Kufutwa kwa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo ni dharau kwa Rais Kikwete na watu wa Pwani

Umeongea vizuri ila hapo mwisho Magu kachukua points zoote. Kwani miaka kumi yoote Kikwete alikuwa wapi?
 
Zama zimesha badilika ndugu yangu china na miaka ile sio ya sasa kwa sasa ni profit After profit
 
China Debt Trap ni hatari kuna mataifa yanalia
Wachina wanakujengea miradi mikubwa kwa pesa yao alafu wanaanza kukudai kabla hawajakukabidhi hakuna rangi utaacha ona
Kwahiyo Chato itachukuliwa na wachina siku za usoni
 
Kila awamu na taratibu zake
Taratibu za awamu Hii ni kutumia TRA kuwabambikia kodi kubwa wafanyabiashara kisha kuwafungia Account zao kupora pesa zao kienyeji kwa njia haramu huku wakiziathiri Bank kwa kukosa imani toka kwa wateja wao ambao wanaona Benk siyo sehemu salama ya kuhifadhi pesa zao
 
Wamepoteza mabilioni kulipa watu fidia kubwa wahame kuipisha hiyo Bandari lakini hizo pesa zimepotea bure
 
Dharau kubwa sana. Washamba wamepewa nchi...
Kazi wanayojua sasa ni kufunga biashara Account kuwabambikia kodi kubwa wafanyabiashara wapate kuwapora fedha zao kwa njia haramu, wanayaua mabenk watu wanaacha kuweka pesa Benk za Tanzania wanaenda nje kuficha pesa zao
 
China Debt Trap ni hatari kuna mataifa yanalia
Wachina wanakujengea miradi mikubwa kwa pesa yao alafu wanaanza kukudai kabla hawajakukabidhi hakuna rangi utaacha ona
Kwani kutumia mifano ya Nchi zingine si unatengeneza mkataba unaokulinda ukizuia kudaiwa hovyo hovyo kienyeji pasipo kufuata makubaliano
 
Umeongea vizuri ila hapo mwisho Magu kachukua points zoote. Kwani miaka kumi yoote Kikwete alikuwa wapi?
Kikwete alijenga Nchi nzima lakini mtukufu yeye anakomaa kujenga chato pekee kwingine hataki
 
Pesa nyingi imetumika kufanya upembuzi yakinifu kuwalipa wakazi fidia lakini mwisho wa siku imekwenda bure kabsa ni aina mbaya ya matumizi mabaya ya pesa za umma
 
Bandari za Tanga, Dar es salaam & Mtwara zikiboreshwa zinatosha.

(kwa kupanuliwa, kuongezwa kina & mifumo ya kiutendaji)
Kama vile viwanja vya ndege vya Mwanza na Bukoba vingeimarishwa vingetosha.
 
Miradi ya mh Kikwete inaukakasi sana,gas ni mfano mkubwa,tz kama nchi mradi wa bandari bagamoyo unafaida gani? siyo ujengwe tu, hayo masharti huyaoni?
 
Miradi ya mh Kikwete inaukakasi sana,gas ni mfano mkubwa,tz kama nchi mradi wa bandari bagamoyo unafaida gani? siyo ujengwe tu, hayo masharti huyaoni?
 
Kikwete Alishindwa Nini Kujenga Hiyo Bandari?
Binafsi Sioni faida ya hiyo bandari zaidi ya kuiua bandari ya Dsm
Faida ya uwanja Chato at the same time linajengwa daraja la busisi unaiona??
 
Miradi ya mh Kikwete inaukakasi sana,gas ni mfano mkubwa,tz kama nchi mradi wa bandari bagamoyo unafaida gani? siyo ujengwe tu, hayo masharti huyaoni?
Wachina hao hao wanamwaga mabilioni yao kukijenga Kijiji cha Chato. Hakuna masharti?
 
Kwani kutumia mifano ya Nchi zingine si unatengeneza mkataba unaokulinda ukizuia kudaiwa hovyo hovyo kienyeji pasipo kufuata makubaliano
Hata kukataa haikuwa kosa pia yote ni heri
 
Pesa nyingi imetumika kufanya upembuzi yakinifu kuwalipa wakazi fidia lakini mwisho wa siku imekwenda bure kabsa ni aina mbaya ya matumizi mabaya ya pesa za umma
Heri nusu shari lakini
 
Yaani Watanzania wauze sehumu kwa wachina kwa kunufaisha watu tu wakati wananchi hata sehemu za kuchunga hawana. Unajua kwenye mkataba Mchina angekuwa na haki kwa hiyo bandari kama vile ni nchi yao ! Yaani unaweza kuzuiwa kuongia huko sasa hii itasaidia vipi bagamoyo? Ni vifaa gani vya ujenzi vinatoka Tanzania? Wachina walikuwa wajenge magodauni ya kuwekea vitu kutoka kwao
 
Ni vizuri ungeeleza zile faida unazoziona kwamba tumezipoteza maana ktk kuufuta mradi huu tulielezwa mapungufu yake na sisi wengine tulielewa kwamba haukuwa na faida kwa watanzania zaidi ya kwamba ulikuwa ni hasara kwani kutekelezwa kwa mradi huu kulikuwa kunaenda kuzuia maendelezo ya bandari katika ukanda wote wa pwani
unaozunguka eneo la bahari hindi ndani tanzania hii ni moja na pili ni kwamba makusanyo yote Kwa 100% yatokanyo na hiyo bandari yalipaswa kuingia ktk mfuko wa huyo tuliyekuwa tunamwita mwekezaji na hii ni kwa muda wa miaka mia

hii tulielezwa na tulimsikia Rais Magufuli akiielezea kwa hasira na hisia kali zilizojaa uchungu wakati akitangaza kuusimamisha mkataba huo wa ujenzi wa bandari

Kwa malezo ya Rais kwamba ni kwa nini aliufuta huo mradi sisi wengine tulimwelewa kwamba mradi haukuwa unawanufaisha watanzania zaidi ya kwamba ulikuwa na faida kwa upande mmoja ambao ni wachina

sasa hapa wewe umekuja na habari kwamba mradi ulikuwa ungewafaudsha watanzania wenzetu ambao ni watu wa bagamoya na na kwamba ni dharau kwa aliyekuwa rais wa awamu ya 4 na ambaye anatokea bagamoyo
Kwa maoni yangu ni kwamba haitoshi tu kusema hivyo ila zaidi kwamba unatakiwa kueleza ni faida gani wangepata watu wa bagamoyo na Tanzania kwa ujumla wake na pia utueleze ni kwa namna gani alivyodharauliwa Rais wa awamu ya nne
Kwa hapa binafsi namsifu Rais magufuli kwa uamuzi aliochukua kuufuta huu mradi
Hongera Rais Magufuli kwani uliangalia masilahi mapana ya Tamzania bila kujali ni nani alisaini mkataba ambao ungekuwa ni maumivu na unyonyaji wa
muda mrefu kwa taifa la Tanzania

kwa hapa ndugu yangu mtoa mada sikuelewi ama pengine uniambie kwamba na wewe ulikuwa ni mnufaika binafsi wa huu mradi na ndiyo maana umeleta mada bila kujali maslahi mapana ya nchi na wananchi kwa ujumla wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…