Kufungua vyuo ni kuwajaribia vijana wetu na kuwamaliza waalimu vyuoni

Corona haiishi leo wala Kesho bro wacha wanafunzi warudi chuo tu hakuna namna inabidi tujifunze kuishi na Corona tu
 
Wale wa UDOM zile theater za CoED kwa masomo ya edu huwa panajaa kupita kias hakuna ata air circulation, yan mule ni nyungu tosha hasa muda wa mchana. may be mkatumie zile cafetheater za humanities..
 
nina dogo ndo anaenda kumalizia semister UDSM,sijui nifanyeje daah jiwe atatuulia watoto
 
Tuko mitaani tunapigiana simu, tunaandikiana sms na kujuliana hali na hasa hii corona. Ninachokiona, wananchi wamebuni tabia ya ziada kujikinga na corona. Hawaendi hospitali kutokana na huduma mbovu/mbaya! Kwa tabia hii, sasa serikali haina taarifa sahihi za wagonjwa wa Corona!

Na bahati mbaya rais anategemea taarifa za wagonjwa waliolazwa hospitalini. Nionavyo sasa kuenea kupitia vyuoni na mashuleni kunakuja.
btw. Huko Arusha vipi????
 
Wangekuwa wale wa Enzi za kina Kitila Mkumbo tungekuwa tuna matumaini ya kupata uhalisia wa ugonjwa huu maana angeugua mmoja kwa maambukizi yatakayosababishwa na wao kurudi vyuoni wangekinukisha ila hawa wa sasa hivi mhhhh.
 
Wangesubiri muda kidogo hata mwezi mwingine kuona inakuaje Elimu zipo tuu ila uhai sio wa kujaribu kabisaa...sema ni vile Afrika uhai wanauchukulia poa tuu ndio maana wanaamua maamuzi yeyote...
 
Wewe vipi? Unawezaje kusema ni mdogo wakati umeua makumi ya maelfu ya watu kote duniani? Be serious.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zaidi ya shule 250 nchini Korea Kusini zimefungwa tena siku chache baada ya kufunguliwa, huku shule 117 zikisitisha mpango wa kufungua kutokana na visa vya #COVID19 kuanza kuongezeka. Nchi hiyo imeanza kulegeza masharti yaliyowekwa kukabiliana na virusi vya corona. Swahili Times on Twitter
 
Akili mbovu za namna hii mnazitoa wapi kuanzisha uzi.....? Sisi sote tunashukuru kuwa sasa hatutapoteza mwaka wa masomo....!! Korona ipo tuhimizane kujihadhari nayo....yaani nawa mikono , Barakoa ,sanitaiza, observe distance etc ,Wajameni korona sio ebola...tusipotezeane malengo kwa mitazamo ya kisiasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…