Ikengya
JF-Expert Member
- Oct 18, 2013
- 614
- 178
Unayejiita Not_Yet_Uhuru, Maneno meeengi hayana hata hulka ya kuwa na busara. Unaposema unapiga kura unategemea nini? Kura maana yake kuna pande mbili. Hata hili hulioni? Ubovu wa Katiba Inayopendekezwa umetoka wapi, kama kweli wewe ni mzalendo wa dhati soma kuanzia utangulizi wake uone kama wananchi hawahusiki. Sema ukweli na ukweli utakuweka huru ..KWA KUWA, sisi wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumeamua rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi yetu jamii inayoheshimu na kuzingatia misingi ya utu na udugu, uhuru, kujitegemea, haki, usawa, amani na utulivu, umoja na mshikamano katika nyanja zote za maisha yetu Huo ni utangulizi tu, pata muda uisome vizuri ujionee na hatimaye muda ukifika usiwe kikwazo kwa Wananchi.
Hayo yote ukinyimwa huna pa kuyadai dadangu. Hivyo ni meneno kama yakwenye kanga hayaaksi uhalisia. Haki isiyo daiwa mahakamani ni ya nini?