Kwanza nipende kumshukuru Mungu kwa zawadi ya uhai, nimeshuhudia marais wa awamu zote 6, katika wote nilimkubali sana JK Nyerere na JPM.
Nikirejea kwenye mada, kufuatia alichokisema Mh Nappe, endapo itathibitika kuwa fedha zilizokopwa na awamu ya 5 zilitumika vibaya, wafuatao wachukuliwe hatua
1. Aliyekuwa Makamu wa Rais wa awamu ya 5 kwakuwa hakumshauri vyema mwenza wake, ikumbukwe kuwa na yeye pia alikuwepo katika karatasi ya kura ya uchaguzi mkuu na mbele ya sura yake ndiyo wapiga kura waliweka alama ya vema.
2. Waziri Mkuu wa awamu ya 5, huyu alikuwa mtendaji mkuu wa Serikali, kwanini alifumbia macho uovu huo?
3. Aliyekuwa Waziri mwenye dhamana ya fedha, huyu nayeye asipone katika sakata hili maana yeye ndiyo mwangalizi wa kila senti ya serikali inatoingia na Kutoka.
Mwisho: kama Hawa hawatachukuliwa hatua basi nachukua fursa hii kumpongeza JPM kwa aliyoyafanya kila kona ya nchi hii.
Kwa mjibu wa sheria za Tanzania mkopaji mkuu kwa niaba ya nchi ni waziri wa fedha na mipango, mgawaji wa fedha kwa kuzingatia mahitaji na mfuatiliaji matumizi ya fedha hizo. Hazina na Benki kuu ziko chini ya waziri wa fedha na mipango. Ndiye mkusanyaji mkuu wa fedha za ndani kutoka kwenye kodi,, tozo, ada, ushuru na maduhuli yote.
Ndiye signatory mwambata wa utoaji fedha kutoka benki kuu na hazina
Fanyeni mchanganuo kwa mtiririko huu ufuatao ili kubaini kwa yakini ni nani amefanya vema zaidi, ubora gani na kukubaliwa kiwango gani:
1. Julius Kambarage Nyerere-1965-1985 (mikopo, misaada, makusanyo ya mapato ya serikali na matumizi yake dhidi ya kile kilichofanyika kwa muda wa miaka ishirini madarakani kama rais wa nchi
2.Ally Hassan Mwinyi-1985-1995 (mikopo, misaada, makusanyo ya mapato yote ya serikali na matumizi yake dhidi ya kile kilichofanyika kwa muda wa miaka kumi madarakani kama rais wa nchi)
3. Benjamini William Mkpa-1995-2005 (mikopo, misaada, makusanyo ya mapato yote ya serikali na matumizi yake dhidi ya kile kilichofanyika kwa kipindi cha miaka kumi madarakani kama rais wa nchi)
4. Jakaya Halfan Mrisho Kikwete-2005-2015 (mikopo, misaada, makusanyo ya mapato yote ya serikali na matumizi yake dhidi ya kile kilichofanyika kwa kipindi cha miaka kumi madarakani kama rais wa nchi)
5. John Joseph Pombe Magufuli-2015-Machi 2021 (mikopo, misaada, makusanyo ya mapato yote ya serikali na matumizi yake dhidi ya kile kilichofanyika kwa kipindi cha miaka mitano na miezi minne akiwa madarakani kama rais wa nchi)
6. Samia Suluhu Hassan-Machi 2021-Oktoba 2021 (mikopo, misaada, makusanyo ya mapato yote ya serikali na matumizi yake dhidi ya kile kilichofanyika ndani ya muda aliokaa madarakani akiwa rais wa nchi