Kufungisha ndoa takatifu huku Bibi Harusi akiwa mjamzito ni kuhalalisha uzinzi

Kufungisha ndoa takatifu huku Bibi Harusi akiwa mjamzito ni kuhalalisha uzinzi

Kwa hali ya sasa haiepukiki hiyo,lazima ujue mapema lasivyo unaweza kuuziwa mbuzi kwenye gunia
 
Halafu ukute bibi harusi ana ujauzito wa miezi sita na bwana harusi ana kitambi! Muda wa pete wanafanana na b zinazotazamana!
 
Kwani kisheria ya kislam mimba inanza kuhesabika ni kiumbe yaani ni mtoto ikiwa na miezi mingapi...?
Halafu nenda ukasome historia ya Nabii Ibrahim (A.S) kisha uje kuniambia kama alimpa au hakumpa mirathi mtoto wake wa nje...?
Hiyo mimba ikiwa imepatikana nje ya ndoa au ndani ya ndoa?
 
Kuna couple zilikuwa zimepanga kufunga ndoa kwenye dhehebu la moravian

Kama kawaida ya wakristo maandalizi ya ndoa na pilikapilika za michango unakuta inachukua miezi kibao mpaka kufikia siku ya ndoa.

Ilikuwa mwezi wa tatu wameanza kutangaza ndoa yao itafungwa mwezi wa 9 ili kuwapa watu muda wa kujipanga waweze kuchangia.

Mwezi wa 9 unafika siku ya harusi pastor anashangaa kuona kibendi kwa bibi harusi. Pastor akawatolea nje akasema hii ndoa sifungishi maana tayari mshazini.

Wanandoa watarajiwa ikabidi waende Roman kule wakapokelewa na kuanzia hapo ndio wakawa rasmi waumini wa dhehebu hilo la Roma

Kisheria ndoa inatangazwa siku 21 huwezi ukatangazwa miezi mitatu. Pili kuna semina za wanandoa na mwenye leseni ya ndoa ndio anaewapa semina wana ndoa na ndie anaefungisha ndoa je siku zote hakuona huo ujauzito?. Yapo makanisa yapo so strict kwanye hilo utaambiwa nenda bomani ukafungiwe ndoa
 
Back
Top Bottom