Kufukuzwa Membe CCM: Hakika siasa ni Mchezo kama ilivyo Karata na Draft

Kufukuzwa Membe CCM: Hakika siasa ni Mchezo kama ilivyo Karata na Draft

Ss km sheria inasema hivyo vp kw wagombea waliotoka vyama vingine na kujiunga ccm hy sheria haiwahusu wao au? Eg Mh.Waitara, Mh Mtolea, Mh. Gekul,.......
Hata kama membe aende chama cha upinzani!hatoruhusiwa tume ya uchaguzi kugombea uraisi!sabb sheria mpya ya vyama vya siasa inamtaka mgombea kukaa kwenye chama takribani miaka miwili!!!MEMBE IMEKULA KWAKE!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Membe akihamia ACT tu wale jamaa waanze kutundika mahema kuashiria msiba.

Na vita yao itakuwa dhidi ya ACT na Zitto na si CCM tena ama wote!

Hii hatua imechukuliwa mapema siyo kwa bahati mbaya!

Kilichomkuta Kachero katika video!😁
 

Attachments

  • 84438045_134566504335650_209091646500724875_n.mp4
    2.2 MB
Inabaki kuwa ni mtazamo.wako tu,huyu kaisha ,utakumbuka maneno yangu siku zijazo,ccm imejipanga haswa,na huwa hawakosei
Katika makosa makubwa ambayo CCM wamefanya ni kumfukuza Membe wakati huu.

Kiintelijensia alipaswa kufukuzwa mwishoni mwa mchakato wa uchaguzi mkuu 2020, Kwani ingewanyima wanachama wa CCM muda wa kutafakari na kujipanga upya.

Tofauti na Lowasa ambaye walimkatilia mbali katika hatua za mwisho kabisa. hata hivyo alikukuruka.

Kwa sasa Membe anawakati mzuri wa kufanya mikakati (kama anataka) na kujijenga upya kisiasa nje ya CCM.

Pili, Inampa nafasi wale wanachama machachali waliokuwa hawapendi uongozi wa sasa wa CCM taifa.

Tatu, Hatua hii imewapa usugu wale wanachama waliokuwa wakiogopa ogopa kusema yaliyo ya moyoni sasa watasema "hata membe amefukuzwa sembuse mimi"


Njia pekee iliyobaki kwa CCM kupona ni kuponya majeraha haraka na kufanya mchakato wa wagomea kwa haki, bila kumuonea Mtu.

Wale watakaofanyiwa figisu mara moja watageuka kuwa wapinzania katika Uchaguzi mkuu 2020.

Waliodhani upinzani umekufa wakae mkao wa kula.

Wapo wengi watamfuata.


Time will tell


Kwa njia yeyote, Ebu Twendeni na Membe au Lissu 2020!
 
Si mlisema hawezi kufukuzwa kachero mbobezi?
ni mkakati wa FISIEM kumfukuza MEMBE ni mpango ulioandaliwa wakiwa wanajiaminisha kuwa atapokewa ACT kuimarisha chama na kujaza wafuasi ili CHADEMA isahaulike sio kuishiwa mana inaonyesha FISIEM kwa CDM WAMEKWAMA VIBAYA SANA. propaganda zao kuiua CDM imefeli ndo wamekuja na mpango huu japo angalao wafanikiwe kuisahaulisha CDM kwa wananchi wa Tanzania.
 
Hongera sana
Kwa bahati mbaya sana wenzenu uchaguzi wetu tulifanya desemba 2019 na chama chetu kilishindwa lakini tumekubali matokeo. Mimi naandika kama mpenda nchi yangu niliyozaliwa. Usidhani kila anayetoa maoni ni ccm ama cdm.. waziri wangu mkuu anaitwa BOJO na si Majaliwa.

In God we Trust
 
Kufukuzwa kwa Membe ni maamuzi ya magufuli siyo Wana CCM.
Hii ndio CCM niliyoifahamu yenye maamuzi yasiyomuangalia mtu usoni.

Haijalishi wewe ni maarufu kiasi gani unapokengeuka lazima hatua zichukuliwe dhidi yako.

Hii ndio CCM aliyotuachia Nyerere na Kawawa

Maendeleio hayana vyama!
 
huu ni mchezo and this can be a strategic move done by ccm. wapinzani wawe makin sana vinginevyo watajitia katika aibu nyingine ya miaka mi 5 na kuua kabisa dhana ya upinzani pamoja na kukatisha tamaa mioyo ya watanzania wanaosubir kwa ham mabadiliko ya kimfumo.
 
Hiyo kesi ilishatolewa hukumu lkn wakubwa hawataki kabisa kuisikia hiyo kitu, sijui wanaogopa kitu gani haswa
Membe afungue kesi ya kudai ugombea binafsi.

