Uchaguzi 2020 Kufuatia kauli ya Polepole ya kuwa CHADEMA walichapisha kura bandia ili kuchafua uchaguzi, CCM tunawataka mfungue kesi kuwashtaki CHADEMA

Sasa CCM ifungue kesi kwa lipi? Imepoteza kipi? Pelekeni hayo makaratasi tume ya uchaguzi ikayachunguze kama ni original uchunguzi ufanyike na watuhumiwa wafikishwe mahakamani na kama ni fake CHADEMA na ACT wafikishwe Mahakamani waeleze walikoyatoa
 
Kufuatia kauli aliyotoa bwana Polepole kuwa CHADEMA walichapisha kura fake ili kuchafua uchaguzi, ni vyema CCM ikawashtaki hawa CHADEMA kwa kutenda kosa hilo la jinai....
Unajua kesi pia zina gharama? Wafungue kesi ili iweje wakati wameshakamata kila kitu?
 
Mwenye dhamana ya kuchukua uhaki na uhuru wa kusimamia uchaguzi upo mikononi mwa chombo gani?Ni NEC siyo? isipo tekeleza wajibu wake kikatiba ulitarajia watu waipongeze?...
Ndugu zetu upinzani walikuwa wanakumbuka walichofanyiwa na CCM kwenye Serikali za mitaa na Tume ile ile, kuna miujiza gani ambayo ilitegemewa saizi. Wangeanza kudai tume huru mara baada ya ule Uchaguzi bas kuna mambo yasingetokea saivi.
 
Kuna vitu Polepole anaongea akidhani kila mtanzania ni mjinga..SMH
 
Fuatilia taarifa ya data kamili, usikurupuke na kijipande cha kanga.
 
Kama ilikuwa ni CHADEMA, iweje, mfano, yule mama na kapu la kura katikati ya Polisi hakukamatwa na Polisi?
 
Jinai ni kesi inayohusisha wahalifu dhidi ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Na huwa haina mwisho huenda Polisi wanalifanyia kazi sio suala la CCM kufungua kesi. Subiri Polisi waanze kusaka wote waliotaka kuvuruga Uchaguzi.
 
Angalau kuna mtu amekiri kwamba kulikua na uchapishwaji wa kura feki. Kuhusu ni nani alichapisha nadhani mtu huyu inabidi aunganishwe na walalamikaji katika uchunguzi.
Haswa! amekiri uwepo wa kura feki sasa mchawi atafutwe maana Tume ilikanusha jambo hili.
 
Hata mtoto wa miaka mitano hataamini matokeo ya uchaguzi huu. Hata CCM wenye nia nzuri wanaukataa!
 
Wewe umewahi kuona wapi mtu anakamata kielelezo cha crime na yeye huyo huyo ndiye anakuwa wa kwanza kukiharibu (kukichoma moto)?

Mambo mengine ni usanii wa ajabu sana!
Ni sawa kuzichoma Polisi wakikamata zinarudi kwenye mzunguko refer madawa ya kulevya inavyokuaga....
 
Wewe umewahi kuona wapi mtu anakamata kielelezo cha crime na yeye huyo huyo ndiye anakuwa wa kwanza kukiharibu (kukichoma moto)?

Mambo mengine ni usanii wa ajabu sana!

Kwa mahakama zipi za kuzipelekea huo ushahidi? Mahakama hizi hizi ambazo anayechagua majaji ndio anaagiza wizi wa kura kwa kisingizio cha uzalendo uchwara?
 
ni sawa kuzichoma police wakikamata zinarudi kwenye mzunguko refer madawa ya kulevya inavyokuaga...

Exactly, na lengo ya kutaka wapewe wao kama ushahidi ilikuwa ni kuzirudisha kwenye kura za wizi, ama kuharibu ushahidi.
 
Ndugu zetu upinzani walikuwa wanakumbuka walichofanyiwa na CCM kwenye Serikali za mitaa na Tume ile ile, kuna miujiza gani ambayo ilitegemewa saizi. Wangeanza kudai tume huru mara baada ya ule Uchaguzi bas kuna mambo yasingetokea saivi.
Nilichogundua, laymen wengi wanapenda sana porojo kwa vitu wasivyovijua, umesema "walichofanyiwa na CCM kwenye serikali za mitaa na Tume ileile" unafahamu kwa wanaosimamia uchaguzi wa serikali za mitaa ni TAMISEMI na sio TUME, i know ulikua hujui well, ndo umejua now. So kabla hujaanza kuropoka, jipange na hoja na facts.
 
Usihangaike Arv anazochukulia Lugalo zinamsumbua huyo Chakubanga .
 
Kabla ya kufungua kesi waje kwanza na majibu kwa nini karibu nchi mzima,kuna tofauti kubwa kati ya kura za rais na wabunge. Wakati wapiga kura ni walewale.ingekukuwa tofauti ni maelfu isingekuwa shida kupata majibu kwamba wasimamizi,mawakal walipiga kura maeneo ambayo hawakujiandikisha hivyo walipiga kura ya rais na mbunge tu basi . Sasa haya malaki mhhh
 
Sikutegemea kijana msomi Kama huyu kushikwa na mapepo mabaya namna hii.
 
Wanaweza fungua kesi na unaowapenda wakasota miezi kadhaa bila dhamana.

Kipi kinashindikana? Au unasahau kuwa kuna kesi ya ugaidi inamkabili mmoja wao?
 
Kuna utafauti gani wa outcome, na pia ukisema tamisemi hao viongozi wa tamisemi( ambayo ipo chini ya serikali) wanateuliwa na nani ambae ni mtu tofauti na yule anaeteua wasimamizi wa uchaguzi mkuu( toka viongozi wa tume hadi wakurugenzi). Ukinipa utofauti huo nitakubali uniite layman nisiejua kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…