Kufuatia ripoti ya CAG, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Devotha Mdachi asimamishwa kazi

Kufuatia ripoti ya CAG, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Devotha Mdachi asimamishwa kazi

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Devotha Mdachi kupisha uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha na rasilimali za serikali.

IMG_20210410_134057_383.jpg

===============
DEVOTHA MDACHI
===============
"Mimi naweza kuwekwa Pembeni kwa uonevu Ila matumuzi ya Pesa kwa Oda za Serekali kuputia waziri wa Mali asili na utalii wa wakati huo ziligubikwa na mkanganyiko mwingi sana Mpaka Kuna wakati nilitafakari kujiuzuru kwa kuyaona haya, Msaidizi wangu ni Shahidi" Devotha Mdachi
=================
IMG_20210410_120625_108.jpg

BIOGRAPHY
Devota Mdachi started working with TTB in 1994 and was first employed as Tourist Information Officer, at the TTB Branch Office in Arusha. In 1998, she was transferred to Dar es Salaam, and was attached to the Tourist Information Centre.

Since then she has worked in various positions at TTB as Senior Tourist Information Officer, Principal Tourist Information Officer, Head of the Dar es Salaam Tourist Information Centre, Principal Marketing Officer, Director of Marketing, and finally Managing Director in 2016.

She is the first Tanzanian woman to hold the positions of Director of Marketing and Managing Director of the TTB. She holds a BA in international relations and advanced French language from the University of Dar es Salaam (1991); an MA in tourism from the Open University of Tanzania (2008), and post-graduate certificate in tourism from the International School of Tourism, Rome (2000).
 
Waziri Wa Mali Asili na Utalii Amemsimamisha Kazi DG Wa TTB Kupisha Uchunguzi Wa Tuhuma Dhidi Yake.

Screenshot_20210410-120926.jpg
 
Mmmh, Mungu anaumba aise, kameenda umri lakini bado kanasumbua kabisa akili zetu wanaume. Back to the topic,hili suala linajulikana kwamba shida ilianzia wizarani hadi rais wa wakati huo amewahi kuwasema waziri na katibu mkuu wake kwamba hawaelewani, huyu dada huenda katolewa KAFARA tu; swali langu ni hili, hivi wakubwa hawa huaga haiwezekani wakashtakiwa kama wanavyo shtakiwa wezi wa kuku?

Kuna mtu alisemwa sana kuhusu kua na kina aunt Ezekiel na wale wapanda mlima hewa kule Kilimanjaro, wananchi mbona tunakumbuka sana? Swali la mwisho, mhe waziri ulitwambia mara ya mwisho kwamba Burigi ya Chato ndio kitovu cha utalii kanda ya ziwa, bado unamsimamo huo huo? Ukitoka tu nje ya wizara na wewe CAG atakuja kulisema hilo, tupo hapa.
 
Ndumbaro nae sasa ajiangalie. Ushenzi afanye Kigwangala alafu kusimamishwa aje kusimamishwa dada wa watu huyu. No way Ndumbaro ajiangalie sana.
 
Kwani kigwangala hawezi naye kuunganishwa ili apate kuchunguzwa hizi tuhuma mzito kabisa?
 
Bi Devotha Mdachi amesimashwa kazi ili kupisha uchunguzi baada ya kuwepo kwa matumizi mabaya ya pesa za umma. Lakini aliyekuwa waziri kipindi hicho bado yupo tu mitaani
IMG_20210410_123300.jpg
 
Back
Top Bottom