Kufanya mauzo makubwa sio kupata faida

Kufanya mauzo makubwa sio kupata faida

Gulio Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2018
Posts
3,325
Reaction score
7,807
Nilikuwa najiuliza kwa muda mrefu kwanini hizi biashara za mtaani kwanini hazikui kwanini watu hawatajiriki nyingi zinakufa

Biashara hizi zilizopo mtaani
Maduka ya vitu vya rejareja
Maduka ya vipodozi
Wachoma chips
Migahawa
Maduka ya dawa nk

Kwanini sasa biashara hizi watu hawatajiriki au kupata mafanikio makubwa sababu kubwa ni kuwa kutokuwa na elimu

Biashara za mtaani hazihitaji mauzo makubwa zinazohitaji faida kubwa

Kuna jambo moja wafanyabiashara wa mitaani hawafahamu unavyofanya biashara ni lazima ujue upo kwenye level gani

Ipo hivi kwenye biashara kama biashara yako kila bidhaa unayouza inakupa faida ya asilimia 5-10 biashara yako itakutaka uuze zaidi ya wilaya 2 ili upate faida na wengi wamefanikiwa wafanyabiasha na Mo na Azam wanasambaza energy nchi nzima kila enery faida haizidi sh 100

Jibu nikaja kupata hapa kwanini wafanyabiashara wa mtaani hawafanikiwi wanatafuta faida ndogo sawa na mtu kama Azam huku wao wanauza mtaa mmoja

Maduka ya rejareja energy inapatikana kwa 700 lakini kwa mfanyabiashara makini atauza energy 1000 sababu ukiuza 700 kwenye katoni ya juisi 12 faida 500 ni faida ndogo sana haitokufikisha popote

Anaetengeneza vocha anauza nchi nzima huku wewe unauza mtaani kwako tu vocha za shilingi elfu 20 faida haizidi 1000 kuna kutajirika hapa wadau ebu tujiongeze

Makampuni ya soda yanawataka muuze soda 700 lakini kiuhalisia soda inatakiwa iuzwe 1000 ili upate faida ukiuza soda 700 ni kama unawafanyia wenye makampuni faida utayoipata ni mbuzi

Nimekuja kujifunza kwanini ukienda supermarket bei zinaongezeka kidogo nimegundua biashara wanaifanya kisomi na ndio mana wanazidi kutajirika kama biashara hakuna wateja mtu anaona Bora afunge kuliko kuendelea kupoteza muda muuzaji wa rejareja ni lazima upandishe vitu bei ukiuza bei Ile ya soko linavyotaka ni kama kupoteza muda tu
 
Biashara za rejareja/jumla hasa vyakula(maduka ya mangi) zina faida ndogo sana. Kiroba cha ngano mtu ananunua 40k anauza 41k, yaani faida ya buku kwenye mtaji wa 40k, na wakati huo ni ngumu kuuza viroba kumi kwa siku. Anayeuza rejareja auze kilo 25 ni lini...
 
Kukosa tu elimu kwa wafanyabiashara wengi wanashusha bei ili wauze lakini naamini siku za mbeleni watu wataelimika bei iyo ndio halali kabisa inawezekana kabisa kuuza kwa bei hiyo Kuna watu hawanywi pombe kabisa watanunua
Unajidanganya,hapo ina maanana bia itapanda bei,kumbuka huyu mtu hauzi item moja,ana item zaidi ya 200,kila item akiuza pc 10 kwa faida ya 100 ni 200,000.we kaa nyumbani usubiri kufungua kiwanda kama cha mo huku watoto wanakufa njaa
 
Nimejaribu kutoa sababu tu kwanini biashara za mitaani hazikui ama kuwapa watu mafanikio tembea mikoa Mingi biashara zipo sehemu za mijini wanakouza zaidi ya wilaya tatu hizi biashara za mitaani hata mamangi wamezikimbia siku hizi

Nimejaribu kutoa muongozo Nini kifanyike kwa hizi biashara za rejareja mitaani nyingi hazikui pia zinafungwa sababu faida ya asilimia 5-10 haijitoshelezi lazima ufunge tu biashara
 
