Kuhama kutoka Tamisemi kwenda Taasisi ya Serikali kwa kufanya usaili

Nini ilikuwa changamoto. Share experience.

Nmejaribu mara mbili, mara ya kwanza nikiwa na miezi 7 kazini sikuomba ruhusa popote nikafika oral kabisa na nikaifanya ila sikuitwa, mwaka huu pia nmeenda taasisi ingine tena kufanya usaili mwezi wa nane nikafika oral ila mpaka sasa sijaitwa.

Kikubwa ni kwamba ukiwa mtumishi wanahitaji uwe na ruhusa ya mwajili wako( kwenye ile barua ya kuomba nafasi uipitishe kwa mwajiri).

Changamoto ipo hapo, binafsi nmemfuata mwajiri zaidi ya mara 6 kagoma kupitisha barua ingawa upande fulani namuelewa sababu sijatimizia miaka mitatu katika kituo nilichopo ila hata waliopo ( wakongwe) wanalalamika sana kupata idhini ya mwajiri, tamisemi wanakaza sana
 
Asante kwa mrejesho. Upo sahihi, kama hujamaliza miaka mitatu kazini huwezi kuhama kituo.

Pia kwa sasa ukiwa mwajiriwa wa serikali huwezi kuomba nafasi za entry level tena. Kuna waraka umekataza. Unaweza tu kuomba nafasi za kuhamia zinazotangazwa na PSRS.
 
Mpak
Hivi kama.inapitishwa kwa Mwajiri wako afu hiyo kazi ukaikosa huwa unaendelea kubaki hapohapo Mkuu!?
Mpaka upate. Utaendelea kubaki kwenye kituo chako cha kazi. Kwa sasa mwajiriwa anaruhusiwa kuomba kazi iwapo ni ya nafasi za kuhamia kwa kada yake ya sasa au kama ni entry level awe anataka kuomba recat; mfano mhasibu amesomea ufamasia ndio anaweza kuomba entry level ya ufamasia ila sio ya uhasibu tena.
 
Andika barua kwa katibu mkuu utumishi kupitia kwa DED kuomba uhamisho, ambatisha hiyo barua ya ajira mpya.Muone DED ana kwa ana mwambie ukweli nina hakika atapitisha barua yako kisha itume Dodoma kwa katibu mkuu utumishi, subiri ndani ya miezi mitatu hadi mitano utapata uhamisho.
Mkuu sahizi Mambo c mfumo
 
Asante kwa mrejesho. Upo sahihi, kama hujamaliza miaka mitatu kazini huwezi kuhama kituo.

Pia kwa sasa ukiwa mwajiriwa wa serikali huwezi kuomba nafasi za entry level tena. Kuna waraka umekataza. Unaweza tu kuomba nafasi za kuhamia zinazotangazwa na PSRS.
Hapa unamaana kuwa Mtumishi haruhusiwi kuomba nafasi kwa kada ile au nyingine kama Ajira mpya sio!?
 
Unaruhusiwa kuomba kada nyingine (tofauti na yako kwa sasa) kwa entry level. Mfano wewe ni mwalimu ila ukasomea degree nyingine ya uhasibu. Unaweza kuomba nafasi ya uhasibu kwa entry level inakubalika. Ila mhasibu wa TAMISEMI hawezi kuomba nafasi ya uhasibu TRA kama entry level.
 
Shukrani sana Kaka Ubarikiwe
 
Back
Top Bottom