Uchaguzi 2020 Kuenguliwa kwa wagombea: Pemba wahimizana kuandika usia kabisa maana sasa wako tayari kwa lolote

Kufa tutakufa tu wote siku moja. Unaweza kuchagua kufa katika manyanyaso ama kufa ukipigania haki yako. Sijui wewe kwa mawazo yako unapoona wagombea wa vyama vingine wanaondolewa bila makosa, sijui inakupa burudani gani? Kama siyo ushetani ni nini? Yaani utaka waondolewe halafu wanyamaze tu. Nchi hii imejaa mashetani sana.
Mashujaa walipata kipigo cha mbwa koko.waliikimbia nchi.wajalibu tena tutawaletea jeshi kanda maalum kutoka tarime ndio size yenu.hayo maneno utajutia ukiwa kilema au umedead
 
Mungu ibariki Pemba
 
Kumbe mkuu ulikuwa unanitega mi nilijua na wewe ni miongoni mwa wale wasiotumia kichwa kufikiri.



MAGUFULI4LIFE.
Mimi niko bara nasubiri nimchinje tu Gwajima nakura yangu nimpe Lissu, lakini huko Zanzibar yakitokea yakutokea kila mtu ataulizwa alitimizaje wajibu wake.
 
Hili ndilo hutasikia toka CCM, NEC, Wakurugenzi wa halmashauri, viongozi wa dini, TBC... Utasikia tu amani, amani, amani.... Hakuna kuongelea haki! Yaani hata wagombea wako wote wakikatwa, kubali ili kuwe na amani!
Nafikiri wanaongelea UTULIVU na si AMANI kwani amani ni swala la ndani ya moyo wa mtu. Haiwezekani mtu akakatwa pasipo kufuata haki na then akabaki na amani yeye na wafuasi wake. Anaweza akatulia kwa kutishwa kwamba akiidai haki yake ataumizwa kwa kipigo cha mbwa koko. Ni vizuri tuzingatie haki ili kuifanya Tanzania sehemu salama.

Baba wa taifa Mwal. Nyerere aliwahi kusema kuwa tusijidanganye kuwa "sisi tuna amani si sawa na wale" na akasema amani hii imetengenezwa na hivyo inabidi tuitunze kama mti kwa kuumwagilia maji, kuutilia mbolea ili uendelee kustawi. Matendo yote mabaya ya kuminya haki za watu na kundi moja kujiona kwamba linaweza kufanya lolote kuchezea haki za watu wengine yatapelekea amani tuliyo nayo kutoweka.

Ukiitazama video hiyo kama ni mfanya maamuzi na unampenda Mungu na watanzania unaweza kutoa maelekezo kuwa wagombea wote wamepita hata kama kuna makosa madogo madogo kwenye forms zao kwani msingi mkubwa ni haki yao iliyopo kwenye katiba ya kuchagua viongozi na kuchaguliwa. Yule DED wa Serengeti ameonesha mfano kwa kuyakataa mapingamizi yote na kuwa wagombea wote wamepitishwa na hivyo wakafanye kampeni na wananchi waamue nani wa kuwawakilisha.

Haiwezekani mgombea kukatwa kwa mfano kwa sababu hajaweka picha na unamwona usimwambie kalete picha au kaandika DSM ambacho tunafahamu kwa mazoea ni kifupi cha Dar es Salaam na ufanye mwingine ambaye kapita kwenye mchakato wa chama awe mwakilishi wa wananchi pasipo kupigiwa kura, haingii kabisa akilini na swala kama hilo liwe chanzo cha kuharibu amani yetu.

Tusifanye form za uchaguzi kama ushindani wa kupata zabuni ambapo mzabuni hana njia ya kuirekebisha zabuni yake mara tu baada ya kuwasilisha na tuzingatie kuwapa fursa wananchi kuchagua wawakilishi wao baada ya kujinadi kwa kueleza ni nini watawafanyia mara watakapo wachagua ni kwa kufanya hivi tutakuwa tumetimiza takwa la kikatiba.
 
Usiamini hili. Ni propaganda za CCM na NEC. Wagombea siyo kwamba wamekosea. Fomu zimebadilishwa. Picha zinatolewa. Tume yenyewe imeandika mapingamizi kwa wagombea wa ACT kule Zanzibar kwa kutumia majina ya wagombea wengine ambao wamekanusha kwa maandihsi kuwa hayo mapingamizi siyo yao. Ni ghiriba za Tume na CCM. Wala siyo kuwa wamekosea kujaza fomu. Wapinzani wanajisumbua tu. Wapiganie mfumo ubadilike hata kama inamaanisha kumwaga damu.
 
Pemba haikuhusu ushike adabu yako.

Ujinga wenu fanyieni hukohuko.
 
Wapigwe tu, kosa lao ni kutafuta chama kidogo badala ya kujiunga na chama kikuu cha upinzani. ACT ina viongozi wabinafsi wanajiangalia wao badala ya umma. Wamekuja kuzigawa kura za wapenda mabadiliko.

Wapigwe tu hakuna namna
Wee komwe mjinga mmoja ikiwa hamwezi uchaguzi huru na haki kwanini mnapoteza pesa kila siku kwa uchaguzi?
 
Mkuu hawa wanaoongea ni wananchi au wana ACT Wazalendo?
 
Mimi naona CCM bara ikubali kuiacha mkono CCM Zanzibar. Watajitia matatizoni bureeee. Mwaka huu, Wapemba wamedhamiria liwalo na liwe. Tutakuja kulaumiana bureeeee kabisa. Wapewe haki yao tu. Dhulma wanayoifanya hii itakuja kuwaumbua, wale wa Kaskazini msumbiji wakipata habari hizi naona watajiandaa kuweka kambi Pemba. Halafu Serikali itaanza kumtafuta mchawi kumbe wachawi wenyewe wamejiroga.

Mwaka huu Zanzibar mbivu na mbichi itajulikana!
 
Kwani muungano watu wameungama na tarehe inajulikana mungano ni sawa sawa sawa na ndoa mdaa wowote mwaweza kuachana hamna mkataba wa milele bora nyinyi mubaki na Tanganyika yenu sisi tubaki na Zanzibar yetu
Muungano havunjwi yakhee
 
Kusini na Membe tu, korosho tunadai, kaua mfumo wa pembejeo, tulikuwa tunapata miche bure sasa hamna, wakala wa pembejeo wanadai hadi leo, nasubiri 28/10/2020.
 
Wazan Wazanzibari hawana unafiki unafiki wakiamuwa kitu wanaamuwa tuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…