Kufanya kosa si kosa, kosa kurudia kosa. CHADEMA inakaribia kufa, hii ndio njia yenu pekee ya kujinasua

Kufanya kosa si kosa, kosa kurudia kosa. CHADEMA inakaribia kufa, hii ndio njia yenu pekee ya kujinasua

Mimi nawapongeza hawa wakina Mama kwakweli ni mashujaa, Chadema kwasasa nawapatia huu mstari wa Biblia Mathayo 10:16.

Wakubali hali ya uwanja ilivyo waende nayo hivyo hivyo huku wakijipanga vilivyo kwa 2025.

Wasisahahu UMOJA NI NGUVU.
 
Mkuu leo ndio rasmi cdm imegeuka kuwa NCCR, tutabaki wapinzani wa kweli bila kutegemea chama chochote cha siasa.
Pole sana Tindo hapa ni formula nyepesi tu IF YOU CAN'T FIGHT THEM,JOIN THEM.

Muhimu ninmshikamano kama Taifa tuvuke pamoja.
 
CHADEMA mkikubali ushauri wa ofisa huyu wa TIC nawahakikishia kifo cha mapema kuliko anachotabiri huyu afisa (Kuwa afisa wa TIC aliwahi kughafilika na kukiri humu).

Chadema fukuza hao wate, suka upya BAWACHA na maisha yaendelee. Mjipange kivingine
 
Hii nayo ni tekiniki ya namna ya kupata mpunga kutoka nje wasioofanya hivyo itakuwa ni ngumu kupata msaada maana watakuwa hawana wawakilishi mjengoni.
 
Hakuna sababu ya kutupa jiwe gizani, Tusubiri taarifa ya vikao halali vya kamati za chama vitoe ufafanunuzi.
 
Kufanya kosa sii kosa, kosa kurudia kosa!. Kususa kupeleka majina ni kosa, mimi niliuita ni ujinga!. Kina Halima Mdee wameukataa ujinga huu, kuwatimua ni kurudia kosa!.
Chadema msifanye death mistakes!.
We Mzee vipi? nani asiyejua dola imepenyeza rupia kwenye njaa?? ndani ya hilo kundi kuna kirusi kilichosambaza upendo... na ni kweli kimefanikiwa kukamlisha deal - Wazungu wanasema "Deal Done" !!

Narudia tena, kilichofanyika ni kwenye njaa watu wamepenyeza rupia na ngoma imetiki- na hii imekuwa tatizo kubwa kwa wanasiasa wa Tanzania hasa vijana kutokuwa na misimamo ya pamoja, kujali tumbo yao kwanza kuliko maslahi ya Taasisi wanayoisimamia kama viongozi.

Kwanza wengi wa hao wamenyanyaswa kijinsia wakati wa kampeni, sasa kukubali kula matapishi ni kuhalalisha hayo yote waliyotendewa kuwa yalikuwa ni halali .. ni sawa kwao lakini si sawa kwa taasisi.

Maamuzi ya Taasisi lazima yaheshimike, hutaki kuyaheshimu kanuni ipo wazi kabisa.
 
Mnyika achana naye, inategemea anaongea wakati gani na yuko katika hali gani kipindi anaongea, akina H.Mdee hawawezi kufikia uamuzi kama huo bila yeye kama KM kujua, hivyo Mnyika ni wa kuhurumia tu, ...
Ni kwa vile uelewa wako ni wa kiwango cha chekechea! Subiri tamko la Chadema
 
We Mzee vipi? nani asiyejua dola imepenyeza rupia kwenye njaa?? ndani ya hilo kundi kuna kirusi kilichosambaza upendo... na ni kweli kimefanikiwa kukamlisha deal - Wazungu wanasema "Deal Done" !!

Narudia tena, kilichofanyika ni kwenye njaa watu wamepenyeza rupia na ngoma imetiki- na hii imekuwa tatizo kubwa kwa wanasiasa wa Tanzania hasa vijana kutokuwa na misimamo ya pamoja, kujali tumbo yao kwanza kuliko maslahi ya Taasisi wanayoisimamia kama viongozi.

