Nilikuwa najiuliza kwa muda mrefu kwanini hizi biashara za mtaani kwanini hazikui kwanini watu hawatajiriki nyingi zinakufa
Biashara hizi zilizopo mtaani
Maduka ya vitu vya rejareja
Maduka ya vipodozi
Wachoma chips
Migahawa
Maduka ya dawa nk
Kwanini sasa biashara hizi watu hawatajiriki au kupata mafanikio makubwa sababu kubwa ni kuwa kutokuwa na elimu
Biashara za mtaani hazihitaji mauzo makubwa zinazohitaji faida kubwa
Kuna jambo moja wafanyabiashara wa mitaani hawafahamu unavyofanya biashara ni lazima ujue upo kwenye level gani
Ipo hivi kwenye biashara kama biashara yako kila bidhaa unayouza inakupa faida ya asilimia 5-10 biashara yako itakutaka uuze zaidi ya wilaya 2 ili upate faida na wengi wamefanikiwa wafanyabiasha na Mo na Azam wanasambaza energy nchi nzima kila enery faida haizidi sh 100
Jibu nikaja kupata hapa kwanini wafanyabiashara wa mtaani hawafanikiwi wanatafuta faida ndogo sawa na mtu kama Azam huku wao wanauza mtaa mmoja
Maduka ya rejareja energy inapatikana kwa 700 lakini kwa mfanyabiashara makini atauza energy 1000 sababu ukiuza 700 kwenye katoni ya juisi 12 faida 500 ni faida ndogo sana haitokufikisha popote
Anaetengeneza vocha anauza nchi nzima huku wewe unauza mtaani kwako tu vocha za shilingi elfu 20 faida haizidi 1000 kuna kutajirika hapa wadau ebu tujiongeze
Makampuni ya soda yanawataka muuze soda 700 lakini kiuhalisia soda inatakiwa iuzwe 1000 ili upate faida ukiuza soda 700 ni kama unawafanyia wenye makampuni faida utayoipata ni mbuzi
Nimekuja kujifunza kwanini ukienda supermarket bei zinaongezeka kidogo nimegundua biashara wanaifanya kisomi na ndio mana wanazidi kutajirika kama biashara hakuna wateja mtu anaona Bora afunge kuliko kuendelea kupoteza muda muuzaji wa rejareja ni lazima upandishe vitu bei ukiuza bei Ile ya soko linavyotaka ni kama kupoteza muda tu