Kufuatia upungufu wa dola, BoT yatoa maelekezo ya kudhibiti Viwango Vya Miamala

Kufuatia upungufu wa dola, BoT yatoa maelekezo ya kudhibiti Viwango Vya Miamala

Dkt. Abdallah Tego abainisha hatua gani za maamuzi magumu ya kisiasa ndiyo yatarekebisha hali hii ya Tanzania kukumbwa na upungufu wa dola


Kufuatia kuadimika kwa Dola ya Marekani tumemtafuta mtaalamu wa masuala ya kifedha Dkt. Abdallah Y. Tego kutuchambulia masuala yenyewe ni haya yafuatayo:

Fiscal revenue measures
Clearance of external arrears
Governance reform
Banking sector restructuring plan
Curbing Government expenditure

Bio:
Dr. Abdallah Yahya Tego is a holder of BA (Ed) (Hons) from University of Uganda, MA in Islamic Studies from Muslim College London and PhD in Economics (Islamic Microfinance) from Omdurman Islamic University Khartoum Sudan.

Sheikh Tego has more than 15 years working experience in the Islamic Finance profession, he has served various Shariah Advisory Boards for several banks including KCBT Sahl Banking Shariah Advisory Board as a member.


Currently he is a lecturer at Muslim University of Morogoro.
Sheikh Tego has more than 15 years working experience in the Islamic Finance profession, he has served different Shari’ah Boards for the banks including AMANA Bank, NBC and now serving KCBT Sahl
Banking Shari’ah Advisory Board as a member.
 
Naomba namna kupata GB za bure.Kwa tigo au airtel na voda.
 
Wanajizalilisha tu mbele ya dunia sikutegemea miaka 800, Mwigulu angeweza ongea kauli ile maamuzi ya US yana athari kwa Tanzania.

Monetary policies za US aziwezi kuwa na impact kwa nchi zingine, wao wanajikita na kupambana na inflation rate huko kwao.

FED kuongeza interest inafanya kukopa kunakuwa na gharama zaidi. Matokeo yake familia zenye floating interest kwenyr mortgage, higher purchase za magari na madeni mengine ya riba; bei ya kugharamia hayo madeni inakuwa kubwa interest rate inapopanda.

Matokeo yake kwa familia disposal income inapunguwa na kupelekea kuacha unnecessary purchases za familia. Upande wa biashara gharama za mikopo inapokuwa kubwa na kwenyewe investments zinapungua, bei ya bidhaa zinapanda, demand inapungua, na mzunguko wa hela unapungua; overtime price zinakuwa stable.

Sasa hayo mambo yanahusiana vipi na wewe na wa nchi ya tatu ambae akiba yako source yake kubwa ni mauzo ya nje unayofanya kwa dollar ambayo ni average for the most part na upungufu ni manunuzi.

Wakati huo bank kuu kwa siku ilikuwa inatoa $1 million kwa matumizi ya ndani. Ilhali kuna mijitu inapata hela za wizi kirahisi; sasa kama inafanyia biashara za nje hizo hela au inahifadhi kwa dollar imepelekea demand kuongezeka na kufanya BoT ianze kuachia $2 million mbili kwa siku. Hizo zilikuwa hatua za mwezi January; na bado supply aitoshi leo sijui imefikia kiasi gani kwa siku.

Hao watu wa IMF wamemsikiliza tu Mwigulu akijidhalilisha tu. Ndio wengine huwa tunauliza hivi hawa watu uwa wanaongea vitu gani kwenye mikutano yao na wawekezaji au wataalamu wa sector kwa sababu uelewa wao daah.
Nondo za maana umeshusha kwa uelewa wangu wa ABC za uchumi.

Lakini hizi rate kuna kipindi cha awamu ya tano zilikuwa zinashushwa gradually? Nini kilipelekea kusimamisha ushushaji wa riba kwa mikopo?

Kudos mkuu.
 
