Kufungua kiwanda Tanzania ni gharama kuliko kuagiza nje, sera ya Tanzania haisapoti viwanda vya ndani

Kufungua kiwanda Tanzania ni gharama kuliko kuagiza nje, sera ya Tanzania haisapoti viwanda vya ndani

Hii Nchi Nyerere aliacha kwenye mikono ya Wahujumu Uchumi.

Taifa linahujumiwa.

Haiwezekani Unga wa Ngano uwe bei rahisi Ukisafirishwa kutoka Brazili kuliko uliolimwa Njombe.

Yaani Chapati unaila kwa unga kuoka Ukrain kwa bei nafuu lakini sio kwa Unga uliolimwa Tanga au Manyara

Hainiingii akilini hata kidogo.
Eti gharama za kusafirisha unga toka Ukraine au Sukari kutoka Brazil ni nafuu kuliko kulima ngano hapa Tanzania au miwa ya mtibwa
 
OK lakini tatizo ni kubwa Sana tolea mfano Sukari wanaozalisha hapa gharama za uzalishaji ni juu ilhali wanalima hapa!!! Sasa nakubaliana nawewe lakini Siyo rahisi Kama ulivyosema una mtaji wa 200M inakuwa heri uagize bidhaa
Sukari ina process nyingi mno, na tupo nyuma kwenye kilimo cha aina yoyote ile, so. Sio mfano mzuri kwamba Sukari ikiwa na bei kubwa basi hatuwezi kutengeneza viwanda vya bei rahisi.

Pia Sukari za nje za bei rahisi hazimaanishi ni Sukari za miwa kama zetu, kuna makemikali na material mengi tu ambayo hutumika kutengeneza Sukari ili kupunguza miwa inayotumika ama hata kutotumia miwa kabisa.
 
Hii Nchi Nyerere aliacha kwenye mikono ya Wahujumu Uchumi.

Taifa linahujumiwa.

Haiwezekani Unga wa Ngano uwe bei rahisi Ukisafirishwa kutoka Brazili kuliko uliolimwa Njombe.

Yaani Chapati unaila kwa unga kuoka Ukrain kwa bei nafuu lakini sio kwa Unga uliolimwa Tanga au Manyara

Hainiingii akilini hata kidogo.
Una mashine na eneo kama lao kulimia? Si kila kitu kinacholimwa nchi X basi kwetu kitastawi kwa ufanisi ule ule.

Tunalima Pamba, Korosho, Mkonge, tumbaku, Mbaazi kwa ufanisi mkubwa tu, je Ukraine nao wanalia kama sisi kwa Nini Tanzania wanalima hivyo na wao hawawezi?
 
Ona sasa tunalima vitu ambavyo hatutumii. Mkonge na pamba.....hahahaa
 
Hata kwenye Sukari, haiwezekani tuagize sukari Brazil wakati mapori ya kutosha yapo Tanzania
Niliweke sawa hilo. "Haiwezekani tuagize sukari toka Brazil wakati tunavyo viwanda vingi tu vya sukari hapa nchini". Sukari toka nje inapunguziwa kodi na pengine inaingizwa bure pasipo kutozwa kadi, wakati sukari ya ndani ina utitiri wa kodi.
 
Wangeajiri experts kutoka taasisi binafsi watu wa PWC, Delloite ,KPMG, EY au BCG waangalie mfumo mzima wa kodi waishauri serikali, tuache mikopo isiyo na tija tupunguze matumizi yasiyo ya lazima. Tuvutie uwekezaji wa Viwanda
Hili nalo ni wazo zuri, wenzetu nchi ziliondelea wana hii kitu. Is why wanapiga hatua.
Complication ninayoina hapa, baadhi ya viongozi hawato taka kuonekana ni incompetent, so watalipiga vita hili. Japo kuwa lina manufaa kwa nchi
 
Ona sasa tunalima vitu ambavyo hatutumii. Mkonge na pamba.....hahahaa
Una uhakika hatutumii?

Kama comment ya juu nimetaja viwanda kama Nida Textiles, Metl, Kiwanda cha mashuka ya shule cha Arusha (nimekisahau jina) wote hawa wanatengeneza bidhaa ambazo zinauzwa soko la ndani, kuanzia mashuka, blanket, kanga, vitenge mpaka Uniform za majeshi.
 
Kwa hiyo kwa kuwa aliyesema maneno hayo ni balozi wa nje basi ni lazima kuna ukweli 100percent kwa faida ya Tanzania ?!!!

Haya mkuu.....
 
Huu ni ukweli usiopingika. Serikali ya kishetani ya CCM siku zote inawaza kukamua kodi tu. Sijawahi kuona serikali ya kiquma kama hii ya CCM hapa ulimwenguni.
Serikali zote za duniani unazijua kwa kuwa umeishi huko ,umeziishi hizo serikali ,umefanya nazo shughuli ama ?!! [emoji1787][emoji1787]
 
Nimemsikiliza balozi wa Uingereza nchini Tanzania anayemaliza muda wake David Concur anasema wazalishaji wengi wa Tanzania wanashindwa kulihudumia soko la ndani kwa sababu bidhaa za kuagiza ni nafuu zaidi. Hii inasababisha viwanda vichache kufunguliwa na kupelekea upungufu wa ajira.

