Kufanya mauzo makubwa sio kupata faida

Ohooo!
 
Pakiti ya viberiti 10 inauzwa 400, ukiuza rejareja kwa 100 unapata faida ya 600!! Hii ni % ngapi??
 
Ni biashara kichaa na kula hasara ni sawa na kugusa, sasa njoo kwenye kuuza Vocha, aisee.
 
1. Mkuu ukiwauliza hao wauza maduka sidhani kama wana ndoto za kuwa Mo au Bakhresa.. Wanataka mahitaji yao yapatikane tu

2. mangi shops zinaweza kuingiza faida ukikaa sehemu yenye location nzuri lakini pia uwe na extra service mfano za kutoa pesa na vinywaji ambazo kiasi huwa zinaongeza faida

3. Mangi shops hazitakiwi kutegemewa kwa 100%, yani chakula na ada humo humo. Hapo ni ngumu kukua ndio maana wengi wanaweza kuwa na duka ila ana boda boda zinamletea hesabu

kiufupi uliyoongea mengi ni kweli mkuu
 
Vaykula vingi na vinywaji vinavyouzwa kwa supermarkets bei ni cheaper ukilinganisha na maduka ya mtaani huko..
ukizingatia bei za supermarket ni pamoja na VAT inclusive
 
Utoshe kusema mtoa post umeandika pumba tupu
Nimesoma comment zote kwa kina lakini bado hujaonesha namna ya kupata faida pindi ww utakapo uza bidhaa kwa gharama kubwa huku mwenzio akiuza kwa gharama ndogo (halisia)

Kuna kitu kimoja mtoa post huelewi, faida inapokua ndogo sio zambi muhimu ni mzunguko kama caton unapata faida ya 500 na zinatoka tano kwa siku sio mbaya kumbuka unauza na vitu vingine
 
Majibu yote nimeshayatoa humu jinsi ya kutengeneza faida ya kuanzia asilimia 20 na kuendelea kwa biashara za mitaani
 
Unachosema ni sahihi lakini inaonekana Kuna vitu hauvifahami
 


Mara nyingi biashara za Mangi huwaga faida yake ni 20-25% na mfanyabiashara akifuata kanuni hiyo ni rahisi sana kuendelea mbele.Mfano energy sehemu nyingi bei ya jumla ni elfu 12. Rejareja wanauza 14400 ukifanya mahesabu faida ni 20% kwa bei ya mia 6 per piece kama bei ikiwa Zaid itakiwa kubwa zaidi.So ikitokea Mangi akauza laki 2 kwa siku ujue gross faida yake kwa mwezi ni 1-1.5M.Ni biashara ngumu lakini ikifanywa kwa kufuata misingi yake Ina faida kubwa sana.
 
Huyu aliendika hii mada ana matatizo ya akili, eti pandisha bei ya bidhaa? Hao wateja utawapata wapi baada ya kupandisha bei?.

Haujui kwamba biashara imebebwa na ushindani? au unafikiri hiyo location utafungua peke yako? nyie ndio wale mna akili za kukalili vitu badala ya kuangalia uhalisia wa vitu
 
Usinibishie hichi nilichoandika hapa Nipo kwenye business mwaka wa kumi nauzoefu mkubwa naona jinsi biashara za mtaani zinavyoshindwa kukua au kushindwa kuleta matokeo

Kuna makosa madogo yanayofanyika katika upangaji wa bei za bidhaa

Mfano mkoa niliopo energy ya mo madukani mengi wanauza 500 faida yake ni 10%-15% wafanyabiashara makini ukienda kwenye duka lake anauza energy hiyo hiyo kwa 600 faida ya 20%-25 kaongeza sh 100 mteja hawezi kuondoka sababu ya ongezeko hilo nazani umeona gap hilo la faida hapo utapojifunza kwanini biashara moja lakini wanaofanikiwa ni wachache

Hii shilingi 100 inayoongezeka ni kubwa sana kwa mfanyabiashara anayezingatia mauzo yake ya mwezi mzima au mwaka
 
Mkoa gani kaka energy wanaouza bei hiyo
 
Mkoa niliopo mo energy inauzwa 500
Haupo, maana bei ya jumla ndoo hiyo ya 500 kwa Azam energy labda hizo energy zingine kama pawa,na Mo extra energy ambazo hata rejareja wanauza 500 maana bei ya jumla iko chini compared to Azam energy
 
Ni kweli biashara inahitaji misingi faida inapatikana
 
Hapa umenifumbua macho..... It's true ukifanya biashara center unahudumia wilaya zaidi ya moja🤔🤔🤔

Mleta mada anamaanisha lazima ulijue soko lako vizuri sio unaenda kama ng'ombe........ Umejificha maporini huko sijui unatafuta nn,, pesa au uchawi🚶🚶
 
Kukosa tu elimu kwa wafanyabiashara wengi wanashusha bei ili wauze sana bila kufikiria faida lakini naamini siku za mbeleni watu wataelimika bei iyo ndio halali kabisa inawezekana kabisa kuuza kwa bei hiyo Kuna watu hawanywi pombe kabisa watanunua
Wakipandisha Bei ni project ikatiki hata mzalishaji atapandisha bei
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…