Kuepuka usumbufu, nakushauri usitume pesa kutoka Tigo/Yas kwenda mitandao mingine kuanzia saa 12 jioni. Be informed

Kuepuka usumbufu, nakushauri usitume pesa kutoka Tigo/Yas kwenda mitandao mingine kuanzia saa 12 jioni. Be informed

Maleven

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2019
Posts
783
Reaction score
3,666
Yani tangu Tigo iwe yasi kuna mambo mengi ya kukera lakini kubwa zaidi ni changamoto ya kutuma pesa kutoka Tigo kwenda mitandao mingine has ikifika usiku.

Imagine unatuma pesa, kisha wanakwambia usubiri masaa 72 ndio utapata majibu kama pesa itarudi au itafika kwa mhusika.

So kujiepusha na usumbufu, bora usifanye miamala ya mitandao tofauti, bora iende kwa wakala au mhusika akupe namba ya Yas.
 
Ebwana, mi nimetoka kuongea nao hapa, nimepewa majibu hayo hayo, masaa 72
 
Yani tangu Tigo iwe yasi kuna mambo mengi ya kukera lakini kubwa zaidi ni changamoto ya kutuma pesa kutoka Tigo kwenda mitandao mingine has ikifika usiku.

Imagine unatuma pesa, kisha wanakwambia usubiri masaa 72 ndio utapata majibu kama pesa itarudi au itafika kwa mhusika.

So kujiepusha na usumbufu, bora usifanye miamala ya mitandao tofauti, bora iende kwa wakala au mhusika akupe namba ya Yas.
Ni kweli usemacho...hata huduma yao ya LIPA NAMBA. ..mfano nimeends juzi sehemu ya starehe wananiambia kama utalipa kwa LIPA NUMBER ya tigo,lipa kabisa kabla ya kuhudumiwa maana inasumbua sana...kiukweli ni kero kero kero......mtandao ushajifia huo
 
Na deal na hilo suala muda huu, nimeambiwa nisubiri masaa 72, nilituma jana jioni kwenda Voda, wameniudh sana
 
Uko sahihi kabisa, kuanzia usiku usifanye masuala ya muamala ktk Yas, kuna usumbufu mnoo. Lol
 
Na deal na hilo suala muda huu, nimeambiwa nisubiri masaa 72, nilituma jana jioni kwenda Voda, wameniudh sana
Kwanini hawaadmit? Kua na tatizo wanaleta ujanja?
 
Yas si wa kuwaamini kwa sasa,hata message hazifiki kwa wakati
 
Nilifikiri ni mimi mwenyewe tu kumbe tupo wengi. Ukituma pesa inakuja meseji kuwa muamala wako umerudishwa. Sasa hiyo kurudishwa kwake nilifuatilia siku tatu napiga simu kwa wahudumu ndio ikarudi kwa mbinde sana. Kila mhudumu unayempigia anakwambia tayari nimesharekebisha utaona muamala wako ukicheki salio bila bila.

Hivi huko YAS shida ni nini kwani si walibadilisha jina tu au walibadilisha na mitambo yao? Mbona wakati wa TIGO ilikuwa poa sana ukiona meseji kuwa muamala umerudishwa basi dakika chache tu unaona pesa zako zimerudi.
 
Back
Top Bottom