Kufukuzwa Membe CCM: Hakika siasa ni Mchezo kama ilivyo Karata na Draft

Kufukuzwa Membe CCM: Hakika siasa ni Mchezo kama ilivyo Karata na Draft

Hata kama membe aende chama cha upinzani!hatoruhusiwa tume ya uchaguzi kugombea uraisi!sabb sheria mpya ya vyama vya siasa inamtaka mgombea kukaa kwenye chama takribani miaka miwili!!!MEMBE IMEKULA KWAKE!!!
ndo mmekazia hapo SWAIN nyie mffiiieeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeewwwww.. mtabana lkn mwisho mtainama tu
 
Hata kama membe aende chama cha upinzani!hatoruhusiwa tume ya uchaguzi kugombea uraisi!sabb sheria mpya ya vyama vya siasa inamtaka mgombea kukaa kwenye chama takribani miaka miwili!!!MEMBE IMEKULA KWAKE!!!
Sheria kandamizi

Jr[emoji769]
 
Katika makosa makubwa ambayo CCM wamefanya ni kumfukuza Membe wakati huu.

Kiintelijensia alipaswa kufukuzwa mwishoni mwa mchakato wa uchaguzi mkuu 2020, Kwani ingewanyima wanachama wa CCM muda wa kutafakari na kujipanga upya.

Tofauti na Lowasa ambaye walimkatilia mbali katika hatua za mwisho kabisa. hata hivyo alikukuruka.

Kwa sasa Membe anawakati mzuri wa kufanya mikakati (kama anataka) na kujijenga upya kisiasa nje ya CCM.

Pili, Inampa nafasi wale wanachama machachali waliokuwa hawapendi uongozi wa sasa wa CCM taifa.

Tatu, Hatua hii imewapa usugu wale wanachama waliokuwa wakiogopa ogopa kusema yaliyo ya moyoni sasa watasema "hata membe amefukuzwa sembuse mimi"

Njia pekee iliyobaki kwa CCM kupona ni kuponya majeraha haraka na kufanya mchakato wa wagomea kwa haki, bila kumuonea Mtu.

Wale watakaofanyiwa figisu mara moja watageuka kuwa wapinzania katika Uchaguzi mkuu 2020.

Waliodhani upinzani umekufa wakae mkao wa kula.

Wapo wengi watamfuata.

Time will tell

Kwa njia yeyote, Ebu Twendeni na Membe au Lissu 2020!
ni mkakati wa FISIEM kumfukuza MEMBE ni mpango ulioandaliwa wakiwa wanajiaminisha kuwa atapokewa ACT kuimarisha chama na kujaza wafuasi ili CHADEMA isahaulike sio kuishiwa mana inaonyesha FISIEM kwa CDM WAMEKWAMA VIBAYA SANA. propaganda zao kuiua CDM imefeli ndo wamekuja na mpango huu japo angalao wafanikiwe kuisahaulisha CDM kwa wananchi wa Tanzania.
 
Kwa nini wasingemuacha achukue fomu halafu wamfanyie kama machadema yalivyomfanyia Sumaye
 
Hata kama membe aende chama cha upinzani!hatoruhusiwa tume ya uchaguzi kugombea uraisi!sabb sheria mpya ya vyama vya siasa inamtaka mgombea kukaa kwenye chama takribani miaka miwili!!!MEMBE IMEKULA KWAKE!!!
Kwani hiyo sheria ya mwaka gani? Yani mtu akae for 2 Yrs? Vipi je kwa mbunge ni mda gani wa kukaa benchi?
 
Kashatoa tamko huko kasema tusubiri atatoa tamko rasmi vita ndio inaanza rasmi
Ataishia kutoa matamko na kushangiliwa na wachache kwenye mitandao lakini hana nguvu yoyote. Nilishasema hakuna aliyewahi kuitikisa ccm kama Mrema na wakati huo mitandao ya kijamii haikuwepo halafu rais alikua mzee Ruksa. Huyu anajidanganya
 
Wanasahau kuwa wapenzi na wana cdm wanazidi kuongezeka kila kukicha na tayari tushagundua mbinu zao chafu dhidi ya cdm!
ni mkakati wa FISIEM kumfukuza MEMBE ni mpango ulioandaliwa wakiwa wanajiaminisha kuwa atapokewa ACT kuimarisha chama na kujaza wafuasi ili CHADEMA isahaulike sio kuishiwa mana inaonyesha FISIEM kwa CDM WAMEKWAMA VIBAYA SANA. propaganda zao kuiua CDM imefeli ndo wamekuja na mpango huu japo angalao wafanikiwe kuisahaulisha CDM kwa wananchi wa Tanzania.

