ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
- Thread starter
- #41
Mikopo ulikuwepo,ipo na itaendelea kuwepo Toka zamani za Mwalimu.Miradi mikubwa ya kimkakati kama mradi wa reli mpya ya SGR, Ujenzi wa Bwawa la JNHPP wa Stiegler's Gorge Rufiji mikopo yake sijui inaiva lini pia malipo na madeni ya taifa yalitoiva yanayohitaji kulipwa kwa wakati wake nayo yanazidi kuielemea akiba ya fedha za kigeni ya Tanzania iliyopo katika Dola za Kimarekani.
Manunuzi ya vitu ambavyo vingeweza kuzalishwa nchini kama mafuta ya kula / kupikia, nondo za ujenzi, simenti, sukari, nafaka ya ngano, samaki n.k vyote hivi hununuliwa kwa wingi kutoka nje wakati uwezo, malighafi, ardhi na mazingira ya kuvizalisha kwa wingi upo nchini Tanzania.
Manunuzi ya vitu kama bidhaa za fenicha, viatu, mikoba n.k vingeweza kuzalishwa nchi bila kutumia fedha nyingi kuviagiza nje
Suala hili la upungufu wa akiba ya fedha za kigeni yaani dola ya Kimarekani na uwiano usiofaa wa kutegemea kununua vitu vingi nje kwa fedha za kigeni kuliko tunachouza nje ni shituo la kuitahadharisha serikali kuja na mikakati mipya na sera madhubuti ya kuweza kupunguza uchumi wetu kufungamana na utegemezi wa kila kitu kutoka nje.
So usijisumbue sana maana Tanzania haipo kwenye debt distress yeyote ,wanachofanya Sasa ni kujaribu kufanya mitigation mapema Ili tusije fikia kwenye Hali ya kushindwa kuagiza bidhaa