Kufuatia upungufu wa dola, BoT yatoa maelekezo ya kudhibiti Viwango Vya Miamala

Kufuatia upungufu wa dola, BoT yatoa maelekezo ya kudhibiti Viwango Vya Miamala

Miradi mikubwa sana ya kimkakati iliyoanzishwa kwa wakati (mkupuo) mmoja inayotumia fedha za kigeni.

Miradi hiyo kama kuhamishia makao makuu Dodoma ambapo kukamilisha nakshi mifumo ya lifti n.k, mradi wa reli mpya ya SGR, Ujenzi wa Bwawa la JNHPP wa Stiegler's Gorge Rufiji, daraja la Busisi, ndege za cash / fedha tasilimu ATCL n.k mikopo yake sijui inaiva lini pia malipo na madeni ya taifa yaliyoiva yanayohitaji kulipwa kwa wakati wake nayo yanazidi kuielemea akiba ya fedha za kigeni ya Tanzania iliyopo katika Dola za Kimarekani.

Manunuzi ya vitu ambavyo vingeweza kuzalishwa nchini kama mafuta ya kula / kupikia, nondo za ujenzi, simenti, sukari, nafaka ya ngano, samaki n.k vyote hivi hununuliwa kwa wingi kutoka nje wakati uwezo, malighafi, ardhi na mazingira ya kuvizalisha kwa wingi upo nchini Tanzania.

Manunuzi ya vitu kama bidhaa za misumari, fenicha, viatu, mikoba, vifaa vya umeme, mafeni, mapambo ya nyumba, mapazia n.k vingeweza kuzalishwa nchi bila kutumia fedha nyingi kuviagiza nje

Suala hili la upungufu wa akiba ya fedha za kigeni yaani dola ya Kimarekani na uwiano usiofaa wa kutegemea kununua vitu vingi nje kwa fedha za kigeni kuliko tunachouza nje ni shituo la kuitahadharisha serikali kuja na mikakati mipya na sera madhubuti ya kuweza kupunguza uchumi wetu kufungamana na utegemezi wa kila kitu kutoka nje.
Mliposema mnafungua nchi mlimaanisha nini? Mmesema mara nyingi kuwa FDI imeongezeka haijawahi kutokea. sasa hivi mambo yapo mrama mnaokoteza sababu
 
Uwezi ku record unrealised income kwenye vitabu vyako vya mapato.

Anyway kwenye hoja yako nilikuwekea income yote hiyo tena kwa estimate ya juu $600 na bado reserve ikabaki $6 billion.

Hayo mengine hayana msingi sana na hoja yako; na nilijua ni juu ya uwezo wako kuyaelewa 🫣be it ni very basic.

👋
Zero brain na huku Turkey wizi na ulanguzi ndio umesababisha negative forex si ndio? 😁😁😁😁😁
 
Mliposema mnafungua nchi mlimaanisha nini? Mmesema mara nyingi kuwa FDI imeongezeka haijawahi kutokea. sasa hivi mambo yapo mrama mnaokoteza sababu
 
Zero brain na huku Turkey wizi na ulanguzi ndio umesababisha negative forex si ndio? 😁😁😁😁😁
Uwe unasoma zaidi ya kichwa cha habari kwenye hizo source zako maelezo yote yamo humo.

Hela yao imepoteza thamani ya 33% kwa miaka miwili mfululizo, so watu wamekuwa wakinunua dollar kama reserve ya hela zao; woga uchaguzi ungeangusha zaidi kiwango cha hela yao watu wengi wamekimbilia dollar na kupelekea huo uhaba.

Hakuna nchi inayoguswa na sera za US kama zipo ni zile chache ambazo zinafanya nae biashara kubwa; ila sio hivi vi nchi vya third world.
 
Uwe unasoma zaidi ya kichwa cha habari kwenye hizo source zako maelezo yote yamo humo.

Hela yao imepoteza thamani ya 33% kwa miaka miwili mfululizo, so watu wamekuwa wakinunua dollar kama reserve ya hela zao; woga uchaguzi ungeangusha zaidi kiwango cha hela yao watu wengi wamekimbilia dollar na kupelekea huo uhaba.

Hakuna nchi inayoguswa na sera za US kama zipo ni zile chache ambazo zinafanya nae biashara kubwa; ila sio hivi vi nchi vya third world.
Nyumbu ni nyumbu tuu
 
Waondoe urasimu kwenye kubadili pesa za kigeni,pesa zangu mashart kibao Mara kitambulisho sijui Nini.
Waruhusu maduka ya kubadili pesa yawe mengi Kama zamani
 
Kwani wachumi wetu na Gavana wa BOT,wanashauri nini, namna ya kujikwamua kutoka kwenye mkwamo huo.?
 
Nyumbu ni nyumbu tuu
Kama kawaida yako poyoyo uelewi unacholeta.

Central bank zina akiba dollars na ya hela za ndani. India wao wanachangan’ya na Rupee kwenye hesabu zao.

