Kufungua kiwanda Tanzania ni gharama kuliko kuagiza nje, sera ya Tanzania haisapoti viwanda vya ndani

Tatizo sio mapori, shida ipo kwenye akili ya kuyageuza hayo mapori kuwa migodi ya bidhaa mbalimbali ndio changamoto.
Kina mzee Bakhresa na Yule mwingine wa Kagera sugar wanaitwa genge halafu tenda ya kuagiza sukari inapewa kampuni ya kuuza vifaa vya simu!!!!
Yaani wanaiba pesa wanaficha halafu wanataka na wafanyabiashara wafilisike CCM inaonea watanzania
 
Wangeajiri experts kutoka taasisi binafsi watu wa PWC, Delloite ,KPMG, EY au BCG waangalie mfumo mzima wa kodi waishauri serikali, tuache mikopo isiyo na tija tupunguze matumizi yasiyo ya lazima. Tuvutie uwekezaji wa Viwanda
 
Acha mkuu kuna project unataka maji, DAWASA hawataki kuunga mpaka uwahonge ,Tanesco hivyohivyo bahati Mbaya tunapoanza kupanga biashara hatuweki bajeti ya Rushwa!!
Adui wa maendeleo ni wenye mamlaka, na mtu anakuambia kabisa bila mimi hapa we hutoboi , na kweli utawekewa vikwazo na misukosuko mpaka utanyoosha mokono
 
Hadi matajiri wanakuwa CHAWA, mtu kama MO au GSM mabilionea lakini utasikia Mama this Mama That.

Kuna madudu wanatufanyia chini ya pazia, wanamplease ili watu wasishtuke
 
Kina mzee Bakhresa na Yule mwingine wa Kagera sugar wanaitwa genge halafu tenda ya kuagiza sukari inapewa kampuni ya kuuza vifaa vya simu!!!!
Yaani wanaiba pesa wanaficha halafu wanataka na wafanyabiashara wafilisike CCM inaonea watanzania
Ni changamoto sana, halafu hao hao utasikia wanasema Tanzania ina walipa kodi wachache yani 2M out of 61M people. Viwanda hakuna, uzalishaji upo duni,yani kila kitu kigonjwa kuanzia kichwa mpaka miguu.
 
Inategemea na kiwanda, baadhi ni gharama hasa kama Raw material hazitoki Tanzania ila kwa ambavyo raw material na kila kitu inatoka Tanzania vipo ambavyo ni competitive.

Mfano viwanda vya tiles, inyotoka Tanzania ni bei rahisi sana compare na zinazotoka Nje, Mashuka ya Nida, Metl ama kile kiwanda cha Arusha bei rahisi na ni cotton, hata hivyo vitenge na Kanga not necessarily vya nje ni bei rahisi, it's just watengenezaji wa ndani capacity ni ndogo hivyo kupelekea demand kuwa kubwa inadababisha watu waagizishie nje.
 
Ni changamoto sana, halafu hao hao utasikia wanasema Tanzania ina walipa kodi wachache yani 2M out of 61M people. Viwanda hakuna, uzalishaji upo duni,yani kila kitu kigonjwa kuanzia kichwa mpaka miguu.
Hao ni wenye TIN lakini hali ni mbaya kwa wafanyabiashara hasa wa viwanda
 
Hii nchi haina viongozi, waliopo ni watawala tena Wabinafsi, Hebu fuatilia Wizara ya viwanda, halafu angalia wizara ya Uwekezaji ambayo yuko Kitilla Mkumbo, badala ya kulia utaishia kucheka tu
Kati ya kitila mkumbo na mbowe yupo anaakili
 
OK lakini tatizo ni kubwa Sana tolea mfano Sukari wanaozalisha hapa gharama za uzalishaji ni juu ilhali wanalima hapa!!! Sasa nakubaliana nawewe lakini Siyo rahisi Kama ulivyosema una mtaji wa 200M inakuwa heri uagize bidhaa
 
Hii Nchi Nyerere aliacha kwenye mikono ya Wahujumu Uchumi.

Taifa linahujumiwa.

Haiwezekani Unga wa Ngano uwe bei rahisi Ukisafirishwa kutoka Brazili kuliko uliolimwa Njombe.

Yaani Chapati unaila kwa unga kuoka Ukrain kwa bei nafuu lakini sio kwa Unga uliolimwa Tanga au Manyara

Hainiingii akilini hata kidogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…