Kufungua kiwanda Tanzania ni gharama kuliko kuagiza nje, sera ya Tanzania haisapoti viwanda vya ndani

Production cost ziko juu maana wanasiasa wanawaza maisha Yao na sio maendeleo ya Taifa zima.

Watanzania wako utumwani, nguvu zao na akili zao zimetwaliwa kutumikia mabwanyenye walioifanya siasa kuwa ajira inayolipa.
 
sawa, nataka kuimport mashine ya kutengeneza misumari, naomba unioneshe link ya kukadiria Kodi ,
 
Hivi kile kiwanda cha jeans pale EPZ (External Mabibo, Dar) wameshindwa/wamegoma kabisa kututengenezea jeans za hadhi yetu sisi waTZ ili angalau na sisi tupendeze kidogo?
 
Hivi kile kiwanda cha jeans pale EPZ (External Mabibo, Dar) wameshindwa/wamegoma kabisa kututengenezea jeans za hadhi yetu sisi waTZ ili angalau na sisi tupendeze kidogo?
Wale wanazalisha for export only. Yaani angalau 80% ya products zao Lazima zile exported.
 
Wale wanazalisha for export only. Yaani angalau 80% ya products zao Lazima zile exported.
Yes. Hoja yangu ni kwamba kwenye uwekezaji wao wangezalisha kiasi fulani kwa ajili ya soko la ndani. Sidhani kama wangepata hasara by creating such a niche market.
 
Uko sahihi.
Hakuna stability/sustainability thus why wafanya biashara wakubwa wa Tanzania wanawekeza pia kwenye nchi zingine kwa ajili ya dharula likitokea lolote anahamia kwenye nchi nyingine.
 
Mfano sisi tumeletewa barua na NSSF wanataka Audit ya miaka 3 nyuma.
Wakijua sisi tuna uwezo wa kununua Auto machine na kuondoa kazini watu 20 wakabaki 7 tu
 
Man just give up, those information should be available in public sio kwa kusaidiwa
Taarifa zote mzee ziko online, ni kwamba haujui and you don’t want to learn. Makampuni yote düniani yana specific departments to navigate through these issues and for compliance purposes. Shida yetu Tanzania biashara tunafanya wenyewe utake kujua sheria wewe, marketing wewe, production wewe, kuagiza mzigo nje wewe, kulalamika mitandaoni wewe, nk Anyway All the best.

Na wewe unaona ni kusaidiwa wakati hapa duniani kuna watu biashara zao ni hizi, kuna clearing and Forwarding agents, kuna consultants kibar n.k. Wameestablish biashara za maana out of this.
 
Land cruiser ambazo zinatakiwa zibebe watalii hiyo kodi yake ni balaa kinachotokea wageni wanabebwa kwenye Cruiser zile banzi au Land rover za kitambo ambazo hatuna uhakika wa kutoboa Serengeti kwa sababu ya kodi kubwa badala ya kupunguza kodi kwenye hayo magari wao wameyachukulia kama anasa Nchi ya ajabu sana hii..
 
hahaha Asante sana mzee, nimekuelewa

ila hata kulalamika mitandaoni unahitaji kuajiri watu kweli ? hata hivyo sijalalamika in this thread, bali nime point out changamoto zilizopo na kutoa mapendekezo yangu tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…