Kufungiwa kwa kanisa la “Kiboko ya Wachawi” pongezi kwa Serikali

Kufungiwa kwa kanisa la “Kiboko ya Wachawi” pongezi kwa Serikali

Sababu walizozitaja mpaka kumfungia ni dhaifu.
Eti kiwango kikubwa cha kumuona , wao kama wasajili wanataka kiwango gani?
Kila nabii na watumishi wengine maarufu hapa Bongo wana kiingilio cha kuwaona sema inakuwa siri . Kiboko ya wachawi tatizo aliweka wazi tofauti na hao wengine.
Nchi hii drama nyingi akienda kuomba msamaha na kukubali kuunga mkono CCM na kumnadi Samia atafunguliwa soon
 
Seeikali imechelewa mno kuchukua hatua. Huyu niliwahi kuandika humu humu Jamii Forum kwamba apewe saa 24 kuondoka nchini na Mali zake zitaifishwe. Arudi Kongo mikono mitupu.
Kwa hio na Mwoposa arudishwe Zambia si ndio?
 
Makanisa yote yana ujanjaujanja sana ndani yake,juzi nimesikia KKKT wamegawanyika na sasa kuna kanisa jipya la KKKT Afrika Mashariki ambalo limeanzishwa na maaskofu waliokuwa KKKT,iyo tisa Kuna shule ambazo wanajenga kwa sadaka za waumini ila muumini masikini hawezi kusomesha mwanae kwasababu ada ni mlima na wala hawasomeshi Bure watoto wa waumini masikini!!
Kkkt ni dhehebu langu ila linaendeshwa kitapta sana, imefika stage hamna tofauti na walokole wanaopiga makelele.
Kuna wainjilisti wengi wanahubiri miujiza.
 
Yule Jamaa watu walikuwa wanamiminika kwake wengne wagonjwa kutoka mikoani hata pakulala hawana af jamaa ikifika mda wakufunga anawatoa waondoke wasije fia pale, basi walikuwa wanawapa sana shida viongozi wa serikali za mitaa wa pale kidagaa kuwaangaikia wagonjwa
 
Inatamani itengeneza akina Mwamposa zaidi ya laki
😂 Yaan wawe km laki hivi ili mafala mafala waendelee kupumbazwa pumbazwa huko na fiksi fiksi za uongo uongo umotivesheno spika wa kutumia Jina la Yesu
 
Hautokuta msikiti ukifanya hivyo, hayo utayakuta kanisani tu.
Hata Makanisani hakuna huo upuuzi, hayo siyo makanisa bali ni vilinge tu vya uganga hata usajili wao huko Wizara ya Mambo ya Ndani vimesajiliwa kama vikundi vya kijamii tu, hao hawahubiri injili bali wanahubiri jinsi ya kutajirika na uponyaji tu.
 
Huyo zile Sadaka zote anazilipia VAT na wale Waumini wanapewa risiti kabisa kila wakituma muamala EFD mashine IPO standby kila mtu ananunua mafuta na maji anakatiwa risiti kutoka TRA kiufupi Jamaa anaiingizia Serikali mapato Ile Siku aliyouza Udongo pale Taifa Serikali iliingiza Pesa nyingi sana TRA kwa kupitia EFD mashine kwani kila kijiko watu walilipia na risiti za EFD walipewa kwa hio Serikali kumfungia mtu km huyu mfanyabiashara mwenye mbwinu ya kucheza na akili za wasioelewa haiwezi kamwe sababu TRA inaingiza mapato mengi kupitia yeye akipiga show tu akajaza watu laki 5 TRA wanachekelea maana Pesa inaingia nyingi
Dah mwamba aliuza mchanga kwa kijiko cha chai 😂 na recipt ya EFD alitoa... 😂😂😂
 
Kumbe wachawi mpo wengi, na mwaka huu wachawi wote mtakufa na uchawi wenu wote utakufa, daima Nuru itashinda Giza. Na huo ndo ukweli, Mungu ana nguvu kuliko shetani huo ndo ukweli, hutaki kajinyonge.
Kiboko ya wachawi huwa anasema wanakufa na hakuna hata mmoja aliyewahi kufa , kelele tu

USSR
 
Sababu walizozitaja mpaka kumfungia ni dhaifu.
Eti kiwango kikubwa cha kumuona , wao kama wasajili wanataka kiwango gani?
Kila nabii na watumishi wengine maarufu hapa Bongo wana kiingilio cha kuwaona sema inakuwa siri . Kiboko ya wachawi tatizo aliweka wazi tofauti na hao wengine.
Nchi hii drama nyingi akienda kuomba msamaha na kukubali kuunga mkono CCM na kumnadi Samia atafunguliwa soon
Hapo ndiyo unaona kabisa kuwa hata Serikali yenyewe inashiriki katika kushamiri kwa huu utapeli. Mtu akishaweka ada ya kumuona moja kwa moja hiyo ni biashara hivyo wasajiliwe kama wafanya biashara na serikali ipate kodi yake, na wasisajiliwe tena Wizara ya Mambo ya Ndani bali wasajiliwe Brela na wakate leseni za kufanya hiyo biashara yao ya utapeli.Kitendo cha serikali kukiri kuwa hao watu wanaweka ada ya kuwaona moja kwa moja imetoa kibali cha watu kupigwa kwani hoja ya kiwango kuwa kikubwa ni kuwa hiyo ni biashara huria kila mmoja anajipangia kiwango chake.
 
Hata Makanisani hakuna huo upuuzi, hayo siyo makanisa bali ni vilinge tu vya uganga hata usajili wao huko Wizara ya Mambo ya Ndani vimesajiliwa kama vikundi vya kijamii tu, hao hawahubiri injili bali wanahubiri jinsi ya kutajirika na uponyaji tu.
Vikundi vya kijamii? Nani anaetoa huo usajiri na hio leseni au kibari anatoa nani? Wizara ya Mambo ya Ndani?
 
Hata Makanisani hakuna huo upuuzi, hayo siyo makanisa bali ni vilinge tu vya uganga hata usajili wao huko Wizara ya Mambo ya Ndani vimesajiliwa kama vikundi vya kijamii tu, hao hawahubiri injili bali wanahubiri jinsi ya kutajirika na uponyaji tu.
Leo unayakana makanisa? Kwani hii mada umeisoma kichwa cha habari?
 
Back
Top Bottom