Kufukuzwa Membe CCM: Hakika siasa ni Mchezo kama ilivyo Karata na Draft

Kufukuzwa Membe CCM: Hakika siasa ni Mchezo kama ilivyo Karata na Draft

1. Viwanda wameviteketeza vyote, sasa hivi wainaimba unafiki kila kona.

2. Wamenunua madege kibabe watoto wetu hawana popote kufanya Elimu kwa vitendo

3. Wamesababisha kibabe wawekezaji wengi kuondoka, kiasi kwamba ajira zimetoweka

4. Wamedidimiza na kupoka madaraka kutoka maamuzi ya wananchi kupitia bunge, sasahivi sijuwi bunge kazi yake nini

5. Wamezigeuza mahakama kuhukumu kwa maelekezo kibabe kiasi kwamba wengine wanasota lupango kwa vijesenti kidogo tu 17million
Kangi, na majizi ya mkobozi bank wapo mtaani

Hakika MEMBE katoweshwa kibabe kwa faida ya mtu mmoja tu sio taifa. Ingelikuwa taifa tungesubiri uchaguzi ili kura ziseme nani anastahili kwa maamuzi ya watanzania.
 
Sote tumesikia na kusoma kufukuzwa kwa Bernard Membe kwenye Chama cha Mapinduzi CCM. Tusilojua ni mikakati iliyopo nyuma ya pazia kuhusu kufukuzwa huku.

Nikiwaza sana ninaona kuwa huu ni mkakati wa siri wa CCM yenyewe katika hatua za mwisho za kujaribu kuua upinzani nchini.

Mkakati huu huenda ulibuniwa na wanamikakati nguli wa TISS akiwepo Membe mwenyewe. Turejee kuwa ukiwa TISS hakuna kustaafu. Ukisaliti unauawa haraka sana kama msaliti yeyote kwenye majeshi.

Mkakati wenyewe upo hivi.

Hatua ya kwanza ilikuwa kwa Membe (aliyejitolea kukinywea kikombe ili kuikomboa CCM dhidi ya kifo cha milele) na baadhi ya wanaCCM kuonyesha kuegemea kusigana na jiwe.

Hatua ya pili ni Chama kuwapa maonyo na kisha kumfukuza mkubwa wa hao wanaharakati wa CCM.

Hatua zitakazofuata ni Membe kuanzisha harakati za kuuteka upinzani kwa kujichomeka kama mtu maarufu anayeweza kuchuana na jiwe. (Hii karata wapinzani wataikataa).

Hatua itakayofuata baada ya kukataliwa na wapinzani wa kweli ni yeye kutafuta chama kilichosajiliwa au kusajili chama chake kisha kuwavuta wanachama kadhaa hasa watakaochujwa na CCM kwenye ugombea 2020.

Baada ya hapo ni tume kumpitisha yeye kama mgonbea huku ikiwazuia wapinzani wa kweli kama CHADEMA nk. kwenye nafasi ya urais.

Mwishoni tutaambiwa wagombea pekee ni Membe na jiwe. Na jiwe atajitapa kuwa uchaguzi utakuwa huru kabisa. Membe ataendelea kuwashawishi wapinzani waungane naye kupambana na jiwe.

Mwisho wa sinema Membe 1% Jiwe 99%. Series inaishia hapo. TISS ni balaa sana. Sisi wanyonge tuendelee kupata Tusker za baridi. Siasa tuiachie TISS.
 
Ni kama utani.

Kufukuzwa CCM mwanachama mwandamizi, mkongwe na mwenye ushawishi kama Membe ilitakiwa ilete mshtuko mkubwa mno.

Sio mzaha huu? Membe afutwe uanachama CCM halafu Mzee Mkapa, Mwinyi na Kikwete wote wapige kimya kama hakuna kilichotokea! Wazee wengine kama kina Warioba na wafia chama wote wapo kimya. Tulioshtuka na kupiga kelele ni sisi watu wa kawaida tu. Ajabu!

Nilitarajia ungeibuka mzozo mkubwa kuanzia ndani ya CCM kwenyewe lakini wapi. Ina maana wote wamekubaliana na maamuzi ya Kamati Kuu? Kweli?

