Kufukuzwa Membe CCM: Hakika siasa ni Mchezo kama ilivyo Karata na Draft

Kufukuzwa Membe CCM: Hakika siasa ni Mchezo kama ilivyo Karata na Draft

Ushauri mzuri sana huo, tuone umwamba wake halisi kisiasa.
 
MBINU HIYO sasahv anaingia ACT wazalendo hadi tunaelekea Kwenye uchaguzi mkuu watakuwa wanasikika ZZK na MEMBE na sio TL na Mbowe na chadema yao halafu baasda ya uchaguzi anarudi ccm kuunga mkono juhudi lengo lao Kuiua chadema na kuinyanyua ACT kuwa chama kikuu cha upinzani,ndiomaana zzk katengenezewa kashfa za kumpa umaarufu tu kuelekea uchaguzi
Mkuu pia nimewaza hivyo, hizi mind game lengo kutokomeza Chadema na pia ni mbinu ya Membe kujisafishia njia 2025
 
Mkuu Kaka Mkubwa Wakudadavua, naunga mkono hoja yako, ila kufuatia kuwa ni kachero mbobezi, anajua akianzisha chama hakitasajiliwa!.

P
 
Wakudadavuwa,
Kama kweli CCM wanajiamini, waruhusu katiba mpya, ili tume ya uchaguzi na mahakama vile huru. Halafu wanaume waingie uwanjani (uchaguzi). CCM lazima itapukutika (au kupotea) itakuwa kama KANU ya Kenya. Ila kwa sasa haki wanayo, lakini yana mwisho. Hili nalo litapita.
 
Seif mwenye influence kubwa hajaanzisha chama chake itakuwa Membe?
 
Mkuu Kaka Mkubwa Wakudadavua, naunga mkono hoja yako, ila kufuatia kuwa ni kachero mbobezi, anajua akianzisha chama hakitasajiliwa!.

P
Membe kundi lake wengi ni wazee wastaafu hawa nia yeyote za kisiasa zaidi ya Biashara zao na amani zao.

Wenye moto wa kisiasa ambao unaishishia aende kwenye "saccos" au maigizo ya wazalendo.

Labda God Father awe na kiu ndio amsaidie. Sasa atakuwa ana cheka cheka na watu wa mtama au akimbilie nje ya nchi.

Lakini sio kule high street
 
Kunazisha Chama sio jumbo rahisi, Membe pia sio mtu anaejukikana Sana huku mitaani tunakoishi makabwela. Huku hana ushawishi. Astaafu siasa ama ajiunge na wenye ushawishi au asubiri kurudishwa CCM siku za mbele Kama ulivyo mkakati

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji40][emoji40]
IMG_20200228_193608.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nadhani angeachana na siasa utumishi aliotumika toka enzi hizo unamtoshea kujivunia mchango wake kwa taifa hili. Na watu wa taifa hili hatutamsahau kwa utumishi wake.

Kama chama alichokuwepo kimeshindwa kuitaimbua thamani yake na kumuhukumu hukumu isio lingana na kosa lake atulie tuu ili sheria ya ulimwengu ichukue nafasi yake yaani karma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kila mshale dhidi ya dubwana hili, JIJINJEMU, ni afya kwa future ya Tanzania!
ALUTA CONTINUA!
✌✌✌
 
Hii ndio dawa sasa.

Salamu ziwafikie wale wote wasiopenda changamoto kutoka aidha kwa watu, kikundi au jamii tofauti na wao, pia wanaojiona wao ni bora kuliko wengine kuwa hiyo bahari mnayoiringia ambayo mpo ndani yake mkumbuke siku mkitoka nje mnakufa.

Nawakumbusha tu bahari inatabia ya kujisafisha yenyewe. Utaiwekea ukingo, utaiboresha pwani yake, utaipandia maua ila ikiwa inajisafisha hayo yote uliyoyafanya ni kazi bure.

Bahari inapenda usafi bwana maana uchafu, mizoga na kila aina ya taka utupwa nje.

By

Mtoto wa mjini
 
Unajua watu wengi hawajui kisa cha bahari kujisafisha na hawashtuki watu wakifa ndani ya bahari wapo ambao hawaonekani kabisa na wengine kwa huruma tu ya bahari upelekwa ufukweni kama taka bahari.

Vijana wa leo wakaka & wadada mpende sana elimu ya kukusaidia kimwili na kiroho maana hii dunia ili uishi unatakiwa ukidharau kwanza kifo yaani usikione chenye maana kabisa kwako ndipo utaiponya nafsi yako.
 
Ni nani aliye na nafuu kati ya wana CCM au Wapinzani, au wote hali zao ziko sawa isipokuwa wale tu wanaojisalimisha kwa mtu mmoja?

Tumeona walionunuliwa tokea upinzani wakiula, kwa teuzi mbalimbali au kuahidiwa mambo kadhaa.

Sasa tunawaona walioko huko huko CCM, lakini wakawa na mawazo yasiyokuwa kwenye mstari wa mwenyekiti wao nao wakionjeshwa shubiri.

Kwa hiyo, ni sahihi kwamba haijalishi wewe upo upande gani, CCM au Upinzani; kama mawazo yako ni nje na yale ya Mwenyekiti huwezi 'survive'.

Tena nadiriki kusema kwamba heri ya wale waliopo upinzani na wamekataa kuuza utu wao, kwani bado wanayo nafasi ya kueleza mambo wasiyoafikiana nayo hata kama hayampendezi mwenyekiti.
Ukiwa ndani ya CCM hata hili dogo tu la kutetea mawazo yako ambayo pengine hayampendezi mwenyekiti hutakiwi kuyawasilisha.

Kwa hiyo ieleweke wazi kwamba wote walioko ndani ya CCM wapo huko kwa njia za 'ku'survive'. Ni lazima ukubali kila kitu anachotaka mwenyekiti. Wote wapo huko kumfurahisha mwenyekiti ili mambo yao yafane, na sio kwa sababu wanakipenda chama chao na sera zake.
 
Hata wapinzani waliokimbilia CCM wajue wamekwenda kufunga midomo yao, huko ni kuimba kwa kusifia tu, hakuna kupinga, hawakujua walioko CCM wanavyovumilia ngoja nao waonjeshwe shubiri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata kama membe aende chama cha upinzani!hatoruhusiwa tume ya uchaguzi kugombea uraisi!sabb sheria mpya ya vyama vya siasa inamtaka mgombea kukaa kwenye chama takribani miaka miwili!!!MEMBE IMEKULA KWAKE!!!
Hiyo haijawa sheria. Na inapingana na Katiba ya JMT khs haki ya kuchagua na kuchaguliwa. Ila kwa mabavu wataipitisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo, ni sahihi kwamba haijalishi wewe upo upande gani, CCM au Upinzani; kama mawazo yako ni nje na yale ya Mwenyekiti huwezi 'survive'.
Hii ndiyo grobal standard operating procedure. Hata nyerere alifanya hivyo
 
Back
Top Bottom