MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Nawasalimu katika jina la chama pendwa CCM.
Leo nimekuja kitofauti.
Leo ninatoa maoni yangu kuhusu mambo ya mapenzi na ndoa. Kabla sijaelezea nataka kila msomaji ajikumbushe ule msemo usemao "fuata maneno yangu sio matendo".
Leo nitaongelea kitendo cha madhehebu yetu hasa ya kikristo kufungisha ndoa watu ambao tayari walishazini. Namaanisha zile harusi ambazo tayari bibi harusi ni mjamzito.
Kabla sijaandika huu uzi ilibidi nisome kwanza biblia kujiridhisha kama kuna sehemu iliruhusiwa watu kupeana tamu kabla ya ndoa. Biblia nzima hakuna sehemu iliyoruhusu hilo jambo. Sikuishia hapo nikasoma katiba ya nchi sikuona.
Nikasoma pia rasimu ya Warioba sikuona. Nikasoma katiba na ilani ya chama cha Mapinduzi pia sikuona ikiruhusu. Hata kwenye katiba ya Chama Cha Mbowe hawajaruhusu uzinzi kabla ya ndoa.
Nimebaki najiuliza hawa viongozi wa dini kwanini wasikemee hili jambo na kuweka ugumu kwenye kufungisha ndoa za watu wa namna hii? Hawaoni wanachangia mmomonyoko wa maadili kwa kuhalalisha uzinzi kabla ya ndoa?
Biblia imesema wazi kwamba kuliko kuwaka tamaa bora mtu aoe. Ila haijasema ukafanye tu ngono kupunguza tamaa zako.
Ninawasihi viongozi wangu wa kikristo wajirekebishe pale walipokosea badala ya kuendelea kufumbia macho uzinzi kabla ya ndoa. Hata kama hizo ndoa zinanufaisha kanisa kiuchumi tuzikatae au tuweke utaratibu mgumu.
Imeshafikia sehemu vijana wakipendana lazima wakulane hapohapo. Hata hapa JF kuna uzi wa kula tunda kimasihara.