Tunawashukuru sana CHADEMA, tunajua mlitaka kuuambia umma kwamba huyu mpendwa wetu hatunaye tena duniani, na mlitaka kuitaka serikali ama ikanushe au ithibitishe jambo hilo. Wameona wawawahi ili kuficha aibu yao. Tunawatakia maisha marefu Chadema. Yeyote anayewaombea mabaya ajiandae kukutana nayo hayo mabaya. Mwigulu aliwawinda sana, lakini baadaye mambo yalimgeukia akaanza kupata mabalaa hadi ya kutumbuliwa hadi alipojikomba bungeni na kurudishwa tena kwenye madaraka.
Tujifunze kutendeana mema na kupendana.
Naomba Chadema mtakapotoa tamko lenu mmalizie na sentensi hii "Kujifunze kupendana, kutakiana mema na kutendeana mema maishani mwetu". Duniani tunapita tusijione ni wa kudumu.