Uchaguzi 2020 Kuenguliwa kwa wagombea: Pemba wahimizana kuandika usia kabisa maana sasa wako tayari kwa lolote

Uchaguzi 2020 Kuenguliwa kwa wagombea: Pemba wahimizana kuandika usia kabisa maana sasa wako tayari kwa lolote

Kufa tutakufa tu wote siku moja. Unaweza kuchagua kufa katika manyanyaso ama kufa ukipigania haki yako. Sijui wewe kwa mawazo yako unapoona wagombea wa vyama vingine wanaondolewa bila makosa, sijui inakupa burudani gani? Kama siyo ushetani ni nini? Yaani utaka waondolewe halafu wanyamaze tu. Nchi hii imejaa mashetani sana.
Mashujaa walipata kipigo cha mbwa koko.waliikimbia nchi.wajalibu tena tutawaletea jeshi kanda maalum kutoka tarime ndio size yenu.hayo maneno utajutia ukiwa kilema au umedead
 
Katika hali inayoashiria uwezekano wa umwagaji mkubwa wa damu huko Zanzibar hasa kisiwani pemba, wananchi wa huko wakiwa na hasira kali kutokana na kuenguliwa wagombea wao, wamejiapiza kukabiliana na chochote kilicho mbele yao hata ikibidi kupoteza maisha yao.

Wamehimizana kila mmoja kuandika usia kabisa kwa sababu chochote kinaweza kutokea.

Kwa kweli kama Taifa hatukupaswa kufika hapa, Wazanzibar wamevumilia mengi, wamevumilia ishu ya uchaguzi wa mwaka 2015, wakavumilia kuingiliwa na kuvurugwa chama chao kikuu cha CUF, sasa leo kweli wavumilie kweli kunyimwa chaguo la kumchagua mtu wamtakaye? —aaah wakubwa, oneni aibu

Lakini Kama wananchi wakimwaga damu zao kwa sababu ya michezomichezo hii ya kunyima haki wananchi, Tume ya Uchaguzi NEC na watawala, hawatakwepa lawama, damu za wananchi wasio na hatia zitakuwa mikononi mwao.

Hapa chini ni video ikionyesha wananchi wakijiapiza kwa lolote!

View attachment 1552518
Mungu ibariki Pemba
 
Kumbe mkuu ulikuwa unanitega mi nilijua na wewe ni miongoni mwa wale wasiotumia kichwa kufikiri.



MAGUFULI4LIFE.
Mimi niko bara nasubiri nimchinje tu Gwajima nakura yangu nimpe Lissu, lakini huko Zanzibar yakitokea yakutokea kila mtu ataulizwa alitimizaje wajibu wake.
 
Hili ndilo hutasikia toka CCM, NEC, Wakurugenzi wa halmashauri, viongozi wa dini, TBC... Utasikia tu amani, amani, amani.... Hakuna kuongelea haki! Yaani hata wagombea wako wote wakikatwa, kubali ili kuwe na amani!
Nafikiri wanaongelea UTULIVU na si AMANI kwani amani ni swala la ndani ya moyo wa mtu. Haiwezekani mtu akakatwa pasipo kufuata haki na then akabaki na amani yeye na wafuasi wake. Anaweza akatulia kwa kutishwa kwamba akiidai haki yake ataumizwa kwa kipigo cha mbwa koko. Ni vizuri tuzingatie haki ili kuifanya Tanzania sehemu salama.

Baba wa taifa Mwal. Nyerere aliwahi kusema kuwa tusijidanganye kuwa "sisi tuna amani si sawa na wale" na akasema amani hii imetengenezwa na hivyo inabidi tuitunze kama mti kwa kuumwagilia maji, kuutilia mbolea ili uendelee kustawi. Matendo yote mabaya ya kuminya haki za watu na kundi moja kujiona kwamba linaweza kufanya lolote kuchezea haki za watu wengine yatapelekea amani tuliyo nayo kutoweka.

Ukiitazama video hiyo kama ni mfanya maamuzi na unampenda Mungu na watanzania unaweza kutoa maelekezo kuwa wagombea wote wamepita hata kama kuna makosa madogo madogo kwenye forms zao kwani msingi mkubwa ni haki yao iliyopo kwenye katiba ya kuchagua viongozi na kuchaguliwa. Yule DED wa Serengeti ameonesha mfano kwa kuyakataa mapingamizi yote na kuwa wagombea wote wamepitishwa na hivyo wakafanye kampeni na wananchi waamue nani wa kuwawakilisha.

Haiwezekani mgombea kukatwa kwa mfano kwa sababu hajaweka picha na unamwona usimwambie kalete picha au kaandika DSM ambacho tunafahamu kwa mazoea ni kifupi cha Dar es Salaam na ufanye mwingine ambaye kapita kwenye mchakato wa chama awe mwakilishi wa wananchi pasipo kupigiwa kura, haingii kabisa akilini na swala kama hilo liwe chanzo cha kuharibu amani yetu.

Tusifanye form za uchaguzi kama ushindani wa kupata zabuni ambapo mzabuni hana njia ya kuirekebisha zabuni yake mara tu baada ya kuwasilisha na tuzingatie kuwapa fursa wananchi kuchagua wawakilishi wao baada ya kujinadi kwa kueleza ni nini watawafanyia mara watakapo wachagua ni kwa kufanya hivi tutakuwa tumetimiza takwa la kikatiba.
 
