31 May 2023
Mwigulu Lameck Nchemba waziri wa fedha afafanua sababu za uhaba dola za Kimarekani nchini Tanzania
DKT. NCHEMBA AWAAGIZA WATAALAM WA UCHUMI WA KITAIFA NA KIMATAIFA KUTAFUTA SULUHU YA UPUNGUFU WA DOLA ZA MAREKANI KATIKA SOKO LA FEDHA
31 May, 2023
Dodoma, Tanzania
Na Farida Ramadhani-Dodoma
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amewaagiza wataalamu wa Wizara ya Fedha na Mipango na ujumbe kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), kujadili namna ya kushughulikia athari za upungufu wa dola za Kimarekani katika mzunguko wa fedha ili kunusuru uchumi wa nchi zinazoendelea.
Mhe. Dkt. Nchemba (Mb) ametoa maagizo hayo wakati wa kufungua kikao kilichowashirikisha wataalam kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) unaoongozwa na Bw. Harris Tsangaride waliowasili nchini kwa ajili ya kufanya tathimini ya Program ya Huduma za Mikopo - Extended Credit Facility (ECF) (EFC), kwa kushirikiana na wataalam wa ndani wa Serikali.
Alisema mabadiliko ya Sera za Fedha nchini Marekani ya kubana matumzi na kupunguza dola kwenye mzunguko wa fedha, yameleta athari zinazoonekana mpaka kwenye nchi zinazoendelea, ikiwemo Tanzania.
"Tumekuwa tukirejea Covid-19 / Uviko na vita baina ya Urusi na Ukraine kama moja ya vitu vinavyoathiri uchumi wa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania lakini upungufu wa dola unaathiri uchumi kwa kiwango kikubwa ikiwemo uagizaji wa mafuta na uagizwaji wa bidhaa mbalimbali zinazotumika katika shughuli za Sekta Binafsi", alisema Dkt. Nchemba.
Alisema ni vema kutafuta namna ya kushughulikia jambo hilo kisera ili kunusuru nchi zinazoendelea kwa kuwa sekta ya nje ni muhimu katika kuchochea ukuaji wa uchumi wa ndani.
Kwa upande wake Kiongozi wa ujumbe kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Bw. Harris Tsangaride, alisema Shirika hilo litaendelea kushirikiana na Tanzania ili kuhakikisha nchi inaendelea kupiga hatua kiuchumi na kijamii.
Bw. Harris Tsangaride amepongeza Serikali kwa Sera zake nzuri ambazo zinaendelea kutekelezwa katika kukabiliana na athari za vita ya Ukraine na kuongeza kuwa ni matarajio yao kuwa zitaendelea kuchokea ukuaji wa uchumi na maisha ya wananchi.
Bw. Tsangaride alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi chache katika kanda ambazo zinafanya vizuri katika kutekeleza programu mbalimbali kwa kushirikiana na Shirika hilo na hivyo katika kikao hicho watajadiliana namna bora ya kuendelea kuiona nchi ikifanya vizuri zaidi.
Mwisho.
Source :
Tovuti ya wizara ya fedha tanzania
More info :
Country Report No. 2023/153
United Republic of Tanzania: 2023
Article IV Consultation and First Review Under the Extended Credit Facility (ECF) Arrangement -Press Release; Staff Report; and Statement by the Executive Director for the United Republic of Tanzania
Spillovers from the war in Ukraine and shortfalls in rainfall stalled Tanzania’s recovery from the COVID-19 pandemic. Despite fuel and fertilizer subsidies, inflation has picked up in recent months, approaching the Bank of Tanzania’s target. External balances deteriorated significantly last year due in large part to spillovers from the war in Ukraine.
Series:
Country Report No. 2023/153
Subject:
International organization Monetary policy
Source :
United Republic of Tanzania: 2023 Article IV Consultation and First Review Under the Extended Credit Facility Arrangement-Press Release; Staff Report; and Statement by the Executive Director for the United Republic of Tanzania