Kufundisha Watu Kura ya Ndiyo (Serikali), Hapana (Maaskofu,UKAWA) ni Sahihi?

Wewe ni mpuuzi namba moja humu cjawah kuona, akili zako hazina tofauti na hizo katuni unazoweka, kwa maana kama ungekuwa na akili timamu ungeweka hoja, sasa wewe unaweka katuni ambazo hazina mashiko na hazina connection zaidi ya kutueleza jinsi akili yako ilivyo.
 
mbona hao wanasiasa walisusa vikao vya kuiandaa
Ache ujinga katiba ni ya wote hivyo mchungaji, kafil, shahe pamoja mwenasiasa wanatakiwa kuwa na nguvu sawa wakati wa kuiandaa.
 
..maajabu haya...wao wanasema wakati ikifika pigia kura ya ndiyo mimi nikisema piga kura ya hapana kosa unalo..WANAFIKI

Ni wakati wako kusema hivyo la matokeo ndio yatawaeleza tukwani tatizo liko wapi?
 
hawa viongzi wahache wanaotaka kutupeleka njia isiyofaa kwa maslahi yao zaidi,chonde viongozi wa dini siuingilie kwenye mambo ya msingi kma hilo a kitiba inayopendekezw!katik kupiga kura wakati ukifika
 

pointless
 
..maajabu haya...wao wanasema wakati ikifika pigia kura ya ndiyo mimi nikisema piga kura ya hapana kosa unalo..WANAFIKI

Wewe hulioni kosa hapo ina maana huoni hilo neno uliloliandika kwa herufi kubwa hulioni wewe?lazime upingwe kwa mitusi yako afu wewe unfikiri nini hapa!
 

Wakristo wanajua sana kutokana na maandiko kwamba Pilato alimhukumu Yesu kufa msalabani si kwa sababu aliona kosa bali aliogopa macho ya Mayahudi na kubembeleza urafiki na Kaisari. Tuangalie kwa makini hapa, kati ya viongozi wa dini wanaowahamasisha waumini waipigie kura ya hapana katiba, na wale wanaopingana na hao, ni kundi lipi kati yao linaogopa macho ya Mayahudi. Lazima tuongozwe na ukweli, kura hupigwa tu pale ambapo kuna ndiyo na hapana. Kama serikali nzima pamoja na chama tawala wote hao kwa nguvu kabisa wanahamasisha wananchi kupiga kura ya ndiyo, taasisi nyingine ikija na wazo tofauti na hilo katika nchi inayoamini utawala wa sheria na demokrasia, kosa liko wapi. Hapa lazima tuulizane, kati ya wale wanaohamasisha watu waipigie kura ya hapana katiba na wale wanaoiunga mkono serikali inayohamasisha watu waipigie katiba kura ya ndiyo ni nani Pilato anayeogopa macho ya Mayahudi. Kiongozi anajitokeza na kusema kwa uhakika kwamba tusiwafanye waamini wetu wajinga na kuwachagulia cha kusema wakati kiongozi huyo huyo alinyamaza kimya serikali ilipowahamasisha watu wapige kura ya ndiyo kwa nini tusimfananishe na Pilato aliyeogopa macho ya Mayahudi na kubembeleza urafiki na Kaisari.
 
Viongozi wa dini jukumu lao ni kutulea kiroho,huku kwenye siasa naona mmeingia sehemu si yenu na hasa hii hatua mliyofikia ya kutushawishi tukapige kura ya hapana kwenye kura ya maoni kuhusu katiba mpya,nashangaa sana hasa viongozi wangu wa katoliki badala ya kupanga mipango ya kuwainua waumini kiroho na kuondoa mambo yasiyofaA ndani ya kanisa,sasa mmegeuka kuwa wanasiasa au mawakala wa siasa zisizofaa zenye chuki na mgawanyiko,hatutaki utaratibu huu wa kutuandikia waraka na kutulazimisha tuufuate,hatutaki ,tunao utashi na tutaamua wenyewe siku ikifika
 
viongozi wa dini jukumu lao ni kutulea kiroho,huku kwenye siasa naona mmeingia sehemu si yenu
haiwezekani kupata malezi mazuri ya kiroho tu wakati huohuo mwili unadhulumiwa au upo katika mateso.siasa haikwepeki kwa maisha ya sasa.
 
haiwezekani kupata malezi mazuri ya kiroho tu wakati huohuo mwili unadhulumiwa au upo katika mateso.siasa haikwepeki kwa maisha ya sasa.

Biblia imewashinda sahiv wanakimbilia siasa jambo ambalo ni hatari kwani linaleta mvurugano.
 
Viongozi wa dini wafuate wito wao waachane na siasa na wajikite kutusaidia waumini wao badala ya kuanza shughuli za siasa ndani ya makanisa yao na misikiti,tuacheni waamini wenu tuacheni tutaamua wenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…