Kama kweli Rais kadhamilia kufungua vyuokwa hali ilivyo sasa hivi, waalimu jiandaeni. Taarifa za kitaalamu ni kwamba Vijana wanapambana na ugonjwa huu vizuri kuliko wazee. Madarasa ya vyuo vyetu ni kama kambi. wanafunzi hujaa hadi pomoni na wengine hukosa kabisa nafasi ya kukaa. Mgonjwa mmoja anatosha kuambukiza darasa zima kwa siku moja tu!
Waalimu wa vyuo walio wengi wako kwenye umri hatarishi kwa corona na hawa ndo watakaokutana na vijana ambao sasa watatoka majumbani kwao na kusafiri nchi nzima. Nionavyo waalimu jiandaeni kupigwa na corona.
Inasikitisha, maana wanasiasa kule Bungeni na hata maofisini na huko ikulu, wanaogopa mikusanyiko lakini wako tayari kuwajaribia vijana wetu na wataalamu wetu kuanza kuchanganyikana kwenye madarasa ambayo yalishazidiwa wingi wa wanafunzi.