Thamani ya dollar imepanda, kwa hivyo wakifanya conversion ya reserve za Rupee kwenye dollar (with current exchange rate) thamani ya akiba yao total inapungua.

Lakini si kwamba wana uhaba wa dollar.
 
Mh. Dr. Saada Mkuya Salum waziri wa fedha Zanzibar agusia sababu ya upungufu wa dola


siku za karibuni pesa ya Marekani (Dola) imeendelea kuadimika kwenye maeneo mbalimbali duniani hali inayosababisha changamoto kwa matumizi yanayohitajia pesa hiyo ikiwemo ununuaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi.

Bio:
Dr. Sanda Mkuya Salum holds a Masters of Business Administration from Heriot-Watt University in Edinburgh, Scotland, and a PhD in Business Administration from the Open University of Tanzania (OUT).

Bank of Tanzania keep enough gold reserve then you will have no problem in monetary exchange the problem now is the exchange rates . Paying your debt is expensive in dollars because bank rates are high borrowing is expensive
 
Lile jiwe vp
Kufuatia Hali ya upungufu wa Fedha za Kigeni hasa Dol ya Marekani,BoT yaja na maelekezo ya kudhibiti Viwango Vya Miamala Kwa mtu mmja mmja, taasisi na kampuni ikiwemo kupiga Marufuku madalali Ili kulinda Afya ya Uchumi.

Awali Waziri wa Fedha amenukuliwa akisema Kupungua Kwa mzunguko wa Dola kumetokana na Sera Mpya za Fedha za Marekani kubana Matumizi na kupunguza dollar kwenye mzunguko hivyo kuleta athari hasi kwenye Nchi zinazoendelea.

Tanzania Current Account (𝐐𝟏 - 𝟐𝟎𝟐𝟑)
Q1 2023: TZS 2.3trn/-
Q2 2022: TZS 2trn/-

The deficit is driven by import bills;
Q1 2022: TZS 6.5trn/-
Q1 2023: TZS 7.5bn/-

Resulting to foreign reserve drop to TZS 11.7trn/- Q1 2023, from 12.9trn/- of Q1 2O22.


My Take: Tupunguze utegemezi wa dollar kwenye miamala yetu na pia tuzaloshe bidhaa nyingi ndani ya Nchi.


Kwa mujibu wa maelekezo hayo mapya, miamala yote ya fedha za kigeni inayozidi thamani ya Dola za Kimarekani milioni 1 kwa muamala mmoja katika soko la rejareja, lazima ifanyike kwa bei ya soko la fedha za kigeni baina ya benki. Aidha, miamala yote ya mteja mmoja kwa siku itajumlishwa ili kujua jumla ya kiasi husika.

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bwana Emmanuel Tutuba, ametoa wito kwa taasisi zinazojihusisha na biashara ya fedha za kigeni kufuata maelekezo hayo. Amesisitiza kuwa ni marufuku kufanya biashara ya fedha za kigeni na madalali wa kimataifa wa fedha za kigeni ambao hawajasajiliwa ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pia, madalali na wafanyabiashara wa fedha za kigeni wanatakiwa kuzingatia utaratibu wa kumtambua mteja (KYC) kabla ya kufanya biashara na mteja yeyote.

Kwa mujibu wa maelekezo hayo, kiwango cha juu cha mizania kati ya mali na amana katika fedha za kigeni (Foreign Exchange Net Open Position - NOP) kitakuwa asilimia 10 ya mtaji wa msingi (core capital), na kinapaswa kuzingatiwa kila wakati.

Gavana Tutuba ameagiza pia kuwa barua za udhamini (Letters of Credit - LCs) za shehena zinazopitia Tanzania (transit cargoes) zitapaswa kutokana na fedha za kigeni kutoka nchi ambako shehena hizo zinakwenda.

Gavana Tutuba amesisitiza kwamba kuzingatia matakwa yaliyoainishwa katika maelekezo hayo ni jambo la muhimu na kukiuka maelekezo hayo kutasababisha adhabu kwa mujibu wa Sheria ya Fedha za Kigeni ya mwaka 1992.

Utekelezaji wa maelekezo haya ya uendeshaji wa huduma za fedha za kigeni, kulingana na mahitaji ya soko la sasa, utaanza rasmi tarehe 1 Juni 2023. Maelekezo haya mapya, yaliyotolewa tarehe 31 Mei 2023, yanafuta maagizo yaliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania tarehe 6 Aprili 2020. Gavana amewakumbusha wahusika wote wa huduma za fedha za kigeni kuzingatia matakwa ya mpango wa fedha za kigeni nchini wakati wote.
 
Kama kawaida yako poyoyo uelewi unacholeta.

Central bank zina akiba dollars na ya hela za ndani. India wao wanachangan’ya na Rupee kwenye hesabu zao.

Thamani ya dollar imepanda, kwa hivyo wakifanya conversion ya reserve za Rupee kwenye dollar (with current exchange rate) thamani ya akiba yao total inapungua.

Lakini si kwamba wana uhaba wa dollar.
Naendelea kupiga kwenye mshono 😁😁
 
Back
Top Bottom