Kukosekana nafasi ya ugombea binafsi kunamnyima haki yake ya kikatiba ya kugombea uongozi.

Sent using Jamii Forums mobile app

In God we Trust
 
Kwani hapa nchini kuna chama kimoja tu cha upinzani? Mbona mnakonda sana kwa ajili ya cdm?
Membe akihamia ACT tu wale jamaa waanze kutundika mahema kuashiria msiba.

Na vita yao itakuwa dhidi ya ACT na Zitto na si CCM tena ama wote!

Hii hatua imechukuliwa mapema siyo kwa bahati mbaya!

In God we Trust
 
Membe njoo chadema ugombee urais,tutakusafisha ufisadi wako wote wa mabilioni ya Libya.

Chama chetu hakibagui mtu uwe mwizi ,mchawi na fisadi sisi hatutajali ili mradi tu unatuletea wana chama wa kutosha na ruzuku yetu inaongezeka..

Nakushauri ukimbilie chadema kwa sababu chama chetu kina uzoefu wa kubadili gia angani na kupokea na kusafisha mafisadi tangu mwaka 2015.

Kabla hujachelewa Membe umeguswa ,sasa nuka ukielekea chadema na sisi tutakupokea kwa kishindo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Cdm wagombea wanao tayari,pia wamejifunza kwa Lowasa aliwaangusha kwa kukubali matokeo haraka
 
Wanabodi Salaam.

Ikiwa taarifa za kufukuzwa uanachama wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu. Bernard Camilius Membe zikiwa bado zinatikisa mimbari ya siasa Tanzania, nimejikuta ninakumbuka matukio machache kabla ya uchaguzi mkuu uliopita mwaka 2015.

Ikumbukwe wakati ule mgombea aliekuwa anapewa nafasi ya kupeperusha bendera ya CCM kwenye uchaguzi mkuu alikuwa ni Ndg. Edward Lowassa, japo baadae aliikosa ile nafasi ikaangukia kwa Rais John Magufuli.

Hata hivyo wachambuzi wa mambo walibainisha kwamba Ndg. Membe ndie alikuwa chaguo la Rais mstaafu Kikwete, lakini kutokana na joto lililokuwepo ndani ya mkutano mkuu wakati ule baada ya jina la Lowassa kukatwa ikabidi ampitishe Rais Magufuli kuwa mgombea wa CCM ili kutuliza hali ya mambo.

Hii ilisababisha Ndg. Lowassa aondoke CCM (sio kwa kufukuzwa) na kuelekea upinzani CHADEMA ambapo aligombea urais japo hakushinda. Membe kwa upande wake aliendelea kuwa mwanachama wa CCM, mpaka leo alivyofukuzwa uanachama.

Tukikumbuka matukio machache yaliyotokea miezi michache iliyopita ambapo kwanza Ndg. Lowassa alirejea CCM, akiongozana na rafiki yake Ndg. Rostam Aziz, ambao kwa nyakati tofauti wote waliondoka CCM chini ya uenyekiti wa Rais Mstaafu Kikwete, sasa hao wote wamerejea CCM na kuongeza nguvu upande wa Rais Magufuli, halafu yule aliekuwa kipenzi cha Mwenyekiti aliepita (Kikwete) amefukuzwa uanachama wake, hivyo kumuondoa kabisa kwenye system kwasababu alionekana threat kwa Rais Magufuli.

Hii inaonesha siasa ni mchezo kama ilivyo michezo mingine karata (last card), na draft, siku zote wachezaji wa hiyo michezo huficha karata zao au kete kumvizia mpinzani wao wampe pigo la kushtukiza waumalize mchezo.

Hili linaweza kuthibitishwa kutokana na kelele zilizozuka siku za karibuni kwamba Ndg. Membe anaweza kuomba nafasi ndani ya CCM aweze kupitishwa kugombea nafasi ya urais ambayo imezoeleka Rais aliepo madarakani hupewa nafasi ya kumalizia muhula wa pili wa utawala wake, hii inaweza kuwa ndio sababu ya Membe leo kufukuzwa uanachama wake ndani ya CCM, na sio sababu za kinidhamu kama zilivyoainishwa na Pole Pole ambazo hazionekani kuwa na direct impact kwa Magufuli ku-seek his second term.

Sent using Jamii Forums mobile app
Chadema haipokei tena maccm inasafisha kutarudisha ccm we uoni chama kipo kwenye kujisafisha
 
Kile chama cha ujamaa akili anazo mmiliki wake na uruhusiwi kuwa na akili au maarufu zaidi ya mmiliki wa chama
 
Back
Top Bottom