Ya pumzi halafu unatakiwa usiwaze chochote.
Sio lazima meditation iwe ni kutokuwaza chochote kabisa, ingawa baadhi ya mbinu za meditation hulenga hali hiyo ya utupu wa akili. Kwa ujumla, meditation ni mazoezi ya akili ambayo yanahusisha kuleta umakini wa ndani, utulivu, na ufahamu wa sasa. Inaweza kufanyika kwa njia mbalimbali, kama hizi hapa 👇👇
Kupumua kwa umakini hii ni ile hali ya Kujikita kwenye hisia za kupumua, kwa mfano, kuhesabu pumzi zako au kuhisi jinsi hewa inavyotembea ndani na nje.
Kujikumbusha kwa ufahamu kwa maana ya Mindfulness, hii ni ile hali ya kuwa na ufahamu wa kile kinachoendelea sasa, bila kuhukumu. Hii inaweza kuwa kuhisi mwili wako, mawazo yako, au mazingira yako.
Lakini pia ipo ya Kutafakari, hii ni ile hali ya kufikiria maneno, dhana, au swali fulani kwa kina (mfano: kuzingatia maneno ya busara au sala au masomo, hii ndio njia ambayo huwa naitumia kusoma).
Pia kuna hii ya kuitwa mantra, ambayo ni hali au kitendo cha kurudia neno au sauti maalum (mfano kuna neno wanalipenda sana linaitwa "Om") na lengo la hii ni kuleta mtiririko wa utulivu kwa maana kadri unavyorudia maneno unajikuta akili na hisia zako zinazamia huko.
Kwahiyo meditation ni kama unavyopanda mti ili uweze kufika kule juu ulikokukusudia basi utadandia Kila tawi ambao unaliona ni imara vya kutosha kuubeba uzito wako pasipo kuleta madhara ya kukuangusha.
Hivyo basi, lengo la meditation si lazima mtu aweze kufanikisha kile kitendo cha kutokuwaza (na hapa ndipo ambapo watu wengi wanapotea na kushindwa kumeditate kwakua wanahisi hili ndio lengo la meditation), meditation ni kitendo cha kudhibiti mawazo au kuyashuhudia kwa namna tulivu bila kuyafuata.
Meditation ni simple sana na inaweza kufanywa kwenye mazingira yoyote yale, chagua tawi ambalo unaona litakufikisha unakotaka kwenda panda nalo taratibu.
NB: Kila aina ya meditation kati ya hizo hapo juu huwa inakitu au jambo moja inaliongeza ndani yako na ndio maana kabla hujaamua kuanza kufanya meditation unatakiwa ujue ni jambo gani utataka ulifikie au umeditate kwalo, na wale ambao wanataka kuwasiliana na ulimwengu wa juu zaidi huwa hawawezi kufika kwenye hiyo hatua kama hawawezi kuifanya akili yao iwe tupu kabisa na hii hatua huwa haifikiwi na Kila mtu.