Mfano mzuri, ni vitenge vinavyozalishwa hapa nchini bei yake ni juu kuliko vinavyoagizwa nje hii inamaanisha gharama za uzalishaji Tanzania ni kubwa kupitiliza.

Ukienda kariakoo, na masoko yote makubwa utagundua bidhaa nyingi zinatengenezwa China. Hata vifaa Kama furniture vinatokea China ilhali mazao ya misitu yanatoka huku Africa.

Tunashindwa nini kuongeza uzalishaji? Sera mbovu!, nini kifanyike tuwajengee uwezo wazawa na wageni kuweka viwanda nchini.

TIC inajitahidi kuhamasisha uwekezaji lakini ni lazma ziwepo jitihada za makusudi kurekebisha Sera zetu. Nchini China, Taiwan, India au Korea uchumi wa viwanda unachangia Sana pato la taifa.

4R HOYEE

Shida ya watawala wa Tanzania matatizo wanayafahamu ila hawataki kuyatatua!!
 
Uwezekano ni wafanyabiashara wakubwa wa uchuuzi either ni wanasiasa au ni washirika wa wanasiasa. Katika mazingira haya, wahusika hawataki stress za uzalishaji, wanataka pesa za chap chap. Ameleta yebo yebo amepakua hapo bandarini, wachuuzi wamenunua, ametengeneza faida. Mambo ya ajira hilo si kipaumbele, kipaumbele ni faida chap chap. Mazingira ya kisiasa yenyewe hayatabiriki, anaweza kuja raisi akaamua la kuamua kiwanda kikawa rehani.
Huko sahihi ndio maana serikali inajenga soko kubwa Ubungo kwa ajili ya wachuuzi,, mgomi wa kariakoo uliendeshwa na wachuuzi.
Uwezekano ni wafanyabiashara wakubwa wa uchuuzi either ni wanasiasa au ni washirika wa wanasiasa. Katika mazingira haya, wahusika hawataki stress za uzalishaji, wanataka pesa za chap chap. Ameleta yebo yebo amepakua hapo bandarini, wachuuzi wamenunua, ametengeneza faida. Mambo ya ajira hilo si kipaumbele, kipaumbele ni faida chap chap. Mazingira ya kisiasa yenyewe hayatabiriki, anaweza kuja raisi akaamua la kuamua kiwanda kikawa rehani.
Upo sahihi serikali inajisifu kujenga soko kubwa Ubungo kwa ajili ya wachuuzi, hata mgomo wa kariakoo uliendeshwa na serikali na wachuuzi.
 
Nimemsikiliza balozi wa Uingereza nchini Tanzania anayemaliza muda wake David Concur anasema wazalishaji wengi wa Tanzania wanashindwa kulihudumia soko la ndani kwa sababu bidhaa za kuagiza ni nafuu zaidi. Hii inasababisha viwanda vichache kufunguliwa na kupelekea upungufu wa ajira.

Mfano mzuri, ni vitenge vinavyozalishwa hapa nchini bei yake ni juu kuliko vinavyoagizwa nje hii inamaanisha gharama za uzalishaji Tanzania ni kubwa kupitiliza.

Ukienda kariakoo, na masoko yote makubwa utagundua bidhaa nyingi zinatengenezwa China. Hata vifaa Kama furniture vinatokea China ilhali mazao ya misitu yanatoka huku Africa.

Tunashindwa nini kuongeza uzalishaji? Sera mbovu!, nini kifanyike tuwajengee uwezo wazawa na wageni kuweka viwanda nchini.

TIC inajitahidi kuhamasisha uwekezaji lakini ni lazma ziwepo jitihada za makusudi kurekebisha Sera zetu. Nchini China, Taiwan, India au Korea uchumi wa viwanda unachangia Sana pato la taifa.

4R HOYEE

Ni kweli kabisa Ndugu yangu
 
Hapo sasa!
 
Attachments

  • images (28).jpeg
    images (28).jpeg
    47.6 KB · Views: 2
  • Screenshot_2024-07-16-11-18-26-538_com.whatsapp.jpg
    Screenshot_2024-07-16-11-18-26-538_com.whatsapp.jpg
    289.6 KB · Views: 2
Naona Kila mtu ana lalamika, tupendekeze suluhisho..unaposema sera irekibishwe be specific sera ipi

Binafsi naona production cost ni kubwa kuwa sababu ya bei ya umeme, umeme Tanzania ni ghali sana,

Pili, Kodi ziondolewe kwa mashine za kuongeza thamani za bidhaa

Na mwisho Mazingira ya kuagiza mashine za kati pamoja na malighafi uboreshwe, uwe na uwazi na rahisi, kusiwe na monopoly au mtu kati,
 
Girland:
Acha mkuu kuna project unataka maji, DAWASA hawataki kuunga mpaka uwahonge ,Tanesco hivyohivyo bahati Mbaya tunapoanza kupanga biashara hatuweki bajeti ya Rushwa!!
Nyie hamuelewi kitu kinaitwa contigency? Au other expenses?
 
Back
Top Bottom