Unajidanganya,hapo ina maanana bia itapanda bei,kumbuka huyu mtu hauzi item moja,ana item zaidi ya 200,kila item akiuza pc 10 kwa faida ya 100 ni 200,000.we kaa nyumbani usubiri kufungua kiwanda kama cha mo huku watoto wanakufa njaa
Mkuu hilo duka lipo wapi items 200 na kila item zitoke pc 10 kwa siku ?
Anachosema mtoa mada ni kweli, huu upuuzi wa kuweka faida ya mia mia kwa kusema kuna mzunguko ni kujidanganya, at least faida ingekuwa 25-40% hapo mtu faida itaonekana, ila hizi za kununua mafuta ya lita 20, kwa laki kisha unapata faida elfu 15 ni upuuzi
 
Ni biashara za kipuuzi sana sema watanzania wengi bado hawaelewi
 
Unajidanganya,hapo ina maanana bia itapanda bei,kumbuka huyu mtu hauzi item moja,ana item zaidi ya 200,kila item akiuza pc 10 kwa faida ya 100 ni 200,000.we kaa nyumbani usubiri kufungua kiwanda kama cha mo huku watoto wanakufa njaa
mmmh!? Sio rahis kuuza items 200 tofauti tofauti kwa siku kwenye duka la rejareja kama unavyo sema. Kumbuka bidha za rejareja faida yake ni ndogo au hamna kabisa ukilinganisha na mda unaotumika kuisupply bidhaa husika. Mfano aliposema mfuko wa ngano unanunua 40k alafu unakuja kuuza 41k kwamba faida ni 1000 + 1000 ya mfuko mtupu jumla faida yake 2000. Je unachukua mda gan had kuipata hio faida ya sh 2000 kwenye mfuko mmoja wa ngano?
Tusiangalie faida tu angalia pia nani mda gani unatumia kupata hio faida then uthaminishe
 
Mafanikio ya biashara yanahitaji watu wenye kujua mbinu watanzania wengi wanajua somo lakufanya mauzo hawajui somo la kutafuta faida na ndio sababu biashara nyingi hazikui miaka na miaka
ni kama unauza pilipili ili upate laki inabidi uuze debe 500 upuzi uwo na bado kweny kila debe moja la pilipili unapata faida ya 50 ndio maana unambiwa kufanya biashara sio kwa kila mtu aise business ni field kubwa sana
 
mtaji alio nao mtu.. ndio una amua akae upande upi.. kuwa muuzaji wa mwiso au kuwa muuzaji wa kati au kuwa msambazaji mkubwa... ila ni vyema sana kuanzia chini na kwenda juu mana ake una jifunza mengi sana kwenye biashara,, biashara ni kukua kila siku.. na mfanyabiashara yoyote ule nia yake yakila siku nikuwa na mauzo makubwa.. hata kama faida kidogo ndio io io ina jaza kibaba!! nyie vijana wa siku izi mnataka mafaida makubwa ghafla bin vuu!
 
Mafanikio ya biashara yanahitaji watu wenye kujua mbinu watanzania wengi wanajua somo lakufanya mauzo hawajui somo la kutafuta faida na ndio sababu biashara nyingi hazikui miaka na miaka
una mjua MNYALU CANVA.. tafuta ofisi yake uone utashangaa !! lakn ni mtu anaye kimbiza vibaya mno na kupata faida nzuri tu! ukiona ofisi yake utasema huyu mtu vipi?? mbona kama hana faida na biashara yake.
 
Kukosa tu elimu kwa wafanyabiashara wengi wanashusha bei ili wauze sana bila kufikiria faida lakini naamini siku za mbeleni watu wataelimika bei iyo ndio halali kabisa inawezekana kabisa kuuza kwa bei hiyo Kuna watu hawanywi pombe kabisa watanunua
hapo ulipo unafanya biashara gani?

watu wanataka unafuu afu unataka mtu akomae na bei kubwa..unataka muuzaji afukuze inzi tu dukani.
 
ukisema hayana faida, unakosea yasingekuwepo basi, ukisema hayakui wakati tunaona watu ana duka mtaa huu anaenda kufungua duka mtaa mwingine huko sio kukua? kumbuka hawa ni retail trade hawategemei faida kwenye bidhaa moja, duka la mangi lina sukari, mchele, unga, maharage, na ni mahitaji ya kila siku, faida ipo mkuu
 
Back
Top Bottom