Mh. Dr. Saada Mkuya Salum waziri wa fedha Zanzibar agusia sababu ya upungufu wa dola


siku za karibuni pesa ya Marekani (Dola) imeendelea kuadimika kwenye maeneo mbalimbali duniani hali inayosababisha changamoto kwa matumizi yanayohitajia pesa hiyo ikiwemo ununuaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi.

Bio:
Dr. Sanda Mkuya Salum holds a Masters of Business Administration from Heriot-Watt University in Edinburgh, Scotland, and a PhD in Business Administration from the Open University of Tanzania (OUT).
 
Nondo za maana umeshusha kwa uelewa wangu wa ABC za uchumi.

Lakini hizi rate kuna kipindi cha awamu ya tano zilikuwa zinashushwa gradually? Nini kilipelekea kusimamisha ushushaji wa riba kwa mikopo?

Kudos mkuu.
My post ilikuwa inaongelea hatua za US central bank katika kupambana na inflation huko kwao na kuonyesha hakuna uhusiano wa karibu na Tanzania kuleta madhara.

Swali lako ni tofauti kidogo na hiyo hoja ya juu; kwa nilivyoelewa unauliza nini kinachangia kupanda au kushuka kwa interest rates za commercial banks, Tanzania.

Hilo swali ni refu kidogo kulielezea ntajaribu kulifupisha hope utapata picha. Kawaida kuna mambo makuu matatu yanayochangia banks kwenye kuamua interest rate ya kukopeshea.

Mainly inajumuisha rate ya wao waliyokopea kwenye hiyo hela wanayokupa, jumlisha rate ya inflation na mwisho rate ya faida. Hiyo ni kwa kifupi kuna rate pia inaweza ongezwa depending na default risk factors za mkopaji.

Matokeo yake ukijumlisha zote hizo unakuta interest rate zipo kwenye double digits Tanzania; sometimes higher than necessary with pressure banks wanaweza shusha. Personal sifuatilii sana riba za banks Tanzania so siwezi testify tofauti ya administration yoyote.
 
Magufuri alifunga hizi Bureau de change za mtaani zisizo na leseni au uhalali wa kufanya mabadilishano ya fedha, mkamuona ana roho mbaya, haya leo mnaona balaa lake.
 
Our economy is heading to a cliff. Bila shaka vihela vyote vya kigeni vinaishia kulipa riba za mikopo mingi mingi iliyokopwa kwa pupa na kificho.

Historia inaweza kujirudia,
Mkapa alikuwa na kazi ngumu ya kurejesha uchumi kwenye reli baada ya mtangulizi wake kuharibu kwelikweli.

Magufuli akalazimika kufanya hivyo hivyo baada ya mtangulizi wake naye kuharibu.
Samahani naomba nikusahihishe mkuu, unatakiwa useme, "Our economy is headed for a cliff.
 
Our economy is heading to a cliff. Bila shaka vihela vyote vya kigeni vinaishia kulipa riba za mikopo mingi mingi iliyokopwa kwa pupa na kificho.

Historia inaweza kujirudia,
Mkapa alikuwa na kazi ngumu ya kurejesha uchumi kwenye reli baada ya mtangulizi wake kuharibu kwelikweli.

Magufuli akalazimika kufanya hivyo hivyo baada ya mtangulizi wake naye kuharibu.
Kuna watu wanadhani urais ni ufalme badala ya kujua kuwa nafasi hiyo ni ya utumishi kwa nchi. Ikulu ni mahali patakatifu!

Mtanikumbuka.
 
Ama wewe kweli mzalendo uchwara unaechagua wa kumpa lawama. Huyo mtangulizi wa Mkapa aliukuta uchumi wa aina gani hata akauharibu? Umesahau vita vya Kagera vilivyoua kila kitu leo lawama unamtupia Mwinyi?

Na huyo Magu na miradi yake inayokunywa fedha ya SGR, daraja na JNHPP unadhani vifaa vilikuwa vinanuliwa kwa fedha za kienyeji?

Be realistic man, wacha lawama za upande upande. NI Mkapa tu ndiye aliyeweza kunyoosha uchumi ukawa na muelekeo.
Aliyemtangulia mkapa wakati wake ndio Structure Adjustment Programs zilifanyika na officially tukaingia katika mfumo wa kiuchumi wa kibepari ingawa ukiuliza hawa wapuuzi wanasema sisi ni taifa la kijamaa, ujamaa my foot.

