ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
Kufuatia Hali ya upungufu wa Fedha za Kigeni hasa Dol ya Marekani,BoT yaja na maelekezo ya kudhibiti Viwango Vya Miamala Kwa mtu mmja mmja, taasisi na kampuni ikiwemo kupiga Marufuku madalali Ili kulinda Afya ya Uchumi.
Awali Waziri wa Fedha amenukuliwa akisema Kupungua Kwa mzunguko wa Dola kumetokana na Sera Mpya za Fedha za Marekani kubana Matumizi na kupunguza dollar kwenye mzunguko hivyo kuleta athari hasi kwenye Nchi zinazoendelea.
Tanzania Current Account (𝐐𝟏 - 𝟐𝟎𝟐𝟑)
Q1 2023: TZS 2.3trn/-
Q2 2022: TZS 2trn/-
The deficit is driven by import bills;
Q1 2022: TZS 6.5trn/-
Q1 2023: TZS 7.5bn/-
Resulting to foreign reserve drop to TZS 11.7trn/- Q1 2023, from 12.9trn/- of Q1 2O22.
My Take: Tupunguze utegemezi wa dollar kwenye miamala yetu na pia tuzaloshe bidhaa nyingi ndani ya Nchi.
Kwa mujibu wa maelekezo hayo mapya, miamala yote ya fedha za kigeni inayozidi thamani ya Dola za Kimarekani milioni 1 kwa muamala mmoja katika soko la rejareja, lazima ifanyike kwa bei ya soko la fedha za kigeni baina ya benki. Aidha, miamala yote ya mteja mmoja kwa siku itajumlishwa ili kujua jumla ya kiasi husika.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bwana Emmanuel Tutuba, ametoa wito kwa taasisi zinazojihusisha na biashara ya fedha za kigeni kufuata maelekezo hayo. Amesisitiza kuwa ni marufuku kufanya biashara ya fedha za kigeni na madalali wa kimataifa wa fedha za kigeni ambao hawajasajiliwa ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pia, madalali na wafanyabiashara wa fedha za kigeni wanatakiwa kuzingatia utaratibu wa kumtambua mteja (KYC) kabla ya kufanya biashara na mteja yeyote.
Kwa mujibu wa maelekezo hayo, kiwango cha juu cha mizania kati ya mali na amana katika fedha za kigeni (Foreign Exchange Net Open Position - NOP) kitakuwa asilimia 10 ya mtaji wa msingi (core capital), na kinapaswa kuzingatiwa kila wakati.
Gavana Tutuba ameagiza pia kuwa barua za udhamini (Letters of Credit - LCs) za shehena zinazopitia Tanzania (transit cargoes) zitapaswa kutokana na fedha za kigeni kutoka nchi ambako shehena hizo zinakwenda.
Gavana Tutuba amesisitiza kwamba kuzingatia matakwa yaliyoainishwa katika maelekezo hayo ni jambo la muhimu na kukiuka maelekezo hayo kutasababisha adhabu kwa mujibu wa Sheria ya Fedha za Kigeni ya mwaka 1992.
Utekelezaji wa maelekezo haya ya uendeshaji wa huduma za fedha za kigeni, kulingana na mahitaji ya soko la sasa, utaanza rasmi tarehe 1 Juni 2023. Maelekezo haya mapya, yaliyotolewa tarehe 31 Mei 2023, yanafuta maagizo yaliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania tarehe 6 Aprili 2020. Gavana amewakumbusha wahusika wote wa huduma za fedha za kigeni kuzingatia matakwa ya mpango wa fedha za kigeni nchini wakati wote.

===