Mwanzi1
JF-Expert Member
- Sep 19, 2016
- 6,000
- 4,589
Wazungu wanapenda kusema "Political Chess Game". Maana katika mchezo wa chess, kete ikisogegezwa inaweza kukuvusha au kukuangusha. CCM imemwaga maji, mara nyingi maji yakimwagika lazima yatafute mkondo.
Ni wazi kuwa Lissu alishaweka hadharani nia ya kugombea urais, na Zitto naye hakuchelewa akaweka nia yake pia wazi. Kama Membe akienda kulia hawezi kumkosa Lissu anamsubiri, akienda kushoto yupo Zitto.
Kijana Zitto alishasema, kadi namba 2 ameiweka kabatini kwa ajili ya mtu mzito kutoka CCM. Kauli hiyo ya Zitto ya kumsubiri nguli wa CCM, inawezakana imeshabadilika kutokana dynamics ya mchezo wa kisiasa unaoendelea hivi sasa.
Wakati huo huo wale waliobanwa Zanzibar kina Maalim Seif na kundi lake dogo watampa mkono? Nyalandu je, yeye anaingia kundi gani? Hapa bila VAR [V] uamuzi utakuwa mgumu sana.