Kutokea pale pesa nyingi sana ziliingia na kuingizwa kwenye mashirika ya bima, bandari, kilimo, mabenki etc. Kwakifupi ilikuwa neema sana pesa ilikuwa ni nyingi sana na huyu magufuri tuliyekutana nae 2015 - 2020 tungempata wakati ule basi hili taifa lingesonga mbele sana ila kwa bahati mbaya mzee Ruksa walimuonea kama wanavyomuonea huyu mama kwa kuzipiga zile pesa especially shirika la bima.

Walipiga sana na kuyafilisi mashirika ya uma huku wakiacha madeni lukuki. Mafisadi hawakuanza leo. Huyu mama na aliyefuata baada ya mkapa wote ni changamoto katika kudeal na waharibifu wa uchumi maana unatakiwa kuwa mtata kweli kweli.
 
Miezi michache tu baada ya Rais wa Tanzania Samia Suluhu kusema kwa ujasiri kwamba nchi iko katika hali nzuri kiuchumi, sasa inaanza kuonekana kama alizungumza mapema sana na anaweza kulazimika kumeza maneno yake.

Suluhu, akizungumza katika mkutano wa hadhara wa Siku ya Wanawake Duniani mapema Machi mwaka huu, alisema Tanzania imeimarika kiuchumi kuliko Nchi nyingine zote za Afrika Mashariki.

 
Wewe ni zero brain, reserve ni $6.7 billion in October 2021 at ukitoa huo mkopo wa $600 million; bado reserve ni kubwa kushinda iliyopo leo na wakati wowote katika historia ya Tanzania.

Baada hapo awajawahi kufikia tena kiwango cha $6 billion reserve, if anything imeendelea kupungua tu mpaka kufikia chini ya $5 billion.

Mwisho nikusaidie extended credit facility upewi yote kwa mkupuo ndio maana unaona IMF wapo nchini kuidhinisha awamu nyingine ya mgao katika hizo hela walizoahidiwa 2021.
Kwa sasa ni chini ya 4.9
 
Ufisadi unasababisha majizi kusaka dola ili yakafiche kwenye akaunti za nje ili yanapopeleka wake zao kujifungulia marekani basi yawe na dola za kutosha kwenye akaunti zao.
 
Pamoja na hatua hizo na maelezo ya Waziri Mwigulu juu ya uhaba wa dola, taifa litaweza kupata ufumbuzi wa tishio linalojitokeza kama zitabuniwa sera na kutekeleza mipango itakayoongeza maunzo ya njena kupata fedha nyingi za kigeni na wakati huo huo kudhibiti matumizi ya fedha za kigeni.

Tusipojifunga mkanda katika matumizi ya kianasa ndivyo hivyo akiba ya fedha za kigeni itazidi kupungua na kusababisha changamoto tusizotegemea. Tutafakari, tusitafute mchawi.
Watu wanafikiria tu kuagiza ma viieite ya viongozi na kuanzisha miradi ya kimchongo ya kilimo sijui na umeme jua.....hovyo kabisa.
 
Our economy is heading for a cliff. Bila shaka vihela vyote vya kigeni vinaishia kulipa riba za mikopo mingi mingi iliyokopwa kwa pupa na kificho.

Historia inaweza kujirudia,
Mkapa alikuwa na kazi ngumu ya kurejesha uchumi kwenye reli baada ya mtangulizi wake kuharibu kwelikweli.

Magufuli akalazimika kufanya hivyo hivyo baada ya mtangulizi wake naye kuharibu.
Haya huwa yanatokea endapo kiongozi akishindwa, akianza vizuri huwa mnapiga vigelegele.

Kama Magufuli alifanya hivyo kwa kurekebisha yaliyoharibiwa na waliopita basi hatukupaswa kumpa sifa pale ambapo mambo yalienda vizuri, tungewapa waliopita.

