Ni bahati nzuri kwenye andishi lako, likisomwa kwa tafakuri, unakiri kuwa kilichofanywa na akina Halima Mdee 'ni kukikosea chama', mengine yanayobaki unataka kutumia huu muda mfupi kushawishi Chadema uingane na uovu wa akina Halima Mdee. Inajulikana kuwa Dk. Mashinji ametumiwa kwanza kumshawishi Esther Bulaya, ili atumike kumshawishi Halima Mdee kufanya hii aibua ambayo imemaliza kabisa kisiasa Halima Mdee na watu wa kariba ya Esther Matiko na Cecil Pareso. Akina Kishoa, angalau hakuna mtu aliyekuwa akiwapa asilimia 90+ katika kuhimili mapambano haya.
Kosa kubwa ambalo litafanywa na Chadema leo ni kuhalalisha huu uhuni. Ni uhuni kwa sababu, kama wataridhia kama unavyoshauri bwana NJAA, maana yake ni kwamba CCM na serikali itakuwa imewachagulia Chadema mpaka wabunge wa Viti maalum. Hawa akina Mdee, Bulaya na wengine hawakuwa katika mpango wa Chadema wa viti maalum. waliokuwa wameandaliwa ni wengine kabisa.
Kumbe hii itakuwa dharau iliyopitiliza: yaani wawapore kura, na wabunge wa viti maalum wawachagulie wenyewe, yaani watu ambao wametongozwa na Dk. Mashinji! UPUUZI
Chadema wawaafukuze mara moja hawa wanawake waliosaliti mapambano. Ni kweli njaa inauma, na wewe bwana NJAA umetuonyesha jinsi njaa ilivyokushughulikia kama inavyowashughulikia wengine awamu hii ya AJABU katika Taifa hili, mpaka ukanyosha mikono, lakini hiki kilichofanywa na akina Mdee hakistahili kuungwa mkono hata kidogo!
Inajulikana huu ni mpango wa kukiua Chadema, Chadema isikubali kufa kupitia hawa wanawake, wanaume wapambane hadi tone la mwisho, nyuma ya Chadema kuna kundi kubwa la wananchi ambao hata kama hawatokei kwenye maandamano wanayoyaitisha, au hata kama hawazungumzi chochote wanapoona wanafanyiwa matendo mabaya ikiwemo viongozi wao kuharibiwa biashara zao, lakini hawakubaliani kabisa na jinsi mambo yanavyoenda. wanaandamana mioyoni! Mtu anayeandamana moyoni.....