Naaaam, wananchi wenzangu!
Nimefikiria kwa kina na kusoma comment za wananchi wenzangu dhidi ya maamuzi ya mwenyekiti wa CCM, kumfuta uanachama Mh. Bernard Membe.
Nimesoma jinsi watu wengi wanavyo comment kwa mihemuko ya kumhurumia Membe.
""JAMANI CCM WANA MBINU NYINGI MNO ""
Hili ni lazima wananchi wenzangu ambao ndiyo wapiga kura, tuamke na kuelimisha wenzetu hasa huko mitaani na huko vijijini.
Kila mwaka wa uchaguzi, CCM hujipanga vyema kupitia makada wake, mbinu kadhaa wa kadhaa, safi na chafu, za siri na za kuelimisha ilimradi kushinda uchaguzi.
Chambo ya Membe haina tofauti na ile ya Lowasa.
Kwa mtazamo wetu sisi wapiga kura, ni kama CCM na Mwenyekiti wake, wamehitalifiana vibaya sana na Membe, hilo si kweli hata kidogo, huyo wamemtuma ili kudhohofisha upinzani na kutugawa wapiga kura.
Na kwa mpango huu Magufuli atashinda kwa urahisi sana uchaguzi huu ujao.
Wanachofanya CCM, ni kumuandaa kada mmoja wenye nguvu, kabla ya uchaguzi aonekane mwenye ugomvi na serikali au chama, halafu atangaze kuhamia upinzani.
Membe atahamia ACT WAZALENDO, hata Zitto anavyoonekana mpinzani mkubwa wa serikali na CCM, yawezekana kabisa katika kipindi hiki lao ni moja, ila wanao umia ni wananchi/wapiga kura.
Naishia hapa, fungue macho, sumaye, lowassa ni mifano tu, iliyotumika kutugawa na kupunguza makali ya kura zetu bila sisi kujua na hivi sasa wanakula pension zao.
Nawakilisha, kukubaliana kutokukubaliana ni BUSARA muhimu .
Sent using
Jamii Forums mobile app