CONSISTENCY
Senior Member
- Feb 16, 2023
- 135
- 309
Kuhusu mkataba wa bandari tumeona mapungufu makubwa ya bunge letu kuhusu namna linavyosimamia serikali, tumeona bunge limetumika kama toilet paper na serikali.
Udhaifu huo wa bunge unapelekea kuchochea zaidi mahitaji ya katiba mpya ili kuepukana na udhaifu na upumbavu kama huo wa bunge.
Hivyo sababu ya jambo hilo la udhaifu wa bunge ni vyema tukawa na mdahalo huru kuhusu huo mkataba wa bandari.
wiki chache nyuma tuliona ulipotokea mgomo wa wafanyabiashara soko la kariakoo serikali iliitisha mkutano na wananchi ili waweze kueleza changamoto zao kwa uwazi, basi pia inawezekana wananchi tukawa na mdahalo huru na serikali ili tuelimishane uzuri na ubaya wa kila kipengele katika huo mkataba wa bandari.
Jambo la bandari halina itikadi za kisiasa, kidini n.k sababu bandari inatunufaisha wananchi wote bila kujali chama, dini, kabila n.k
Hivyo wale wanaoona mkataba ule ni mzuri na ambao tunaoona mkataba haufai tukutane katika mdahalo huru ikiwezekana mdahalo ufanyike viwanja vya uhuru jijini Dar es salaam ili tujadili mkataba bila itikadi zozote sababu ni jambo la linalotoa mustakabali wa taifa na vizazi vyake.
Kwa kua mkataba ule unatetewa na serikali kwamba una manufaa makubwa sana, pia upande wa pili unapingwa na wananchi kwamba una mapungufu makubwa sana hivyo kwa ustawi, utulivu na amani ya nchi ni vyema tukawa na wawakilishi toka serikalini wakiongozwa na mwanasheria mkuu wa serikali, waziri makame mbarawa, katibu mkuu wake wa wizara n.k
Upande wa wananchi tutakua na wanasheria mbalimbali wanaoaminika, wanasheria hao watapendekezwa na wananchi baada ya kua hadi sasa tumeona michango mingi sana ya kukosoa mkataba wa bandari kwa uwazi bila hofu kabisa, michango hiyo ni ile tulioiona kutoka youtube video mbalimbali kutoka chaneli tofauti, michango hiyo ni ile liyohusu maelezo ya mapungufu ya mkataba huo wa bandari..
inabidi tufikie hatua hii sababu tulitegemea bunge ndio liwe msuruhishi wa utata wa mkataba wa bandari kati ya serikali na wananchi ila jambo la kusikitisha na fedheha mbaya ni kwamba bunge likiongozwa na spika tulia, wapambe wengine kama nape nnauye, msukuma n.k limeamua kutumika na serikali kwa kukejeli na kutisha hofu wananchi wanapoelezea mapungufu makubwa ya mkataba huo wa bandari.
Pia ni muhimu kufanyika mdahalo huo kuhusu mkataba wa bandari ili kuendelea kuimarisha ustawi, umoja, utulivu na amani ya nchi.