Kwanza wengi wa hao wamenyanyaswa kijinsia wakati wa kampeni, sasa kukubali kula matapishi ni kuhalalisha hayo yote waliyotendewa kuwa yalikuwa ni halali .. ni sawa kwao lakini si sawa kwa taasisi.

Maamuzi ya Taasisi lazima yaheshimike, hutaki kuyaheshimu kanuni ipo wazi kabisa.
Kama Ni hivyo basi CHADEMA wananukia rushwa
 
Uko sahihi Ushindi wa Kisiasa huchangiwa na Vyama vyote hata wale wasio navyo, tushikamane tulete Mawazo Mbadala na tujenge Taifa moja
 
Ni bahati nzuri kwenye andishi lako, likisomwa kwa tafakuri, unakiri kuwa kilichofanywa na akina Halima Mdee 'ni kukikosea chama', mengine yanayobaki unataka kutumia huu muda mfupi kushawishi Chadema uingane na uovu wa akina Halima Mdee. Inajulikana kuwa Dk. Mashinji ametumiwa kwanza kumshawishi Esther Bulaya, ili atumike kumshawishi Halima Mdee kufanya hii aibua ambayo imemaliza kabisa kisiasa Halima Mdee na watu wa kariba ya Esther Matiko na Cecil Pareso. Akina Kishoa, angalau hakuna mtu aliyekuwa akiwapa asilimia 90+ katika kuhimili mapambano haya.

Kosa kubwa ambalo litafanywa na Chadema leo ni kuhalalisha huu uhuni. Ni uhuni kwa sababu, kama wataridhia kama unavyoshauri bwana NJAA, maana yake ni kwamba CCM na serikali itakuwa imewachagulia Chadema mpaka wabunge wa Viti maalum. Hawa akina Mdee, Bulaya na wengine hawakuwa katika mpango wa Chadema wa viti maalum. waliokuwa wameandaliwa ni wengine kabisa.

Kumbe hii itakuwa dharau iliyopitiliza: yaani wawapore kura, na wabunge wa viti maalum wawachagulie wenyewe, yaani watu ambao wametongozwa na Dk. Mashinji! UPUUZI

Chadema wawaafukuze mara moja hawa wanawake waliosaliti mapambano. Ni kweli njaa inauma, na wewe bwana NJAA umetuonyesha jinsi njaa ilivyokushughulikia kama inavyowashughulikia wengine awamu hii ya AJABU katika Taifa hili, mpaka ukanyosha mikono, lakini hiki kilichofanywa na akina Mdee hakistahili kuungwa mkono hata kidogo!

Inajulikana huu ni mpango wa kukiua Chadema, Chadema isikubali kufa kupitia hawa wanawake, wanaume wapambane hadi tone la mwisho, nyuma ya Chadema kuna kundi kubwa la wananchi ambao hata kama hawatokei kwenye maandamano wanayoyaitisha, au hata kama hawazungumzi chochote wanapoona wanafanyiwa matendo mabaya ikiwemo viongozi wao kuharibiwa biashara zao, lakini hawakubaliani kabisa na jinsi mambo yanavyoenda. wanaandamana mioyoni! Mtu anayeandamana moyoni.....
 
Chadema iko imara kuliko kipindi chochote kile.
Juzi bahada ya kuwashirikisha ndugu na rafiki uhamuzi wangu wa kujiunga na CHADEMA ndani ya siku kumi na nne,Jana rafiki za takribani 53 wanajiunga na chadema ,na pendekezo nikufanya sherehe si chini ya watu 183 ya kwa kujiunga na CHADEMA
 
Naunga mkono kuwafukuza ni utoporo kwani Mbowe chama ashakitia nuksi tangu akatae na kususa chaguzi za kata na vijiji alafu akajipeleka uchaguzi Mkuu Wa wa raais wabunge
 
Ndo mana kuna mzee mmoja nlimsikia mahali akisema kwa utani lakini utani wenye ujumbe alisema kuwa "baada ya shetani kuingia Motoni anayefuata ni mwanasiasa halafu ndo yanafuatia makundi mengine"
 
Back
Top Bottom