Kufungua kiwanda Tanzania ni gharama kuliko kuagiza nje, sera ya Tanzania haisapoti viwanda vya ndani

Kufungua kiwanda Tanzania ni gharama kuliko kuagiza nje, sera ya Tanzania haisapoti viwanda vya ndani

Production cost ziko juu maana wanasiasa wanawaza maisha Yao na sio maendeleo ya Taifa zima.

Watanzania wako utumwani, nguvu zao na akili zao zimetwaliwa kutumikia mabwanyenye walioifanya siasa kuwa ajira inayolipa.
 
Asante kwa swali zuri,

Unachotaliwa kufahaku ni kuwa gharama kubwa kwenye utengenezaji wa nondo na bidhaa zake ni upatikanaji wa raw materials. Kwa sasa chuma tunakitoa Misri baada ya uzalishaji wa South Africa kutuma baada ya Covid. Chuma ni gharama na pia kina import duty kwa kuwa hatuko kwenye jumiya nayo Kama ilivyo EAC na SADC. Just to note, gharama za chuma ziliongezeka Dunian after COVID.

lakini unavyosema nondo zimepanda sana bei unamaanisha nini, against what, Je nondo kwenye nchi nyingine bei zake zipoje??? Haujui kuwa mfumuko wa bei duniani umeathiri bidhaa Karibia zote?

Mfano kuna mdau Jana alichangia kuhusu bei ya Sukari kuwa chini Malawi, lakini ukiangalia mwaka huu Malawi bei ya Sukari ilifikia kwacha 3800 ambayo ni Karibu 6000 ya TZ. na Bado average price ni Kwacha 2200 ambayo ni zaidi ya bei ya Sukari hapa kwetu. Bei ya mafuta TZ ni Ndogo Kuliko Kenya n.k ni muhimu watanzania hasa tulio Mitandaoni kutafuta taarifa sahihi kuhusu nchi yetu.
sawa, nataka kuimport mashine ya kutengeneza misumari, naomba unioneshe link ya kukadiria Kodi ,
 
Hivi kile kiwanda cha jeans pale EPZ (External Mabibo, Dar) wameshindwa/wamegoma kabisa kututengenezea jeans za hadhi yetu sisi waTZ ili angalau na sisi tupendeze kidogo?
 
Hivi kile kiwanda cha jeans pale EPZ (External Mabibo, Dar) wameshindwa/wamegoma kabisa kututengenezea jeans za hadhi yetu sisi waTZ ili angalau na sisi tupendeze kidogo?
Wale wanazalisha for export only. Yaani angalau 80% ya products zao Lazima zile exported.
 
Wale wanazalisha for export only. Yaani angalau 80% ya products zao Lazima zile exported.
Yes. Hoja yangu ni kwamba kwenye uwekezaji wao wangezalisha kiasi fulani kwa ajili ya soko la ndani. Sidhani kama wangepata hasara by creating such a niche market.
 
Uwezekano ni wafanyabiashara wakubwa wa uchuuzi either ni wanasiasa au ni washirika wa wanasiasa. Katika mazingira haya, wahusika hawataki stress za uzalishaji, wanataka pesa za chap chap. Ameleta yebo yebo amepakua hapo bandarini, wachuuzi wamenunua, ametengeneza faida. Mambo ya ajira hilo si kipaumbele, kipaumbele ni faida chap chap. Mazingira ya kisiasa yenyewe hayatabiriki, anaweza kuja raisi akaamua la kuamua kiwanda kikawa rehani.
Uko sahihi.
Hakuna stability/sustainability thus why wafanya biashara wakubwa wa Tanzania wanawekeza pia kwenye nchi zingine kwa ajili ya dharula likitokea lolote anahamia kwenye nchi nyingine.
 
Mfano sisi tumeletewa barua na NSSF wanataka Audit ya miaka 3 nyuma.
Wakijua sisi tuna uwezo wa kununua Auto machine na kuondoa kazini watu 20 wakabaki 7 tu
 
Man just give up, those information should be available in public sio kwa kusaidiwa
Taarifa zote mzee ziko online, ni kwamba haujui and you don’t want to learn. Makampuni yote düniani yana specific departments to navigate through these issues and for compliance purposes. Shida yetu Tanzania biashara tunafanya wenyewe utake kujua sheria wewe, marketing wewe, production wewe, kuagiza mzigo nje wewe, kulalamika mitandaoni wewe, nk Anyway All the best.

Na wewe unaona ni kusaidiwa wakati hapa duniani kuna watu biashara zao ni hizi, kuna clearing and Forwarding agents, kuna consultants kibar n.k. Wameestablish biashara za maana out of this.
 
Land cruiser ambazo zinatakiwa zibebe watalii hiyo kodi yake ni balaa kinachotokea wageni wanabebwa kwenye Cruiser zile banzi au Land rover za kitambo ambazo hatuna uhakika wa kutoboa Serengeti kwa sababu ya kodi kubwa badala ya kupunguza kodi kwenye hayo magari wao wameyachukulia kama anasa Nchi ya ajabu sana hii..
 
Taarifa zote mzee ziko online, ni kwamba haujui and you don’t want to learn. Makampuni yote düniani yana specific departments to navigate through these issues and for compliance purposes. Shida yetu Tanzania biashara tunafanya wenyewe utake kujua sheria wewe, marketing wewe, production wewe, kuagiza mzigo nje wewe, kulalamika mitandaoni wewe, nk Anyway All the best.

Na wewe unaona ni kusaidiwa wakati hapa duniani kuna watu biashara zao ni hizi, kuna clearing and Forwarding agents, kuna consultants kibar n.k. Wameestablish biashara za maana out of this.
hahaha Asante sana mzee, nimekuelewa

ila hata kulalamika mitandaoni unahitaji kuajiri watu kweli ? hata hivyo sijalalamika in this thread, bali nime point out changamoto zilizopo na kutoa mapendekezo yangu tu.
 
Back
Top Bottom