Inashangaza na kufikirisha. Membe kwa nyadhifa alizowahi kushika na utiifu wake wa muda mrefu kwa chama na serikali zake, sio wa kufutwa kimya kimya hivi kama mwanachama tu wa kawaida.

Ni wanaCCM wanaogopa au wanajua ni mchezo wa uchaguzi mkuu kama ilivyofanyika kwa Lowassa, Sumaye na majemedari wengine mwaka 2015?

Muda utasema.
 
Hii ndo CCM banaa na si CDM,vyama vinavyomilikiwa na watu/familia/ukoo/kabila Kama kina zito na mbowe.
CCM ni chama Cha wananchi wa nchi hii,ukizingua Basi hawatokufumbia macho kwa ustawi wa chama na vizazi vijavyo wapate kujifunza zaidi
 
Interest,
Wanasubiri makongamano wakasemee huko then tukinukuu walichosema wanarudi kusema tumewanukuu vibaya na mambo yanaendelea. Magufuli aliwahi kujitapa kuwa "Power is power" Pia aliwahi kuwaonya kuwa yeye ndiye Rais!
 
Dikteta Bashiru Ally
Bashiru moja Kati ya makatibu wachache kutokea wasio muonea haya mtu Wala kuonea wengine.Watu wametafuna fedha za umma/chama na bado wanataka kuendeleza umwinyi!CCM hyo ya kulambana miguu imeishia 2015.
 
1. Sitarajii cdm watampokea membe

2. Act wanaweza lakini sidhani pia

3. Uwezekano kuanzisha chama chake 95%

Sitarajii tishio lolote kwa wapinzani lakini ndani ya ccm kunatisha, tujikumbushe historia ya akina kolimba, Kombe, sokoine, malima, jumbe nk
 
Shushushu adukuliwe halafu maongezi yake yawekwe hadharani na huyo huyo JIWE!

Lazima yawekwe hadharani ili kuwa hadaa watu kwamba ni mkosaji na ipatikane sababu ya kumfukuza.hii kitu imepangwa Mzee jaribu kufikiria asinge dukuliwa ni sababu ipi ingemfukuzisha chamani?
 
Lazima yawekwe hadharani ili kuwa hadaa watu kwamba ni mkosaji na ipatikane sababu ya kumfukuza.hii kitu imepangwa Mzee jaribu kufikiria asinge dukuliwa ni sababu ipi ingemfukuzisha chamani?
Hii nchi ukiwa na upeo unawaburuza kama gari bovu na hawashtuki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku zote huwa namuona captain Lowassa kama mwanasiasa aliyejipatia mafanikio makubwa ndani na nje ya CCM.

Lakini mpiganaji huyu wa vita vya Kagera captain Lowassa siasa za upinzani zilimshinda baada ya kuwaeleza wazi Chadema kuwa kushindwa kwao kuingia Ikulu mwaka 2015 kutaifanya CCM itawale kwa miaka mingine 50.

Ndiposa najiuliza mh Membe anaweza kwenda kupindua meza huko upinzani na hatimaye 2025 akatinga Ikulu?

Maendeleio hayana vyama!
 
Ukitaka kukipanda kichwani Chama Cha Mapinduzi lazima wakufyeke. Hawa watu bado wanatawala sababu ya kuheshimu yule waliompa dhamana kuongoza chama na serikali.

Mnafikiri marais wastaafu tangu enzi hizo walishindwa kuanzisha timbwili? Membe alidekezwa utawala iliopita akajisahau. Rostam aliwahi kusema hawezi kupambana na mwenye dola! Membe anajua hili lakini amejisahau! Hope atajirudi ajipange kimkakati.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Membe achukuliwe na nani.... abakie hukohuko ccm

Yaliyotupata kwa
1. Lowasa
2. Sumaye
3. Mwita
4. Katambi
Na wengine wengi inatosha

Upinzani kuna vijana wengi, wana uwezo mzuri kiakili na weledi, wanatutosha.
 
Back
Top Bottom