Kufunga 'PM' ni ishara ya kuwa mchoyo na mbinafsi

Kufunga 'PM' ni ishara ya kuwa mchoyo na mbinafsi

Ngoja tu wafunge, wanatusaidia sana, wangefunga wote huenda tungeokoka kwa mengi 😁😁

PM kuwa wazi ni temptation kwa Me walio wengi, ila ukijaribu na kuona PM ina kufuli ni "kuvuja kwa pakacha..."!
 

Kufunga 'pm' ni dalili ya uchoyo; ni sawa na kupika chakula kizuri na kitamu, na kujifungia ndani na makufuli makubwa, ili mgeni yeyote atakayependa kuja kukutembelea, asiweze kuingia na kula chakula hicho ulichokiandaa; kwa namna nyingine tunasema huo ni uchoyo.

Pia inazuia mgeni kuja kukuletea habari njema; kwa sababu ataishia nje ya mlango, na hatoweza kuja kukuhabarisha habari njema zenye tija.

Ni sawa pia na kujenga nyumba na kuzungushiwa na ukuta mrefu; ili wapitao bara barani wasiweze kuingia ndani; na mara nyingi waliojifungia ndani, wanakuwa hawana furaha mpaka pale watakapo toka nje ya uzio na kujumuika na wapita njia n.k

Kwa ujumla, hiyo ni dalili ya uchoyo; fungueni 'pm'​
CC Bantu Lady
 
Pengine ni Bora hao kuliko sisi wenye sura personal na hela imetupiga teke.Ukimsalimia mtoto mzuri ghafla anashikilia pochi na simu yake vizuri akihisi huyu atakuwa kibaka
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣Umenichekesha Aisee!Ila kweli halafu uwe umetoka kupiga zako kibarua juani umejichokea macho mekundu maskini ya Mungu tunajua Ni mvuta bangi na mkora mzoefu
 
Back
Top Bottom