Kufanya biashara ya ubia partnership na mbongo bora pesa yako ujenge nyumba ya wapangaji

Umesema ukweli kabisa. Ila mimi nadhani ni watanzania wote tuko hivi. Hata waliokaa ugahaibuni, kuan wenye tabia kama hizi. Kwa kifupi ni hivi: kuliko kuingia ubia na mtanzania ni bora fedha ufanyie starehe angalau uje kukumbuka ulikula good time.
Kwanini usijenge nyumba na upangishe kuliko kushinda kumbi za starehe.
 
Watanzania wameshajenga culture ya kuiba sehemu ya kazi. Infact kuiba kazini inaonekana kama ndiyo ujanja na usipoiba unakuwa mjinga kwa jamii.
 
Wengine huwa wanasoma sana ili waibe na post wanazotafuta ni za kupiga na akipanda cheo ndio matokeo ya EPA, ESCROW na bandari
Bora kuwa masikini kuliko mwenye elimu mwizi
 
Kinao saidiwa waislamu kua na waaminifu kiasi ila sio wote ni kuogopa dhuruma wanaihimizwa sana misikitini kwamba ukila dhuruma unakula moto tupu......siku ya kiama utaletwa mbele ya ule ulio mdhurumu
View attachment 2685668
 
Kwanini usijenge nyumba na upangishe kuliko kushinda kumbi za starehe.
Hiyo nimetumia sarcasm mkuu. Kuwa; bora uzitumie kwa starehe kuliko kuingia ubia i.e. kuonyesha ubaya ya kuamini biashara ya ubia na mtanzania. Hilo unalolalamikia limeshawapata wengi. Ni utamaduni ambao umeshajijenga kwa siku nyingi. Mbaya zaidi hata wanawake siku hizi wanatapeli waume zao.
 
Watanzania wameshajenga culture ya kuiba sehemu ya kazi. Infact kuiba kazini inaonekana kama ndiyo ujanja na usipoiba unakuwa mjinga kwa jamii.
Kuna kabila moja huwa wanaamini usipoiba ni mpumbavu
Hiyo ilikuwa zamani sana, ila sasa ni nchi nzima

Akikamatwa mwizi wa billions hakuna kufungwa kwa sababu hata aliemkamata na aliepiga kelele upigaji wote majizi

Ndio maana huoni mtu anafungwa kwa wizi
Na kesi ya mkurugenzi wa TPA na wenzake naona wataachiwa karibuni ingawa kuna hela ndefu zimepigwa

Hapo unaona kabisa kuna tatizo la wizi nchi nzima
 
Kinao saidiwa waislamu kua na waaminifu kiasi ila sio wote ni kuogopa dhuruma wanaihimizwa sana misikitini kwamba ukila dhuruma unakula moto tupu......siku ya kiama utaletwa mbele ya ule ulio mdhurumu
Hata wahindi wana asili ya uaminifu. Mhindi hata akikupiga atahakikisha ameleta faida halafu anakata hapo kidogo. Mtanzania anakula mpaka mtaji.
 
Naam, nakubaliana na wewe. Kwenye uaminifu wa tz wengi ni chini ya sifuri.
 
Swala la ubia, swala la kuajiri ndugu na watu wasio ndugu....ni kilio kikubwa Tanzania, ni nini suluhisho la kudumu la hili?
 
Aya ya mwisho mkuu, naomba ongezea maelezo tafadhali!!
 
[emoji1787]
 
Ina maana una-generalize kuwa Watanzania wote ambao hawana exposure nje ni wezi na waongo?

Kwanini unafanya hivyo? Ina maana Mufti pia una-generalize kuwa ni muongo kisa umefanyiwa na Watanzania wachache ambao sio waaminifu?

Tatizo ulitumia hisia na Imani kwenye mambo yanayohitaji akili. Wapo Watanzania waaminifu na wachapakazi sana. Ni sawasawa na mtu aseme watu wa jamiiforums wanawaza ngono, hawako serious, je ni kweli Iko hivyo?

Usiwakoseshe watu fursa, sema kuwa watu wawe makini na selections zao basi.
 
Swala la ubia, swala la kuajiri ndugu na watu wasio ndugu....ni kilio kikubwa Tanzania, ni nini suluhisho la kudumu la hili?
Tatizo linaanza tangu udogoni yaani mtoto anaona mwalimu anaiba chakula cha wanafunzi (ushuhuda upo)
Na yeye anaiba kalamu ya mwanafunzi baada ya kupoteza ya kwake
Mtoto hafuatiliwi na mzazi na haangalii bag lake
Mtoto haulizi kalamu kumbe mwizi

Wafundisheni watoto kuwa na maadili na pia msiwafanye wasiijue hela wapeni hata 200 mara moja moja hata 500 sawa azoee hela

Sasa kama msukuma anasema alikuwa anaiba dhahabu kupitisha mpakani unategemea mtoto akimuona kiongozi anaongea hivyo au mwanae ataacha kuwa mwizi?

Sisi tulikuwa tunapewa hela kuzihesabu tulipokuwa wadogo na tulikuwa tunaona jambo la kawaida na tumekuwa tunaziona
 
Kuwajenga watoto tangu wakiwa wadogo... nimekuelewa mkuu.

Nimeona maelezo ya mzee Wa NJEE YA BOX (Mh. Kigwangala) mitandaoni, nimeona maelezo yake jinsi alivyoibiwa, na watu aliowaamini. Pia ulisoma michango (comments) za watu wengine nao wanalalamika kuibiwa na ndugu nk. Suluhisho kwa watu ambao hawajajengwa tangu wangali wadogo ni lipi mkuu, kwa uzoefu wako?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…