Kufukuzwa Membe CCM: Hakika siasa ni Mchezo kama ilivyo Karata na Draft

Kufukuzwa Membe CCM: Hakika siasa ni Mchezo kama ilivyo Karata na Draft

jd41

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2015
Posts
3,756
Reaction score
4,847
Wanabodi Salaam.

Ikiwa taarifa za kufukuzwa uanachama wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu. Bernard Camilius Membe zikiwa bado zinatikisa mimbari ya siasa Tanzania, nimejikuta ninakumbuka matukio machache kabla ya uchaguzi mkuu uliopita mwaka 2015.

Ikumbukwe wakati ule mgombea aliekuwa anapewa nafasi ya kupeperusha bendera ya CCM kwenye uchaguzi mkuu alikuwa ni Ndg. Edward Lowassa, japo baadae aliikosa ile nafasi ikaangukia kwa Rais John Magufuli.

Hata hivyo wachambuzi wa mambo walibainisha kwamba Ndg. Membe ndie alikuwa chaguo la Rais mstaafu Kikwete, lakini kutokana na joto lililokuwepo ndani ya mkutano mkuu wakati ule baada ya jina la Lowassa kukatwa ikabidi ampitishe Rais Magufuli kuwa mgombea wa CCM ili kutuliza hali ya mambo.

Hii ilisababisha Ndg. Lowassa aondoke CCM (sio kwa kufukuzwa) na kuelekea upinzani CHADEMA ambapo aligombea urais japo hakushinda. Membe kwa upande wake aliendelea kuwa mwanachama wa CCM, mpaka leo alivyofukuzwa uanachama.

Tukikumbuka matukio machache yaliyotokea miezi michache iliyopita ambapo kwanza Ndg. Lowassa alirejea CCM, akiongozana na rafiki yake Ndg. Rostam Aziz, ambao kwa nyakati tofauti wote waliondoka CCM chini ya uenyekiti wa Rais Mstaafu Kikwete, sasa hao wote wamerejea CCM na kuongeza nguvu upande wa Rais Magufuli, halafu yule aliekuwa kipenzi cha Mwenyekiti aliepita (Kikwete) amefukuzwa uanachama wake, hivyo kumuondoa kabisa kwenye system kwasababu alionekana threat kwa Rais Magufuli.

Hii inaonesha siasa ni mchezo kama ilivyo michezo mingine karata (last card), na draft, siku zote wachezaji wa hiyo michezo huficha karata zao au kete kumvizia mpinzani wao wampe pigo la kushtukiza waumalize mchezo.

Hili linaweza kuthibitishwa kutokana na kelele zilizozuka siku za karibuni kwamba Ndg. Membe anaweza kuomba nafasi ndani ya CCM aweze kupitishwa kugombea nafasi ya urais ambayo imezoeleka Rais aliepo madarakani hupewa nafasi ya kumalizia muhula wa pili wa utawala wake, hii inaweza kuwa ndio sababu ya Membe leo kufukuzwa uanachama wake ndani ya CCM, na sio sababu za kinidhamu kama zilivyoainishwa na Pole Pole ambazo hazionekani kuwa na direct impact kwa Magufuli ku-seek his second term.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MBINU HIYO sasahv anaingia ACT wazalendo hadi tunaelekea Kwenye uchaguzi mkuu watakuwa wanasikika ZZK na MEMBE na sio TL na Mbowe na chadema yao halafu baasda ya uchaguzi anarudi ccm kuunga mkono juhudi lengo lao Kuiua chadema na kuinyanyua ACT kuwa chama kikuu cha upinzani,ndiomaana zzk katengenezewa kashfa za kumpa umaarufu tu kuelekea uchaguzi
 
Hata kama membe aende chama cha upinzani!hatoruhusiwa tume ya uchaguzi kugombea uraisi!sabb sheria mpya ya vyama vya siasa inamtaka mgombea kukaa kwenye chama takribani miaka miwili!!!MEMBE IMEKULA KWAKE!!!
Hiyo sheria ilipitishwa lini?!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ingekuwa huyo amefukuzwa upinzani na hasa Chadema humu vijana wa ccm wangechaniana nguo wakiisakama Chadema kama chama kisicho na demokrasia.

Sasa kwa kuwa ni huko kwao na kwa kuwa kafukuzwa kwa kutishia nafasi ya mfalme wao ktk azma yake ya kuendelea kuhodhi kiti chake, wanadai eti ni kwa kukiuka maadili.. maadili gani, hawasemi.!!! Ni unafiki ulioje.
 
Katika makosa makubwa ambayo CCM wamefanya ni kumfukuza Membe wakati huu.

Kiintelijensia alipaswa kufukuzwa mwishoni mwa mchakato wa uchaguzi mkuu 2020, Kwani ingewanyima wanachama wa CCM muda wa kutafakari na kujipanga upya.

Tofauti na Lowasa ambaye walimkatilia mbali katika hatua za mwisho kabisa. hata hivyo alikukuruka.

Kwa sasa Membe anawakati mzuri wa kufanya mikakati (kama anataka) na kujijenga upya kisiasa nje ya CCM.

Pili, Inampa nafasi wale wanachama machachali waliokuwa hawapendi uongozi wa sasa wa CCM taifa.

Tatu, Hatua hii imewapa usugu wale wanachama waliokuwa wakiogopa ogopa kusema yaliyo ya moyoni sasa watasema "hata membe amefukuzwa sembuse mimi"


Njia pekee iliyobaki kwa CCM kupona ni kuponya majeraha haraka na kufanya mchakato wa wagomea kwa haki, bila kumuonea Mtu.

Wale watakaofanyiwa figisu mara moja watageuka kuwa wapinzania katika Uchaguzi mkuu 2020.

Waliodhani upinzani umekufa wakae mkao wa kula.

Wapo wengi watamfuata.


Time will tell


Kwa njia yeyote, Ebu Twendeni na Membe au Lissu 2020!
 
Membe njoo chadema ugombee urais,tutakusafisha ufisadi wako wote wa mabilioni ya Libya.

Chama chetu hakibagui mtu uwe mwizi ,mchawi na fisadi sisi hatutajali ili mradi tu unatuletea wana chama wa kutosha na ruzuku yetu inaongezeka..

Nakushauri ukimbilie chadema kwa sababu chama chetu kina uzoefu wa kubadili gia angani na kupokea na kusafisha mafisadi tangu mwaka 2015.

Kabla hujachelewa Membe umeguswa ,sasa nuka ukielekea chadema na sisi tutakupokea kwa kishindo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom