Uchaguzi 2020 Kufa kwa Sekta Binafsi na Makampuni ya Ujenzi ya ndani ndio kunanifanya nimpe kura Lissu

Uchaguzi 2020 Kufa kwa Sekta Binafsi na Makampuni ya Ujenzi ya ndani ndio kunanifanya nimpe kura Lissu

Kabisa.... Jamaa alipoingia alikuwa na mentality kwamba private sector ni maadui wakubwa wa maendeleo ya nchi. But alisahau kuwa ni private sector ndio inaajiri zaidi..... Leo hii mpaka kazi za wanawake wa vikundi kazi zake zimechukuliwa na SUMA JKT..... Uppuzi mkubwa kweli
Huu mtihani mkubwa sana.
 
Amini nawaambia hata maccm wenyewe wanajuta kumsukumiza mshamba na Limbukeni wa kihutu wanaombea ashindwe ila hawawezi kuonyesha hadharani .
IMG_20200928_120550.jpg
 
Utawala huu hakuna janja janja,mpe tu lissu kura yako atakufufulia Richmond,hakuna tatizo
Kama mwenyekiti wenu anakwapua 1.5tilion kwa mkupuo mmoja na anazuia mbwa kubweka, kweli huoni aibu kusema janjajanja imeisha
 
Kuanguka kwa sekta binafsi kumesababisha watu kukosa ajira na hivyo ukosefu wa kipato ambacho kingesaidia mzunguko wa pesa. Watu waliokuwa wananunua mahitaji kama vyakula, nguo na hata kupata hata bia moja mbili tatu hawapo tena. Kwa wafanyabiashara ambao walikuwa wakiwauzia wenye ajira nao pia wanalia hivyo nao pia inakuwa shida kwao kununua vyakula, nguo nk na hivyo mzunguko wa athari unakuwa mrefu.

Pesa hiyo pia ilikuwa inatumwa kwa wazazi vijijini ambao walikuwa wanakwenda sokoni na kwingineko kununua mahitaji yao lakini watoto wao walipokosa ajira, hakuna pesa inayozunguka kwenda mpaka vijijini. Uendeshaji wa uchumi unahitaji busara na weredi katika uchumi. Ni vizuri kupata ushauri wa wachumi katika uendeshaji wake badala ya wewe kuwashauri wao au kuelekeza nini kifanyike.
 
Wa tz wengi maisha yetu tulizoea kuishi kwa ujanja ujanja kaja Magufuli mianya yote kaziba tunaanza kulalamika ila hakuna rais bora kama magufuli kura yangu na yafamilia yangu atapata hakuna shaka ndani yake

Mkuu, bila kuathiri uelekeo wako wa kupiga kura, hivi huo ujanja ujanja mnaoukariri humu jukwaani kila wakati ni upi?

Hivi mnapenda watanzania waishi kama mazoba au?

Yaani watu wakitumia akili zao kufanikisha maisha yao nyie mnasema “wanaishi kwa ujanja ujanja”. Toka lini binadamu akaishi bila kutumia akili?.

Nchi ina utawala wa sheria. Kwa nini wanaoihalifu sheria ya nchi wasiwajibishwe na sheria hiyo hiyo wanayoivunja na badala yake mnajumuisha watanzania wote kuwa ni wahalifu, eti wamezoea kuishi kiujanja ujanja?

Na kama sheria zilikuwa zinavunjwa kosa ni la wananchi au serikali iliyokuwa madarakani?


Mkuu utaniwia radhi lakini maoni ya jumla jumla kama hayo yanasadifu ukosefu wa fikra na wivu unaotokana na inferiority complex.

Siasa sio uadui.
 
Mpaka 2015 private sectors zilikuwa zinashamiri. Jakaya aliacha mazingira mazuri na bora kabisa kwa sekta binafsi kukua na kuboreka. Ila tokea 2016 makampuni ambayo idadi yake haijulikani yamefungwa katika nchi hii, na bado yanaendelea kufungwa. Vijana lukuki wamepoteza ajira katika makampuni hayo.... na wale ambao walijiajiri kwa kufungua makampuni kwa sasa wanalia kilio cha kusaga meno, baada ya kuwindup makampuni yao....