In God we Trust
 
Wenzako wenye akili sasa hivi wapo muhimbili pressure zimewapanda, wewe kisa Membe kufukuzwa ndani ya ccm lkn wewe chumia tumbo unaishia kumbwela mbwela tu hapo lumumba
Ataishia kutoa matamko na kushangiliwa na wachache kwenye mitandao lakini hana nguvu yoyote. Nilishasema hakuna aliyewahi kuitikisa ccm kama Mrema na wakati huo mitandao ya kijamii haikuwepo halafu rais alikua mzee Ruksa. Huyu anajidanganya

In God we Trust
 
Maccm hawajiamini kabisa kabisa, wakati wanajitapa wanapendwa
Mmmmmmm huwatakii mema wenzio yani wangemuacha hadi achukue fomu? Je akipita dirishani akaingia ndani kosa la nani?

In God we Trust
 
Wenzako wenye akili sasa hivi wapo muhimbili pressure zimewapanda, wewe kisa Membe kufukuzwa ndani ya ccm lkn wewe chumia tumbo unaishia kumbwela mbwela tu hapo lumumba

In God we Trust
Kwa bahati mbaya sana wenzenu uchaguzi wetu tulifanya desemba 2019 na chama chetu kilishindwa lakini tumekubali matokeo. Mimi naandika kama mpenda nchi yangu niliyozaliwa. Usidhani kila anayetoa maoni ni ccm ama cdm.. waziri wangu mkuu anaitwa BOJO na si Majaliwa.
 
MBINU HIYO sasahv anaingia ACT wazalendo hadi tunaelekea Kwenye uchaguzi mkuu watakuwa wanasikika ZZK na MEMBE na sio TL na Mbowe na chadema yao halafu baasda ya uchaguzi anarudi ccm kuunga mkono juhudi lengo lao Kuiua chadema na kuinyanyua ACT kuwa chama kikuu cha upinzani,ndiomaana zzk katengenezewa kashfa za kumpa umaarufu tu kuelekea uchaguzi
Mku sema kwa siasa za Tz hazitabiliki. Ngoja baada ya 2020 ndo utatwambia kama CDM ndo tishio au ACT ya Zitto?
 
Hayo ni mawazo yako kwa kutomjua membe alivyofanya na anavyobehave
Wanabodi Salaam.

Ikiwa taarifa za kufukuzwa uanachama wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu. Bernard Camilius Membe zikiwa bado zinatikisa mimbari ya siasa Tanzania, nimejikuta ninakumbuka matukio machache kabla ya uchaguzi mkuu uliopita mwaka 2015.

Ikumbukwe wakati ule mgombea aliekuwa anapewa nafasi ya kupeperusha bendera ya CCM kwenye uchaguzi mkuu alikuwa ni Ndg. Edward Lowassa, japo baadae aliikosa ile nafasi ikaangukia kwa Rais John Magufuli.

Hata hivyo wachambuzi wa mambo walibainisha kwamba Ndg. Membe ndie alikuwa chaguo la Rais mstaafu Kikwete, lakini kutokana na joto lililokuwepo ndani ya mkutano mkuu wakati ule baada ya jina la Lowassa kukatwa ikabidi ampitishe Rais Magufuli kuwa mgombea wa CCM ili kutuliza hali ya mambo.

Hii ilisababisha Ndg. Lowassa aondoke CCM (sio kwa kufukuzwa) na kuelekea upinzani CHADEMA ambapo aligombea urais japo hakushinda. Membe kwa upande wake aliendelea kuwa mwanachama wa CCM, mpaka leo alivyofukuzwa uanachama.

Tukikumbuka matukio machache yaliyotokea miezi michache iliyopita ambapo kwanza Ndg. Lowassa alirejea CCM, akiongozana na rafiki yake Ndg. Rostam Aziz, ambao kwa nyakati tofauti wote waliondoka CCM chini ya uenyekiti wa Rais Mstaafu Kikwete, sasa hao wote wamerejea CCM na kuongeza nguvu upande wa Rais Magufuli, halafu yule aliekuwa kipenzi cha Mwenyekiti aliepita (Kikwete) amefukuzwa uanachama wake, hivyo kumuondoa kabisa kwenye system kwasababu alionekana threat kwa Rais Magufuli.

Hii inaonesha siasa ni mchezo kama ilivyo michezo mingine karata (last card), na draft, siku zote wachezaji wa hiyo michezo huficha karata zao au kete kumvizia mpinzani wao wampe pigo la kushtukiza waumalize mchezo.

Hili linaweza kuthibitishwa kutokana na kelele zilizozuka siku za karibuni kwamba Ndg. Membe anaweza kuomba nafasi ndani ya CCM aweze kupitishwa kugombea nafasi ya urais ambayo imezoeleka Rais aliepo madarakani hupewa nafasi ya kumalizia muhula wa pili wa utawala wake, hii inaweza kuwa ndio sababu ya Membe leo kufukuzwa uanachama wake ndani ya CCM, na sio sababu za kinidhamu kama zilivyoainishwa na Pole Pole ambazo hazionekani kuwa na direct impact kwa Magufuli ku-seek his second term.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom