Kufunga 'PM' ni ishara ya kuwa mchoyo na mbinafsi

Kufunga 'PM' ni ishara ya kuwa mchoyo na mbinafsi

🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣Umenichekesha Aisee!Ila kweli halafu uwe umetoka kupiga zako kibarua juani umejichokea macho mekundu maskini ya Mungu tunajua Ni mvuta bangi na mkora mzoefu
Umeona Mungu hakupi vyote ila ànaweza akakunyima vyote
 
Ngoja tu wafunge, wanatusaidia sana, wangefunga wote huenda tungeokoka kwa mengi 😁😁

PM kuwa wazi ni temptation kwa Me walio wengi, ila ukijaribu na kuona PM ina kufuli ni "kuvuja kwa pakacha..."!
Pm huko kuna mengi 😅
Bora wafunge tu maana ni vilio
 

Kufunga 'pm' ni dalili ya uchoyo; ni sawa na kupika chakula kizuri na kitamu, na kujifungia ndani na makufuli makubwa, ili mgeni yeyote atakayependa kuja kukutembelea, asiweze kuingia na kula chakula hicho ulichokiandaa; kwa namna nyingine tunasema huo ni uchoyo.

Pia inazuia mgeni kuja kukuletea habari njema; kwa sababu ataishia nje ya mlango, na hatoweza kuja kukuhabarisha habari njema zenye tija.

Ni sawa pia na kujenga nyumba na kuzungushiwa na ukuta mrefu; ili wapitao bara barani wasiweze kuingia ndani; na mara nyingi waliojifungia ndani, wanakuwa hawana furaha mpaka pale watakapo toka nje ya uzio na kujumuika na wapita njia n.k

Kwa ujumla, hiyo ni dalili ya uchoyo; fungueni 'pm'​
Hata kuweka milango kwenye nyumba zetu ni ubinafsi. Tujenge nyumba tusiweke milango
 
nimeingia jf mda huu nakutana na mkeka mrefu wa kutufokea sisi tuliofunga PM.

nasemaje, acha nionekane mbinafsi na mchoyo. liwake jua inyeshe mvua, PM sifungui. binafsi sihitaji ku establish network or friendship na mtu yoyote wa JF.

nimeridhika na network ya marafiki ambao nimefahamiananao linkedin, instagram na twitter.

jf tuishie kupiga story tu na kujadiliana masuala mbalimbali ya kijimii. kuchati PM is a BIG NO for me, ili iweje kwa mfano?, mwisho tuanze kuombana namba za simu....then what!.



.
 
Back
Top Bottom