Kufutwa kwa mradi wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo ni ujumbe wenye taarifa kamili kwamba awamu ya tano inadharau mipango na miradi mizuri iliyoanzishwa na awamu ya 4.
Lkn pia, hatua hii inaua ndoto na matumaini ya kupunguza umaskini kwa watu wa Pwani kupitia mradi huu ambao ulipambaniwa na kufanikisshwa na mpwani mwenzao (rais wa awamu ya 4).
Mbona Chato kunajengwa viwanja vya ndege nje kabisa ya bajeti hatusemi?
Mbona Chato kunajengwa maghorofa yanayokaliwa tu na popo hatusemi?
Mbona Chato kunawekwa mataa barabarani zinazoishia kuongoza mikokoteni hatusemi?
Hii siyo dharau kwa rais Kikwete na watu wa Pwani?
N.B Bado hawajasahau majibu ya nyodo waliopewa walipo omba kiwanda cha kusindika nanasi: "rais wa awamu ya 4 anatoka hapa na analima nanasi, hakujenga. Mlisubiri mm niwe rais ndiyo nije nijenge?"
Ni vizuri ungeeleza zile faida unazoziona kwamba tumezipoteza maana ktk kuufuta mradi huu tulielezwa mapungufu yake na sisi wengine tulielewa kwamba haukuwa na faida kwa watanzania zaidi ya kwamba ulikuwa ni hasara kwani kutekelezwa kwa mradi huu kulikuwa kunaenda kuzuia maendelezo ya bandari katika ukanda wote wa pwani
unaozunguka eneo la bahari hindi ndani tanzania hii ni moja na pili ni kwamba makusanyo yote Kwa 100% yatokanyo na hiyo bandari yalipaswa kuingia ktk mfuko wa huyo tuliyekuwa tunamwita mwekezaji na hii ni kwa muda wa miaka mia
hii tulielezwa na tulimsikia Rais Magufuli akiielezea kwa hasira na hisia kali zilizojaa uchungu wakati akitangaza kuusimamisha mkataba huo wa ujenzi wa bandari
Kwa malezo ya Rais kwamba ni kwa nini aliufuta huo mradi sisi wengine tulimwelewa kwamba mradi haukuwa unawanufaisha watanzania zaidi ya kwamba ulikuwa na faida kwa upande mmoja ambao ni wachina
sasa hapa wewe umekuja na habari kwamba mradi ulikuwa ungewafaudsha watanzania wenzetu ambao ni watu wa bagamoya na na kwamba ni dharau kwa aliyekuwa rais wa awamu ya 4 na ambaye anatokea bagamoyo
Kwa maoni yangu ni kwamba haitoshi tu kusema hivyo ila zaidi kwamba unatakiwa kueleza ni faida gani wangepata watu wa bagamoyo na Tanzania kwa ujumla wake na pia utueleze ni kwa namna gani alivyodharauliwa Rais wa awamu ya nne
Kwa hapa binafsi namsifu Rais magufuli kwa uamuzi aliochukua kuufuta huu mradi
Hongera Rais Magufuli kwani uliangalia masilahi mapana ya Tamzania bila kujali ni nani alisaini mkataba ambao ungekuwa ni maumivu na unyonyaji wa
muda mrefu kwa taifa la Tanzania
kwa hapa ndugu yangu mtoa mada sikuelewi ama pengine uniambie kwamba na wewe ulikuwa ni mnufaika binafsi wa huu mradi na ndiyo maana umeleta mada bila kujali maslahi mapana ya nchi na wananchi kwa ujumla wake.