Kufanikisha kutengeneza gari, Kipanya ni shujaa

Kufanikisha kutengeneza gari, Kipanya ni shujaa

ego

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2013
Posts
1,620
Reaction score
1,407
Kitendo alichokifanya Masoud Kipanya ni cha kishujaa na kinastahili kupewa pongezi.

Tunahitaji vijana wengi kuiga alichokifanya kipanya katika bidhaa mbalimbali zinazozalishwa huko ulimwenguni, wabuni kwa brand zao na kutengeneza.

Labda nimshauri Kipanya kuwa gari lake asiliweke makumbusho kulifanyia maonyesho kama anavyotangaza bali aliweke barabara kulifanyia majaribio.

Daima product ya kwanza huwa ina changamoto nyingi sana na kadiri atakavyoliingiza barabarani hili la mwanzo na kulijaribu ataweza kugundua changamoto na kuzitafutia ufumbuzi kabla ya kuanza kufanya commercial production

Hongera sana Kipanya mimi naamini ulichokifanya kitaleta mapinduzi katika fani ya uhandisi nao wataanza kuwa kama wana bongofleva kila mtu anaibuka na product yake

masouudpic.jpg
 
Kwa kutengenezwa gari kazi, me hapa nikiwa na mtaji , naweza ibuka na product ya gari la umeme, treni ya umeme, baiskeli, pikipiki na kila kitu.
 
Uzi bila picha mkuu? Tuwekee picha sisi ambao tupo wilaya ya Tanganyika tuweze kuliona
20220404_091131.jpg

Pamoja na kuonekana shujaa bado kuna jambo la kushangaza ambalo mimi nawashangaa watanzania wenzangu.

Nadhani masoud si Mtanzania wa kwanza kuunda gari tena likiwa la umeme tofauti na yale ya mafuta ambayo mengi yamepotezewa na mamlaka sababu wanasema hayana ubora.

Kinachomfanya masoud aonekane ni vile ametumia matangazo, kufahamika, mamlaka husika kama ya uwekezaji nk, ambao watampa support.

But mkumbuke kuna vijana wamekuwa na ujuzi mkubwa sana tatizo ni mamlaka zetu za kiafrika ndizo hazioni vipaji na hata kama zikiona basi ukiwa tayari mikononi mwa wadau wakubwa.
 
Wenzetu Malasyia tena chini ya mwembe au garage bubu wanaunda mabus classic. Finishing mfano dashboard, viti, keria ya ndani, taa, vioo nk ndo ununua dukani. Tena wanatumia nyundo, tindo, grenda, welding machine tu. Ndo mabus wanayauza huku milioni 500.
 
Ila hajalenga Soko la Tanzania, maana kama nilimsikia vizuri anasema kwamba ametumia 45 milioni mpaka kulikamilisha, Sasa kwa Tanzania yetu hii tutegemee bado watu watafanya Option ya Kuagiza Used Japan kuliko New ya Hela hiyo.

Brand New car itakuwa mziki kwa majority ya WTZ
 
Kitendo alichokifanya Masoud Kipanya ni cha kishujaa na kinastahili kupewa pongezi.

Tunahitaji vijana wengi kuiga alichokifanya kipanya katika bidhaa mbalimbali zinazozalishwa huko ulimwenguni, wabuni kwa brand zao na kutengeneza.

labda nimshauri kipanya kuwa gari lake asiliweke makumbusho kulifanyia maonyesho kama anavyotangaza bali aliweke barabara kulifanyia majaribio.

Daima product ya kwanza huwa ina changamoto nyingi sana na kadiri atakavyoliingiza barabarani hili la mwanzo na kulijaribu ataweza kugundua changamoto na kuzitafutia ufumbuzi kabla ya kuanza kufanya commercial production

Hongera sana Kipanya mimi naamini ulichokifanya kitaleta mapinduzi katika fani ya uhandisi nao wataanza kuwa kama wana bongofleva kila mtu anaibuka na product yake

View attachment 2175048

Hadi sasa ninashangaa kwanini chuo kikuu cha Dar es salaam hakijamtunuku kipanya PhD.​

Back
Top Bottom