Ni uamuzi makini sana kusafisha nyumba mapema, kwani hawa mngewaacha mwishoni kabisa karibia na uchaguzi wangewaletea yale ya mwaka 2015, na matokeo yake wanachama wangegawanyika na kupunguza ushindi wa CCM halikadhalika CCM kujipa tabu kuisaka dola.
Ndio maana wapinzani wamelaani sana Kinana, hasa Membe kutolewa mapema, kwani turufu yao ilikua ajikatae uchaguzi ukikaribia.
Sasa Membe kabla hajafanya hivyo amewahiwa. Kiukweli CCM muendelee kuhakikisha masalia yote ya 2015 ya makundi yanakwisha au kumalizwa nguvu kabisa.
Nidhamu ndani ya chama kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka huu ni muhimu sana.
Mwisho kabisa CCM hongereni kwa kuonyesha kwamba ni taasisi imara haiyumbishwi na majina ya wale wanaojifanya bila wao CCM haipo.