Hata sasa mambo yakienda vizuri ni ya sasa, yakihribika ni waliopita. Mnafanya watu kama mazuzu.
 
Banking sector restructuring plan
Curbing Government expenditure

MIKOPO MINGI YA KIBIASHARA DUNIANI IMEKUWA YA GHARAMA KUBWA, SASA TUNAGEUKIA MIKOPO YA NDANI​

mikopo mingi ya kibiashara Duniani imekuwa ikipatikana kwa gharama kubwa

29 May, 2023
NCHI ZA KUSINI MWA AFRIKA ZAGEUKIA MIKOPO YA NDANI

Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Madeni wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Japhet Justine, akifungua mkutano wa Wataalamu 30 kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Natu El- Maamry Mwamba, unaofanyika jijini Arusha.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Natu El- Maamry Mwamba, amesema kuwa nchi za Kusini mwa Afrika zinaangalia namna ya kuendeleza soko la ndani la mitaji kwa kutumia Hati fungani ili kuziwezesha kupata mikopo ya ndani wakati ambao mikopo mingi ya kibiashara Duniani imekuwa ikipatikana kwa gharama kubwa.

Hayo yamebainishwa jijini Arusha kwa niaba yake na Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Madeni wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Japhet Justine, wakati wa Mkutano wa Wataalamu wa masuala ya uchumi na fedha wanaosimamia madeni ya nchi zao kutoka nchi 16 za kusini mwa Afrika.

Bw. Japhet Justine amesema kuwa nchi za kusini mwa Afrika zinaangalia namna ya kutumia Soko au Hati fungani za ndani ambazo ni za muda mfupi, wa kati na mrefu zinatoa nafuu kubwa kwa nchi za Afrika, kwa kuwa mikopo ya aina hiyo ni nafuu na haihitaji matumizi ya dola wala uwekezaji wa nje na haina shinikizo wakati huu ambao soko la Dunia halifanyi vizuri.

“Duniani mikopo ya kibiashara inapatikana kwa gharama kubwa, hivyo mikopo ya ndani itakuwa sehemu ya hatua muhimu ya kuzisaidia nchi za Afrika kufanikisha ufadhili wa bajeti kwa ajili ya maendeleo yao”, alisema Bw. Justine.

Bw. Justine alieleza kuwa kuliendeleza Soko la ndani la Hati Fungani kunatoa fursa kwa nchi za Afrika kufanya vizuri zaidi, ambapo Tanzania kwa sasa inapata mikopo ya zaidi ya trilioni saba kutoka soko la ndani ambayo husaidia kufanikisha bajeti Kuu ya Serikali.

Aliongeza kuwa zipo nchi ambazo zinafanya vizuri katika bajeti zao kwa kutumia fursa ya soko hilo ikiwemo Namibia ambayo zaidi ya asilimia 80 ya Bajeti yake inatokana na mikopo ya ndani kupitia hati fungani zake.

Alisema Mkutano huo utajadili na kuchambua aina ya hati fungani za ndani zinazotolewa huwa na manufaa katika kukuza uchumi wakati ambao mikopo inapopungua kutoka kwa wakopeshaji wa kimataifa na pia wakati huu ambao Soko la hati fungani la Ulaya limepungua kwa kiasi kikubwa.

Aidha amewataka wajumbe wa Mkutano huo kuhakikisha wanakuwa na majadiliano yenye tija na kubadilishana uzoefu ili kuzisaidia Serikali za nchi zao katika kufikia maendeleo endelevu.

Bw. Justine amezipongeza nchi zote zilizoleta wawakilishi wao na pia amewataka wajumbe wa mkutano kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania Bara na Zanzibar.

Mkutano huo umezishirikisha nchi za kusini mwa Afrika ikiwemo wenyeji Tanzania, Namibia, Zambia, Zimbabwe, Malawi, Afrika Kusini, Uganda, Kenya, Sudani Kusini na Ethiopia.
Mwisho
Source : NCHI ZA KUSINI MWA AFRIKA ZAGEUKIA MIKOPO YA NDANI | MoF - Ministry of Finance and Planning
 
Back
Top Bottom