Dragunov Sniper
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 2,795
- 9
....kwenye rasimu ya chenge hakuna uzalendo hata kidogo....Nina nakala (hardcopy) ya Rasimu ya Wananchi(Warioba)...Nimeisoma mwanzo mpaka mwisho....tangu mambo ya msingi niliyotegemea Kupitishwa yalipoondolewa sikuona sababu ya kupoteza muda kuisoma ya chenge....Nilichukua maamuzi hayo baada ya kuona muhtasari wa yaliyomo na yaliyoondolewa....kwa kifupi rasimu ya Chenge haina Tofauti na katiba ya sasa(kama ipo ni ndogo na insignificant)...na ni kheri kuchukua muda zaidi ili kupata katiba stahiki kwa miaka hamsini ijayo
Hivi unajua kuwa rasimu ni maoni? Bunge Maalumu la Katiba limefanya kazi ya kukamilisha Katiba Inayopendekezwa baada ya kuhakikisha wamechambua na kutoka na kitu bora zaidi baada ya kubakisha asilimia 75 yaliyokuwa kwenye Rasimu ya Tume ya Katiba na kuboresha mengine asilimia 25. Tuwe wa kweli hivi huoni kuwa karibu maoni menginyaliyokuwepo kwenye Rasimu ya Tume yamewekwa? Usitamani usichokiona, tumia haki yako kujiandikisha na kisha upige kura ili kutimiza haki yako ya kikatiba.