kuaminishana kuwa uovu Tanzania ulianza kwa Magufuli na kuishia kwa Magufuli.
 
Samahani nitakua nje ya Mada kidogo:

Mashaka yangu Ni kwenye umri wako na uwezo wako wa kujadili Mambo yanayohusu umma critically(kwa kuhoji na kujihoji)

Taifa lazima litafanikiwa kwa maana ya kwamba, kwa madhara aliyoacha negatively watu ambao wanatamani au watakaopewa dhamana ya uongozi katika taifa hili hawatarudia makosa hayo in the future na Tanzania pataendelea kuwa mahala salama pa kuishi.

Niliandika Jana Kama ulisoma vizuri . Magufuli hakuwahi kujitenga na matendo maovu yaliyofanyika chini ya utawala wake kwa mwamvuli wa UZALENDO!

Kama awamu zilizopita zilifanya maovu yalikemewa hivi hivi hadharani. Na Ni nafasi yako Sasa kubainisha kwamba wakati wa JKN, AHM, BEN na JK kulikua na uovu gani ulio-outshine mazuri ya serikali!

Two wrongs can never make it right! Kama yalifanyika makosa wakati wa nyuma sio tiketi ya kuendelea kufanya makosa ndio Samia Mwenyekiti wa Chama chako anafaya marekebisho ili Mambo hayo yasijiruddie!

Kama unasoma historia utaona Ni dhahiri kwamba historia inatusaidia kujua wapi tumetoka, tulipo na tunapotaka kwenda!

Ukweli Ni kwamba hatujasema hakufanya lolote jema Ila mema yake sio sababu ya kukataa kujitenga na uovu uliofanyika chini ya utawala wake na akakataa kutoka hadharani na kuukemea! Lugha magizo kutoka juu ilitamalaki Sana enzi zake!

Na kwa taarifa yako sio watanzania wote wataokukubali yule jamaa alikuwa mwovu kuliko mtawala yeyote aliyewahi kuitawala TANZANIA. Ikiwemo wewe hautakubali. Kwahiyo usiwe na hofu.

Wakati watu wanakazana kueleza maovu yake nadhani na wewe ungetumia nguvu kubwa kutangaza mema yake!

Kabla ya kuonesha mapenzi binafsi zingatia public interests halafu uweke mizania! Vinginevyo utaumia Sana na yeye alishakufa Ni mzoga hakusikii Wala haoni ukimtetea!
Tatizo kwenye mada za kuhusu Magufuli sijui kwa nini huwa mnapenda kuwaweka watu kwenye makundi mawili tu kwamba kuna wenye kupenda kuona yanaelezwa mabaya tu ya Magufuli na wasiopenda kuona yanaelezwa mabaya ya Magufuli? Hii mada inahoji tunafaidikaje kwa kutumia muda mwingi kueleza mabaya ya Magufuli kuliko hata mabaya yanayotendeka sasa? Hivyo ni kujadiliana katika hilo ila kwa bahati mmetafsiri kama labda mnataka kuzuiliwa msieleze mabaya ya Magufuli.

Kama tutaendelea kutengeneza huu mvutano wa kwamba et wewe eleza mazuri kama yapo na mie nitaeleza mabaya tu basi sidhani kama tutafaidika na lolote kwenye hii mijadala, hii ni sawa na ushabiki wa Simba na Yanga.
 
Anaandika, Robert Heriel

Sikuwa mshabiki wa Magufuli Kutokana na namna alivyokuwa anaongoza, sisemi Kuwa Magufuli hakuwa na mambo Mema aliyoyafanya, yapo mengi mazuri Sana hasa ya miundombinu, lakini pia yapo Mabaya ambayo aidha aliyafanya au kuyafumbia macho, ambayo ndio yalinifanya nimuone kama kiongozi asiyefaa.

Ninashangazwa na kile kinachoendelea hasa Kwa upande wa Upinzani kuendelea kumtaja taja MTU ambaye tayari anasiku nyingi ameshafariki.

Wabaya Waliohai wapo wengi, Kwa nini mhangaike na Watu waliokwisha Kufa wasio na chochote cha kuchangia katika Ulimwengu wa Waliohai? Wema Waliohai pia wapo wengi.

Hatuwezi kuongoza nchi Kwa kuangalia Wafu, na hatutataka nchi yetu iongozwe na watu wenye mawazo na Matendo ya Wafu.

Tunahitaji viongozi ambao wanaongoza nchi Kwa kuangalia Maisha ya kizazi kijacho kitaishije,
Nchi inaongozwa Kwa mahitaji yajayo sio mahitaji yaliyopita. Nchi inaongozwa Kwa maslahi ya Watu wa kesho sio Kwa maslahi ya Watu wa Jana na juzi waliokwisha Kufa.

Wanaoishi Wasiwe watumwa wa Wafu, Watu waliokwisha Kufa. Hivyo ndivyo taifa hili linapaswa kujengwa na kuongozwa. Kwa sababu tunaenda Mbele na sio Nyuma.

Sijui Fulani alikuwa Nani akasema nini, hiyo haina maana yoyote Kwa wakati au kizazi kijacho, kitakachoangaliwa ni manufaa ya kizazi kijacho.

Hata Mungu tunayemuabudu ni MUNGU aliyehai na Mungu wa Waliohai sio Mungu wa Wafu.

Wanasiasa mnaomtaja taja Magufuli Kwa ubaya mnayohaja ya kujitafakari, kama mnaagenda zenu za Siri Sawa lakini eleweni kuwa haitasaidia Jambo LOLOTE lile.

Acha nipumzike SASA.

Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Makanya, Same, Kilimanjaro.
Mbona shetani aliasi maelfu ya miaka nyuma na bado anatajwa hadi leo.

Kwanini mnataka wahuni wengine wasitajwe ?
 
Wanasiasa mnaomtaja taja Magufuli Kwa ubaya mnayohaja ya kujitafakari, kama mnaagenda zenu za Siri Sawa lakini eleweni kuwa haitasaidia Jambo LOLOTE lile.
Mkuu Robert Heriel kiufupi kwa sasa utawala uliopo unapambana kumfanya magufuli aonekane kuwa alikuwa kiongozi mbovu sana na hata hawa akina Lissu kurudi wamekuja special kwenye hii mission ya kuhakikisha kila mtanzania anapata ujumbe wa namna magufoòl alivyokuwa kiongozi was hovyo kabisa

Ila kiuhalisia magufuli alikuwa rais kituko toka nchi ipate Uhuru ni basi tu kuna idadi kubwa sana ya ng'ombe mtaani plus maiti zinazojongea
 
Back
Top Bottom