Usiamini hili. Ni propaganda za CCM na NEC. Wagombea siyo kwamba wamekosea. Fomu zimebadilishwa. Picha zinatolewa. Tume yenyewe imeandika mapingamizi kwa wagombea wa ACT kule Zanzibar kwa kutumia majina ya wagombea wengine ambao wamekanusha kwa maandihsi kuwa hayo mapingamizi siyo yao. Ni ghiriba za Tume na CCM. Wala siyo kuwa wamekosea kujaza fomu. Wapinzani wanajisumbua tu. Wapiganie mfumo ubadilike hata kama inamaanisha kumwaga damu.
Haiwezekani mgombea kukatwa kwa mfano kwa sababu hajaweka picha na unamwona usimwambie kalete picha au kaandika DSM ambacho tunafahamu kwa mazoea ni kifupi cha Dar es Salaam na ufanye mwingine ambaye kapita kwenye mchakato wa chama awe mwakilishi wa wananchi pasipo kupigiwa kura, haingii kabisa akilini na swala kama hilo liwe chanzo cha kuharibu amani yetu. Tusifanye form za uchaguzi kama ushindani wa kupata zabuni ambapo mzabuni hana njia ya kuirekebisha zabuni yake mara tu ya kuwasilisha na tuzingatie kiwapa fursa wananchi kuchagua wawakiloshi wao baada ya kujinadi kwa kueleza ni nini watawafanyia mara watakapo wachagua ni kwa kufanya hivi titakuwa tumetimiza takwa la kikatiba.
 
Sasa wewe unataka kutufundisha sisi wasukuma kipi.yaani MTU wa ujaruoni wa Kenya aje atuendeshe cc watu wa mwanza .kila siku maandamano.tukaona upumbafu mtupu.tukatupilia mbali.hapo hapo unawakubali wapemba na wewe si mpemba watakuchokonoa.angalia sana
Pemba haikuhusu ushike adabu yako.

Ujinga wenu fanyieni hukohuko.
 
Wapigwe tu, kosa lao ni kutafuta chama kidogo badala ya kujiunga na chama kikuu cha upinzani. ACT ina viongozi wabinafsi wanajiangalia wao badala ya umma. Wamekuja kuzigawa kura za wapenda mabadiliko.

Wapigwe tu hakuna namna
Wee komwe mjinga mmoja ikiwa hamwezi uchaguzi huru na haki kwanini mnapoteza pesa kila siku kwa uchaguzi?
 
Katika hali inayoashiria uwezekano wa umwagaji mkubwa wa damu huko Zanzibar hasa kisiwani pemba, wananchi wa huko wakiwa na hasira kali kutokana na kuenguliwa wagombea wao, wamejiapiza kukabiliana na chochote kilicho mbele yao hata ikibidi kupoteza maisha yao.

Wamehimizana kila mmoja kuandika usia kabisa kwa sababu chochote kinaweza kutokea.

Kwa kweli kama Taifa hatukupaswa kufika hapa, Wazanzibar wamevumilia mengi, wamevumilia ishu ya uchaguzi wa mwaka 2015, wakavumilia kuingiliwa na kuvurugwa chama chao kikuu cha CUF, sasa leo kweli wavumilie kweli kunyimwa chaguo la kumchagua mtu wamtakaye? —aaah wakubwa, oneni aibu

Lakini Kama wananchi wakimwaga damu zao kwa sababu ya michezomichezo hii ya kunyima haki wananchi, Tume ya Uchaguzi NEC na watawala, hawatakwepa lawama, damu za wananchi wasio na hatia zitakuwa mikononi mwao.

Hapa chini ni video ikionyesha wananchi wakijiapiza kwa lolote!

View attachment 1552518
Mkuu hawa wanaoongea ni wananchi au wana ACT Wazalendo?
 
Mimi naona CCM bara ikubali kuiacha mkono CCM Zanzibar. Watajitia matatizoni bureeee. Mwaka huu, Wapemba wamedhamiria liwalo na liwe. Tutakuja kulaumiana bureeeee kabisa. Wapewe haki yao tu. Dhulma wanayoifanya hii itakuja kuwaumbua, wale wa Kaskazini msumbiji wakipata habari hizi naona watajiandaa kuweka kambi Pemba. Halafu Serikali itaanza kumtafuta mchawi kumbe wachawi wenyewe wamejiroga.

Mwaka huu Zanzibar mbivu na mbichi itajulikana!
 
Kwani muungano watu wameungama na tarehe inajulikana mungano ni sawa sawa sawa na ndoa mdaa wowote mwaweza kuachana hamna mkataba wa milele bora nyinyi mubaki na Tanganyika yenu sisi tubaki na Zanzibar yetu
Muungano havunjwi yakhee
 
Kusini na Membe tu, korosho tunadai, kaua mfumo wa pembejeo, tulikuwa tunapata miche bure sasa hamna, wakala wa pembejeo wanadai hadi leo, nasubiri 28/10/2020.
 
Wazan
Hayati Mkapa alijuta mpaka siku anaondoka duniani kumwagika kwa damu ya wazanzibar mwaka 2001. Alijitahidi sana kadri ya ushawishi wake kuwaasa viongozi waliokuja baadae waiangalie Zanzibar kwa jicho la umakini maana uonevu kwa wale watu unaweza pelekea hata hao watu kuukataa muungano wenyewe, ikifikia hatua ya wao kuukataa muungano hata upeleke majeshi milioni utaishia kumwaga damu zaidi tu lakini kamwe hutopata ridhaa yao!.
Kama kuna watu wenye akili na wanatafakari waufanyie kazi ushauri ule wa Mkapa la sivyo nao wataburuzwa ICC kwa umwagaji wa damu za wananchi!
Wazanzibari hawana unafiki unafiki wakiamuwa kitu wanaamuwa tuu
 
Back
Top Bottom