Sikupata muda wa kutazama mechi ya leo dhidi ya Libya.
Kama mtanzania huru na mzalendo acha niseme kidogo. Nimeona mjadala kuhusu mchango wa Samata kwenye timu ya Taifa, naomba nipige msumari hapo hapo haya ya matokeo siyazungumzii.
Kwa miaka mingi tumekosa wachezaji haiba ya Samata hapa nchini, ni wazi toka tupate uhuru ndiye mchezaji aliyecheza soka la mafanikio kuliko yeyote yule. Samata huonekana machoni mwa wengi kuwa ni bora huwenda tu anawapumbaza na vitu vichache ambavyo kwa macho ya mihemko huwezi kuvigundua.
Lazima tukubali kuwa tuna captain ambaye hana uchungu na timu yake, hana uchungu na taifa lake ila ana uchungu na hicho klabu chake ambacho kimemjaza sifa hadi kuona Taifa Stars ni ya kuchezea huku unalinda kuumia. Kuna sehemu za huyu kijana kufanyia mzaha ila siyo kwenye timu ya taifa. Kama anaogopa kupata majeraha kisa klabu yake basi atoke timuni.
Tunashindwa kumuimba Msuva kisa giza la huyu kijana ambaye mabega yake hataki yaumie kisa hofu ya majeraha! Tuna vichezaji vya hovyo sana kwenye hili taifa.
Huo upatu anaopigiwa kwenda EPL aende kwa mpira upi huo ambao utaduwaza wazungu. Ni mpira upi ambao hauchezi kwenye timu ya taifa na anataka aupeleke England?
Sijawahi kukubali na sitokuja kukubali kuwa Samata ni mchezaji bora Tanzania, labda niwe nimewehuka akili ishindwe kupambanua mambo.
Wekeni rangi 4 za bendera yetu mabegani mwenu kama Msuva, Yondani na wengine wafanyavyo. Siyo kupaka rangi mpira kwa sifa za kijinga. Ukweli mzito ambao Samata hawezi kuamini ni kuwa mpira wake hauwezi kufika hata nusu ya mpira achezao Msuva.
Captain Captain Captain kitu gani!