Nilikuwa naongea na Mwanasheria moja jana anasema kazi nyingi anazopata kwa sasa ni kuwindup makampuni. Kwa mwezi anawindup makampuni 46-50 na kwa upande mwingine anafungua 2-3 tu. Sasa cheki hiyo ratio mwenyewe uone.. The private sector is tottaly dead!. Na ndio sector ambayo ingechukua vijana wengi hasa wahitimu wa vyuo. UD inamwaga kila mwaka, UDOM inamwaga kila mwaka, Mzumbe, Tumaini, Muhimbili, TIA na wengine wengi. zaidi ya vyuo 40.... Sasa vijana hao wote hawawezi kuajiriwa sijui na SUMA JKT, TBA,NHC ambao kwa sasa ndio wanafanya kazi zote mpaka za kufagia barabara wakati hizo zilikuwa ni kazi za vikundi vya wanawake na vijana katika mitaa chini ya usimamizi wa Halmashauri.

Jakaya kipindi anatoka aliacha makampuni ya ujenzi ya ndani yalioweza kushindana na Wachina kibao. But look now they are all dead. Kivipi, TRA Kuwabambikizia kesi za madeni, kazi kubwa zote wamechukua makampuni ya nje, kazi za ndani zote za serikali anafanya SUMA JKT, TBA, NHC, mpaka na Magereza. Is simpe local contractors can not survive in that circumstance. Ok!.. Mpaka yale maujenzi ya Halmashauri wameleta mfumo wa Force Account ambao ni ulaji wa watu wa manunuzi bila kujua wanauwa private sekta... Tuliona enzi za Jakaya akipambana kuweka mazingira bora, ndio maana tukaona wazawa wakiflourish kama vile SKOL (now is dead), DELEMONTE (now is dead), MILEMBE (now is dead), MECCO (now id dead), CASPIAN (is almost dead kabaki na kazi za Barrik tu)... the list is endless..

Sasa kwa hali kama hiyo how can You dare to vote for this man again!. No, way unless atuambie kuwa atabadilika na kubadili mfumo wake wa kuuwa makampuni ya ndani. Wahenge wanasema kuuwa uchumi ni suala la siku 2 au tatu ila kuujemga ni miaka 10 t0 20... Hii miaka 5 uchumi umekufa kabisa, mpaka kuja kusimamisha uchumi is not now and haitatokkea kama hatobadilika au kama wananchi tusipoamua kumpa kura Lisu

Kuna uwongo mwingi kuliko ukweli.
Tunachotakiwa tuzungumzie ni kwa nini haziingii mifukoni kwa wengi.

Serikali ya Magufuli na uchumi huu huu wa Tanzanaia umetengeneza Dollar Millionaires wengi kuliko nchi yeyote kwa kanda ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika kuondoa Afrika ya Kusini pekee yake.
 
Huo uwongo wenu wa chadema mwisho wenu ni October

Mlizoea ufisad,hamlipi kodi imekula kwenu

Ungejiita tu msopage, dadii au chimpumu yetu.

Mnajidai wazalendo lakini hamkosi kujishaua na majina ya “kibeberu”.
 
Wanatugeuza Kama chapati:
. BINAFSISHA
. GAWA NYUMBA ZA UMMA KWA WAPENDWA
. RUDIA UJIMA
. SERIKARI NUNUA KOROSHO
.
.
AS YOU WERE! 😎
KIZUNGUZUNGU!
🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔💥🔥
 
Wababaishaji tu ndo wanafunga na pengine ndo walikuwa wengi.

SONGORO MARINES mbona hajafunga?

Kuna makampuni ya wakenya yanashinda tenda Tz toka enzi za JK,kama mko competent kweli si mvuke border mkashindane huko ambako sector binafsi ipo hai tuone badala ya kulilia upendeleo wa uzawa.

CASPIAN ilijifia kitambo tu baada ya mgodi wa Lusu/Resolute-Nzega kufungasha.

BTW:Kura yako ingekuwa labda ya Turufu ndo ingekuwa habari tofauti na hapo wewe utampigia unayejisikia tu kumpa na si lazima uwe na sababu.
 
NCHI YETU YA TANZANIA YUMEKUWA NA BUBLE ECONOMY MUDA WA MIAKA 6, TANGU 2008 MPAKA 2015.

Marekebisho yake yangechukuwa muda mrefu, lakini marekebisho nafikiri yamefanya tayari. Mnacho lalamikia wangu wengi tulikua tunaishi katika uchumi ambao matatizo mengi tulitumia kwa kuongeza pesa katika mfumo mzima wa uchumi.

Uchumi tulio nao sasa hivi ndio uchumi halisi wa kibepari ambao kuna chama fulani kina uhubiri.
Bwana Pagan ningeweza kukupa riport ambayo niliitayarishe ambayo ingekupa picha ya ninavyo uona uchumi wetu na Mkuu kabisa nilimtumia.

Naomba ufuatiliye kwenye Inbox yako.
 
Back
Top Bottom